Usafiri Dar - Mbeya

jashmoe32

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2012
Posts
1,098
Reaction score
437
Heshima mbele Wadau,

Nina safari ya kuelekea Mbeya nikitokea Jijini Dar es Salaam. Nlikua naomba kujua yafuatayo:

[*] gari linalofanya safari kutokea Dar-Mbeya (ambayo ni luxury na ni salama sio kukimbizana)

[*] Nyumba ya wageni (lodge au hotel) iliyo salama na bei ya Mtanzania wa kawaida (Economy Class. Nitashukuru ikiwa karibu na stendi ya mabasi na pia mkintajia gharama ya hoteli au lodge

Natanguliza shukrani zangu wadau.
 
JM Luxury Ni mazuri,
Rungwe Express,
New Force.
anza namba moja kwensa chini.
Kwa lodge Kuna Mbeya Hotel Na zingine
 
Pa

Panda- Ndenjela au Dar Lux
Kulala- Paradise Hotel
 
Ila sio peace of mind..kuna ndugu yangu alikaa pale akaibiwa vitu chumbani kwake na hawakutoa ushirikiano kabisa mxuuuu
 
Panda dar lux mkuu ndiyo basi bora Kwa sasa njia ya mbeya, nilipanda jana kuja dar yani sijajutia safari yangu kabisa.
Wana basi mpya kabisa full kipupwe njia nzima.

Kuhusu hoteli unaweza fikia padz Lodge au usungilo Lodge ambazo zipo bara bara ya mbalizi sio mbali sana na stendi. Pia Kuna GR hotel ipo soweto Mbeya nao wapo vizuri sana.
Karibu sana mbeya
 
Kaka Paradise Hotel ina umbali gani toka stendi kuu??Je gharama zao zina range shillingi ngapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…