Mkuu hapa njia moja kubwa ni wewe kuumiza kichwa kumkamata mmoja wa wazalishaji akubali kukupa mpango mzima. Na dawa ni moja tuu mlungula au cash, lakini usiende kienyeji enyeji utapoteza pesa na hupati recipe. Cha kufanya kwanza poteza muda kuisoma business yenyewe kwa nje nje macro analysis, angalia washindani wako, angalia weakness (udhaifu) wa product zote kwenye soko, angalia kama ukipata hiyo secret source utajiposition vipi kukamata % ya soko. Wakati ushapoteza muda huo na kwamba umehakiki unafahamu soko lote na umejua udhaifu wa product zilizo sokoni, sasa weka mkakati (strategy) wa kutafuta dhaifu mzalishaji (weaker) ambae atakubaliana na wewe either wa kupartner na wewe sababu unakuja na cash and technical know-how ya kuingia sokoni, au umnunue mtu kabisa wewe utengeneze mchakato mzima.
Mafuta ya nywele mimi pia natolea macho, hasa ambayo ni natural ingredients yasiyo na artificial chemicals. Kingine sababuni za kuogea na shampoo vyote liquid hii nayo naitolea macho.