Urusi: NATO inachochea machafuko Mashariki ya Kati

Sinoni

JF-Expert Member
May 16, 2011
6,188
10,667
Wizara ya Ulinzi ya Russia imejibu tuhuma za shika la kijeshi la nchi za Magharibi (NATO) ikisema muungano huo wa kijeshi imeitumbukiza Syria katika matatizo
makubwa na kusababisha machafuko katika eneo lote la Mashariki ya Kati.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Russia, Meja Jenerali Igor Konashenkov amesema kuwa nchi wanachama wa NATO zimechukua hatua ambazo zimelitumbukiza eneo la Mashariki ya Kati katika machafuko na vita na kwamba operesheni za kijeshi za Russia dhidi ya makundi ya kigaidi si sababu ya hali ya sasa katika eneo hilo.

Igor Konashenko ameongeza kuwa matamshi yaliyotolewa siku chache zilizopita na Katibu Mkuu wa jumuiya ya NATO, Jens Stoltenberg ni ya kipumbavu. Katibu Mkuu wa NATO alidai kuwa mashambulizi ya anga yanayofanywa na Russia dhidi ya makundi ya waasi nchini Syria yanadhoofisha jitihada za kupatikana njia ya utatuzi wa amani wa vita nchini Syria!


Chanzo:
www.irib.ir
 
Kila mmoja anakorofisha/anatetea kwa maslahi yake binafsi, ndo wazungu wanavyotufanya nchi zetu, ukikaidi tu amri wanakutengezea zengwe ili wakupige !!!!
 
Back
Top Bottom