Usalama wa Nchi, Pimeni haya

Usalama wa Nchi, Pimeni haya

jbmalya

Senior Member
Joined
May 1, 2012
Posts
111
Reaction score
29
1.Katiba ya wanachi ni msingi wa kuliongoza taifa kuelekea kwenye maendeleo, ccm walizusha propaganda kuwa katiba pendekezi inataka kuuvunja muungano, ili kuwalaghai ninyi watu wa usalama ili mfikiri katiba pendekezi ni hatari kwa Taifa.Ukweli ni kwamba hoja ilikuwa sio muungano, ila vipengele vingine ambavyo vilikuwa vinaenda kuwabana viongozi waliohujumu Taifa na kuwabana viongozi wajao.

2.Kwa sasa siasa imekuwa ni vita na uhasama na hatari ya kuuwana, hii yote ni ccm katika kuweka mifumo yake, watu wanaona siasa ni sehemu ya kwenda kujitajirisha, katiba ilikuwa inaenda kudhibiti hali hiyo.

3. Katiba ilikuwa inaenda kutenganisha majukumu ya majeshi yetu na mihimili mingine ya nchi, Bunge, Mahakama, na serikali, hii ingelete amani na utulivu kwenye vyombo hivi vyenye mamlaka ki nchi.Leo hii ssm imefikia pahala inatisha hata askari. Jeshi halipaswi kutishwa na wala kamanda hapaswi kutishwa na mwana siasa.

4.Mikataba mibovu inayoingiwa na ccm ni ishara tosha kuwa ndani ya ccm nchi haipo salama, nchi inatafunwa, hauoni hilo?

5.Ona kashfa mbalimbali zinavyotokea na wahusika walivyo na jeuri ya kujibu hizo kashfa, bila hata wasiwasi? usalama wa nchi upo wapi?

6.CCM ya Nyerere sio ya sasa, nachokiona ni genge la watu wachache wenye hofu, na ubinafsi uliojaa tele, wenye kukandamiza mtu yeyote mwenye mawazo tofauti na wao, wenye visasi kwa watu wanao waonesha mapungufu yao, wenye unafiki ulio wa hali ya juu ya kuweza kulaghai hata vyombo vya usalama na Dunia kuhusu Nchi yetu. Hatutofika.

7. Unajisikiaje unapo ona wewe ukiweza kwenda hospitali kwa matibabu ya bima au kwa ela zako wakati maelfu wanataabika? Usalama wa nchi upo wapi, usalama wa watu upo wapi?, unajisikiaje watoto vichanga na wazazi wanapokufa kila mara ma hospitalini kwa kuwa tu wamekosa pesa ya kujihudumia wakati wewe unauwezo huo, unajisikiaje wakati mtanzania anakula mlo mmoja kwa siku au mboga ya aina moja wakati wewe unabadilisha kila siku, unajisikiaje wewe unapoweza toka na kufurahi na wenzako wakati maelefu ya watanzania wapo bize kutafuta ela ya mlo wa siku, unajisikiaje watu wanapokosa maji safi, shule bora wakati wewe unapeleka watoto wako internationa school. Mlio na mafanikio mnaipenda hali hii, mnafaidika na hali hii, manaona ufahari na hali hii. ni ubinafsi hauzi kuwa bora wakati malaki wana taabika, ubora wako upo wapi.

8. Chonde chonde fuateni pimeni kuna faida gani kwa tulivyo kama nchi kutumia nguvu kubwa kuwaweka watu wanao paswa wakae pembeni na kujifunza mabaya yao.

Mungu Atasaidia tu.
 
Back
Top Bottom