Urusi yatuma msaada wa matibabu kwa Serbia kukabiliana na corona

mohamedidrisa789

JF-Expert Member
Jun 20, 2015
5,111
21,657
Wizara ya ulinzi nchini Urusi imesema leo kuwa nchi hiyo itatuma ndege 11 za kijeshi zilizobeba vifaa vya tiba nchini Serbia kusaidia kukabiliana na mripuko wa virusi vya corona. Mikhail Chernyshov, ambaye ni Meja Jenerali katika jeshi la Urusi amesema kuwa jeshi la nchi hiyo linaelekea Serbia kusaidia kupambana na mripuko wa virusi vya corona na kwamba kundi lao linajumuisha idara za kemikali na biologia zitakazotoa huduma za kukabiliana na maambukizii pamoja na kundi la madkatari litakalotoa usaidizi wa matibabu.Tangazo hilo linakuja siku moja baada ya ikulu ya Kremlin kusema kuwa rais wa Serbia Aleksandar Vucic ametoa ombi la msaada wa kibinadamu kwa rais Vladmir Putin kwa taifa lake ambalo limerekodi visa 1476 vya maambukizi ya virusi vya corona na vifo 39. Urusi na Serbia zina uhusiano thabiti wa kisiasa, kijeshi na kibiashara. Urusi inaiunga mkono Serbia kwa kukataa kuutambua uhuru wa Kosovo iliyokuwa mkoa wa Serbia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Geopolitics

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom