Hey hey good people,
Leo ningependa tujadiliane kuhusu usaliti kwa njia ya mtandao na kanuni zipi ambazo zinaweza kutumika kuashiria usaliti kwa njia hio.
Kama tunavyotambua usaliti upo katika mafungu tofauti na uzito tofauti.Je huu usaliti kwa njia ya mitandao ya aina mbalimbali kama Facebook,Viber,Whatsapp,Twiter,Instagram au hata hapa Jamiiforums tunaupa uzito gani?
Nikiongelea usaliti wa aina hii namaanisha ile kuongea na mtu ambae huna mahusiano nae yoyote kuhusu masuala ambayo yanaweza kuleta hamasa tofauti,kumpa mtu huyo uhuru wa kuwasiliana na wewe,kuongea nae maongezi ya kimahaba,kuitana majina ya kimapenzi,kuanika hisia zako kwa mtu huyo n.k
Viashiria vipi vinaweza kutumika ili kudhihirishia kama huu usaliti umepiga hatua mbele,iwapo mwenza wako anapoteza hisia juu yako au mawasiliano yamenoga mpaka mwenza wako anakudharau na kuupa kipaumbele usaliti huu?Au kama wasaliti hawa wana miadi ya kuonana?
Kwa nadharia tu,watu wanaotenda usaliti wa aina hii wana madhumuni ya kupata manufaa gani?Je kuna sababu zinazoweza kupelekea wahusika hawa kutenda usaliti kwa njia hii?Mfano kutafuta vile vitu ambavyo anavikosa kwenye mahusiano yao,kwahio wanatafuta kipoozeo? Au ni tabia na hulka tu?
Tujadiliane.
Wasalaam G
Kwanza kabisa napenda niseme kuwa usaliti katika mahusiano kwa njia ya mtandao upo na kadiri siku zinavyozidi kwenda ndivyo jinsi usaliti huu kwa kutumia mitandao unavyozidi kuongezeka.
Watu wengi wanaofanya usaliti kwa njia ya mtandao, hufanya usaliti huo kwa sababu mbali mbali. Wengine ni kwa sababu ya kutaka faraja kutokana na matatizo yanayomkumba katika uhusiano wake, wengine ni kwa sababu ya kutafuta kitu fulani ambacho ananakikosa kwa mpenzi wake ambacho anadhani atakipata kwa huyo ambaye anafanya naye usaliti. Lakini wengi wao hufanya usaliti kwa sababu ya kutokuwa na msimamo, tamaa ya uzinzi na kutaka kuanzisha uhusiano na kila mwanamke au mwanauem anayemvutia machoni pake.
Mwanzoni uhusiano huu huanza kama mzaha tu, lakini kadiri mawasiliano yao yanavyozidi kuimarika ndivyo ukaribu wao unavyozidi kuongezeka na hatimaye kujikuta wamekuwa wapenzi kabisaaa.
Kugundua kama mtu anakusaliti au akusaliti ni mtihani mgumu sana hasa kwa mtu ambaye ni msiri kupitiliza na kwa mtu ambaye anayeweza kuigiza na kuficha hisia zake. Lakini waswahili wanasema, "Penzi ni kikohozi" maana yake upendo hauwezi kujificha. Kwa kusema hayo, naomba niainishe dalili ambazo zinaweza kukusaidia na kusaidia wengine kutambua mpenzi ambaye anasaliti iwe kwa njia ya mtandao au kwa njia nyingine yoyote ile:
Atapunguza Mapenzi Kwako
Katika ulimwwengu huu hakuna binadamu anayeweza kupenda watu wawili au zaidi ya wawili kwa wakati mmoja na akawapa upendo wenye uwiano sawa. Ama atampenda huyu na kumchukia huyu, au atakashikama na huyu na kumdharau yule.
Atapunguza Mawasiliano na Wewe
Mtu ambaye anakusaliti lazima atapunguza kukujali na kuwasiliana na wewe kwa sababu muda mwingi akili yake na mawazo yake yote yapo kwenye kuimarisha uhusiano huo mpya na ndio maana wakati mwingine zinaweza zikapita siku kadhaa asiliwasiliane na wewe bila ya sababu ya msingi na hata ukimuuliza anaweza akakupa sababu zisizokuwa za msingi. Na hii yote ni kwa sababu upendo wake kwako umepungua.
Anakuwa Msiri
Uhusiano wa kusaliti huwa sio uhusiano halali kwa sababu hiyo, lazima uhusiano huo ufanyike kwa siri. Hivyo mtu ambaye anafanya usaliti lazima atakuwa msiri sana kwa mambo yote anayoyafanya kati yake na huyo anayesaliti naye, hiyo ikiwa ni pamoja na mawasiliano yao na dating appointments zao na ndio maana hata wakati mwingine mpenzi ambaye anasaliti anakuwa hakupi uhuru na simu yake, login passwords za social accounts zake etc. Ukiona mpenzi wako amekuwa msiri kuliko kawaida tena bila ya sababu za msingi ujue kuna uwezekano kuwa mpenzi wako anakusaliti.
Atakuwa Mtu wa Kukulaumu
Siku zote mahali penye upendo wa kweli huwa kuna uvumilivu. Lakini upendo huo unapopungua na kutoweka uvumilivu nao hutoweka.
Hivyo mtu ambaye anakusaliti atakuwa mtu wa kukulaumu na kukutamkia maneno yasiyofaa hasa pale unapokosea badala ya kukukosoa na kukurekebisha kwa upendo. Na yote hiyo ni kwa sababu upendo wake kwako umepungua na ndio maana anashindwa kuvumilia mapungufu yako na anashindwa kukuvumia na kukusamehe hasa pale unapokosea.