Ushahidi wa Vyama mamluki kuhongwa ili kuishambulia Chadema Kuwekwa hadharani

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
118,374
219,749


Baada ya Chama Kikuu kabisa cha siasa nchini Tanzania, CHADEMA, kutangaza tarehe ya Maandamano, huku Wananchi kwa Mamilioni wakionyesha kuunga Mkono na kutangaza kushiriki, Kumeibuka kikundi cha Wachumia Tumbo wanaojiita viongozi wa vyama vya siasa waliotangaza kupinga mpango huo kabambe wa kidemokrasia.

Zipo tetesi kwamba Mamluki hao wamehongwa, huku taarifa zingine zikisema kwamba baadhi yao walionekana jana kwenye maduka ya nguo wakinunuliwa Suti kwa ajili ya Mkutano wao na waandishi wa Habari ulioandaliwa na "Watu wa serikali"

Timu yetu ya uchunguzi itaanika ukweli wote hapa hapa, namna Mamluki hao walivyohongwa hela ndogo ili kuja kupotosha .

Usiondoke JF
 
Achaneni na hawa wapumbavu
 
@Erythrocyte Kwa nini umekimbilia kuandika tetesi badala ya kusubiri taarifa iliyokamilika?
Kama hukuweza kuuanika ukweli unaodai kuwa nao leo,huo mwingine utaupata wapi?
Hao mamilioni ya watanzania waliokuahidini kuwaunga mkono ebu tuwekee mfano wake hapa?
Tatizo Chadema mlidekezwa na Samia na mkavimba bichwa mkiwadharau wanasiasa wengine.
Juzi hapa mliwafanyia Uhuni "Sauti ya Watanzania"mkawaahidi kuwapa ushirikiano na zilipokaribia siku ya kuwaruhusu kufanya maandalizi ya mkutano Dsm kupitia platform yenu mkawahujumu kwa kuwazimia simu.
Mnyika huyo huyo na Mbowe wake.
What goes around also comes around!
Na sasa ni zamu yenu.

Waambie Mbowe, Lema na Lissu walete pia familia zao toka Ughaibuni kuja kushiriki maandamano ya 24/01/24.
Sio wajifanye kuhanikiza huku wakiwa na Passport zao mifukoni.
Tunawajua mabingwa wa kutimkia Dubai,Canada na Ubelgiji.
Lissu juzi kati alitimks toka karatu mpaka Ubelgiji.
Bisha kama nasema uongo?
Mwambie Mbowe arufishe ile milioni 150 ya Samia aliyopewa juzi kanisani. Acheni kututapeli watanzania!
 
Lakini jamaa wote kweli wana suti mpya, au zote walizitoa sandukuni?

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Mpaka nguo za mkutanošŸ˜€
 
Kuna unaotoka na unaotokana (tengenezwa) huu wa hawa wanunuliwa suti ni unaotokana na CCM, ni upinzani maigizo tu.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app

..aliyelelewa na Ccm hawezi dumu ktk upinzani.

..waulize Steven Wassira, Makongoro Nyerere, Frederick Sumaye, na Edward Lowassa.

..mtu aliyezoeshwa kuishi kama raia wa daraja la kwanza hawezi kuvumilia kuwa mpinzani na kuishi kama raia daraja la kumi.
 
Siasa ni maisha ya watu wala si kwa viongozi tu na familia , ikiwa ni jambo la kawaida kwanini viongozi wanunuliwe suti mpya ?
 
Lakini jamaa wote kweli wana suti mpya, au zote walizitoa sandukuni?

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Kuna ukweli fulani hapo ila mimi pia Chadema siwaamini nawaoma ni walewale na mfumo uleule.
Mbowe wiki iliyopita hapa kapokea milioni 150 toka kwa Samia huku amekenua meno yote.
Kisha abakuja jukwaani eti peepers!
Wote wachumia tumbo tupu.
Nimemuona Mnyika amenona shingo full, shauri ya Posho za vikao vya maridhiano mwaka mzima.
 
Siasa ni maisha ya watu wala si kwa viongozi tu na familia , ikiwa ni jambo la kawaida kwanini viongozi wanunuliwe suti mpya ?
Tungemuelewa mleta hoja kama angeweka evidence mezani mifano kama picha au screen shot ya WhattsApp ikitoa maelekezo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreā€¦