usaliti CHADEMA sawa ,CCM hapana!

Malata Junior

JF-Expert Member
Nov 29, 2011
3,104
2,549
Poleni kwa majukumu wanajamvi.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekuwa na utaratibu wa kuwachukulia hatua za kinidhamu ikiwemo kuwafutia uanachama wanachama wake wanaokiuka katiba na kanuni za chama hicho.

Mojawapo WA ukiukwaji WA katiba na kanuni za chama hicho ni usaliti ambapo baadhi ya wanachama hukihujumu chama kwa kushirikiana na wapinzani wa chama ,kutoa siri za chama,kubambikizia KESI viongozi na wanachama waaminifu,kuunda chama kingine cha siasa wakiwa ndani ya chama,kuengua wagombea wa chama kwenye uchaguzi, kukashifu viongozi wa chama mitandaoni,kupigia kampeni vyama vingine n.k.

Baadhi ya wanachama waliochukuliwa hatua za kinidhamu na kufutiwa uanachama na vikao halali vya chama ni Zitto Kabwe,Kitila Mkumbo,Samson Mwigamba,baadhi ya vijana wa Bavicha maarufu kama MASALIA na wengine wengi.

Wakati CHADEMA ikichukua hatua hizo za kinidhamu dhidi ya wanachama wake,CCM na vyombo vyake vya propaganda ikiwemo ofisi ya msajili wa vyama vya siasa walipaza sauti kwamba huko ni kukiuka msingi ya demokrasia na kwamba CHADEMA haitaki mawazo mbadala.

Leo hii tunaona fukuza fukuza ya wanachama wa CCM kila kona ya nchi kwa madai ya kukiaaliti chama wakati wa uchaguzi mkuu mwaka jana. Yaani leo hii CCM wanaona wana haki ya kufukuza wasaliti lakini vyama vingine vikifukuza hapana ni kukiuka demokrasia. Hata hao akina Zitto waliofukuzwa CHADEMA nao pia wameshafukuza wanachama wao waliokiuka taratibu, kanuni na katiba ya chama chao akiwemo mgombea urais wa Zanzibar.

CCM acheni double standards, naomba kuwasilisha.
 
Zitto alipofukuzwa chadema, alitetewa mpaka na wabunge wa ccm bungeni, jamani unafiki mbaya sana.
 
CCM imeanza kufukuza wasaliti tokea zamani...kwa uchache...Maalim Seif,Ahmad Rashid,Kambona..nk..sio jambo jipya hata kidogo.
 
wapnzani na makapi.jpg
tena wote wakitokaga ccm uelekeo ni ukawa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom