Ushahidi wa majipu katika mfuko wa maendeleo ya vijana

Suleomary

Member
Jul 4, 2015
12
12
Kutokana na kutokuona hatua zikichukuliwa kufuatia uzi ambao nilileta hapa jukwaani unaohusu majipu katika mwili wa waziri mkuu Kassim Majaliwa kupitia wizara ya Sera, uratibu , Bunge, vijana na walemavu, leo naweka hadharani mazingira ya ufisadi katika mfuko wa maendeleo ya vijana unaofanywa na wenye mamlaka ya kuidhinisha malipo ya fedha katika mfuko huo. Hapa namaanisha Mkurugenzi wa vijana na Mhasibu wa wizara ya Habari.

Mwaka jana kilifanyika kikao cha maafisa vijana wote nchini kilichodhaminiwa na bank ya NMB, lakini jambo la kushangaza gharama za kikao hicho tena zililipwa kwenye mfuko wa maendeleo ya vijana, wakaguzi wa ndani walipokagua waliambiwa fedha za kikao hicho zilitoka kwenye mfuko wa vijana.

Mkurugenzi amekuwa akitumia fedha za mfuko kwa safari zake binafsi kwa kisingizio kwamba ankwenda kukagua shughuli za mfuko, lakini ukweli ni kwamba hiyo imekuwa njia yake anayoitumia kuchota fedha za mfuko wakati hakuna ukaguzi wowote.

Kwa ufupi ni kwamba Mhasibu wa wizara ya habari anapokuwa na shida macho yote wanaangalia kwenye mfuko wa vijana, wao ndio wanajua kuna shilingi ngapi sisi kila tukiomba mikopo kwa jili ya vikundi vyetu tunaambiwa hakuna hela lakini nimeenda hadi benki nikaangalia akaunti yao inahela nyingi na wala hawatumii.

Kassim Majaliwa, Jenista Mhagama nendeni mkafanye ukaguzi maalum kwenye mfuko wa vijana, tumieni wakaguzi ambao hawahongeki maana wale wazee ni wazuri wa kuhonga.

Mkihitaji taarifa zaidi nitawapa, ofisi yetu iko Kigamboni ukifika mbele ya Chuo cha Mwl Nyerere ulizia Asasi ya vijana inayoitwa TYDA, niulizie SALIM MOHAMMED au Mzee wa Fursa.
 
hongera kwa uthubutu mkuu

wanaitajika watu waliochoka kuonewa na kunyinywa kama wewe ili Tanzania iwe sehemu nzuri ya kuishi

Mungu akulinde dhidi ya uliowafichua
 
Mkuu, hongera. Naona umeamua kutoka kiukweli, safi sana. Bila shaka wahusika watafuatilia kama unayoyasema ni kweli.
 
Back
Top Bottom