Usafiri majini marufuku siku ya uchaguzi

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
MAMLAKA ya Usafiri Baharini Zanzibar imefuta safari zote za baharini siku ya uchaguzi wa marudio Zanzibar, Machi 20 mwaka huu kutoa fursa kwa wananchi wenye sifa kupiga kura visiwani humo.

Katika taarifa yake jana, mamlaka hiyo ilisema siku hiyo ni marufuku kwa vyombo hivyo kusafirisha abiria kwa vile hiyo ni fursa pekee kwa wananchi kushiriki uchaguzi huo.

Taarifa hiyo ilisema uamuzi huo umefikiwa kutokana na wananchi wengi kujiandikisha kupiga kura.

Machi 20 mwaka huu wananchi wa Zanzibar watachagua viongozi wa ngazi mbalimbali baada ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana kufutwa kwa kile kinachodaiwa kuwa kasoro wakati wa upigaji kura.

Matokeo hayo yalifutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha.

Baadhi ya vyama vya upinzani vimesusia uchaguzi huo wa marudio kikiwamo chama kikuu cha upinzani cha CUF.

Chanzo: Mtanzania
 
Duniani, ni Zanzibar tu (kwenye uchaguzi huu wa Rais wa chama) ambapo wapigakura wanashurutishwa kupiga kura. anayepiga si akapige na anayetaka kusafiri si asafiri? siku nne kabla ya siku ya uchaguzi, wooote hapa Pemba na robo kule Unguja tunasepa. Yaani hawa Interahamwe na Mazombie damu na dhulma waliyofanya inawafanya waweweseke na kurukwa na akili na kutoa maamuzi ambayo ni kituko kwa jamii ya ndani na ya nje. Mshaambiwa watu hawashiriki uchaguzi, jichagueni wenyewe sasa kwa nini mlazimishe watu washiriki?
 
Back
Top Bottom