Hii thread si mpya. Si ajabu kiongozi wa Irani hataki kujadili kasoro za uongozi wake kuhusu Corona (maana walishindwa kufunga msikiti wa kaburi pale Ghom ambako maelfu waliambukizwa), badala yake kupiga debe kuhusu "maadui wa mapinduzi ya Kiislamu" (kwa kawaida Marekani na Israeli, ikihitajika pia nchi yoyote nyingine) waliosababisha balaa.
Siku hizi wanajitahidi hasa kuwatesi wafuasi wa Ubahai (dini ya Kiirani iliyoazishwa karne ya 19, balaa kubwa eti waliongozwa na nabii baada ya Mtume Muhamad), pamoja na Wakristo wapya walioachana na Uislamu.