Usafiri kwenda Iringa mchana

Saa 7 mchana basi la mwisho upendo, lakini unaweza kwenda mbezi mwisho au Misugusugu ukavizie IT
 
Lipo Abood saa saba mchana. Nauli Sh. 15,000/=. Sijui kama uko stand saa hizi utaliwahi.

Au nenda mpaka Morogoro, unaweza kubahatisha Hood za kutoka Arusha, yako mawili moja linaelekea Mbeya nyingine linaishia Arusha. Kwa Morogoro huwezi kukosa usafiri wa gari ndogo lakini kuna madalali/wapiga debe.
 
Nenda ubungo pale tanesko ni kabla hujagija rombo kuna noah huwa zinapakia mbeya, nauli ni 25-30. Ukikosa nenda rombo zinapopaki fuso , pia kuna gari za iringa na mbeya.
 
Basi za mwisho zinatoka Ubungo saa saba mchana na kama hauko Ubungo kwa sasa ushachelewa. Cha kufanya nenda pale TANESCO kwa mbele unaweza ukapata watu watakaokuunganisha na gari za IT au mafuso ya kwenda pande hizo. Nachoamini mimi ni kuwa ukiwa barabarani utaenda popote na usafiri wa aina yoyote unatakiwa tu kuwa kama mjeshi usichague muhimu kufika unapoenda
 
Morogoro zipo Noah Huwa zinakwepo hadi Saa Moja usiku.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je Iringa kurud dodoma mida hii zipo?

Sent from my Iphone 7 using JamiiForums mobile app
 
Habari zenu jamani,je kuna msafiri yoyote mwenye kwenda iringa wiki hii jamani,
 
Kwa hapa Lindi gari za Iringa mchana kwa kweli sio rahisi. Labda uvizie lift ya watoto wa mkuu wa mkoa. Wamefunga shule sasa wanarudi kwa bibi Songwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…