Urithi wetu

Fundi Mchundo

Platinum Member
Nov 9, 2007
8,943
6,863

Wakati tunawabebea mabango hao tunaowaita mafisadi kuna umuhimu wa kuangalia sehemu nyingine za rasilimali zetu. Hapa juu tunazungumzia footstep zinazokisiwa kutoka kwa jamii ya kwanza ya binadamu kutembea wima. Hizi ziko kwetu. Si wengi tunajua hilo. Inakwenda na maji kama yanavyoainisha maandishi(ingawa sikubaliani na wazo la kujenga makumbusho na kupafanya mahali accessible kwa maana naamini kwa kufanya hivyo tuta-accelerate kupotea kwake). Tunazungumzia vyura wa Kihansi ambao nakumbuka tuliwacheka sana wazungu kwa kuhangaikia VYURA. Tuliwaona wapuuzi. Tumebaki na Kihansi inayojaa tope na wao wamebaki na chura ambao wanawaongezea umaarufu. Tunashabikia ujenzi wa mahoteli Ngorongoro bila kuangalia athari zake kimazingira. Tukiulizwa, tunajibu kwa jeuri, mbona Kenya wana hoteli kibao kwa nini sisi tunakatazwa. Kivutio kikubwa cha mbuga za Tanzania ni authenticity na exclusivity zake. Unawaona wanyama katika hali aliyotarajia muumba na hamkumbani na watalii kibao. Tunasahau kuwa Ngorongoro ni eco-system ya pekee duniani. Tunawatosa Flamingoes wa Ziwa Natron kwa hela mbuzi tutakayoipata kwa kuvuna soda ash. Itakapoisha, wawekezaji watafunga virago wakituachia ziwa tupu bila hao flamingoes. Nashangaa shujaa yetu Slaa yuko kimya kwenye hili! Kwa kuweka pamba masikioni tunajimaliza na kesho na keshokutwa hatutakuwa na kitu cha kuwaachia wajukuu wetu.
 

Fundi Mchundo:

Ngoja tujazie hii mada. Watanzania tuna mapungufu fulani ya kiakili. Tunapiga kelele pale matatizo yanapotokea katika Pesa Taslimu (CASH). Lakini kwenye rasimali ambazo zinaweza kuwa vyanzo za pesa katika miaka inayokuja tumekaa kimya.
 

Shukran, Bin Maryam. Mimi nimeiweka hapa kiuchokozi. Pamoja na nyimbo zote za kupinga tunachokiita ufisadi, priorities zetu ziko warped. Tunagombea vijisenti wakati rasilimali yetu halisi tunaiangalia ikiteketea. Na hapo tukapokuta imeondoka na kuhamia ulaya ambako angalau wanaiheshimu na kuihifadhi tunapiga kelele za FOUL! Tutabaki kuwa perpetual victims.
 

Ni kweli Bin Mariam,

Nadhani ni bora tukawaza yale yanayoleteleea pesa hizo na jinsi ya kuzihifadhi kuliko kushikia bango kilichopotea kwani hakitarudi hizo zote zilizo baki ni porojo tu.

Mimi nadhani tuna mchango mkubwa kwenye hili,kwa mawazo tutakayo yatoa hapa kwani si wote wanao fahamu kwamab sehemu ile itapotea kama hakutakua na wakuwakumbusha wahusika kufanya linaro wezekana
 
Tupo busy na "mafisadi" wa BOT hayo mambo ya heritage no-one alie tayari kuyaangalia...
 
Tupo busy na "mafisadi" wa BOT hayo mambo ya heritage no-one alie tayari kuyaangalia...

Kweli tupu! Nimechungulia huko kwa Meghji nimewakuta wote! Hii apathy yetu kwenye mambo ya msingi itatumaliza.
 
Kufikiria mazingira kabla ya kula ni kitu kigumu.Ndiyo maana watu wana hii apathy.Kuanzia wabunge mpaka hapa bodini.

Sasa wengine hata kama wameshapata "escape velocity" ya kuondoka kwenye maisha ya "a dollar a day" bado tunakuwa na ile mentality ya kama kitu hakiko tangible kama mabilioni ya BoT basi si muhimu, na kama ni muhimu kinaweza kusubiri haya yaliyo tangible.

Tunahitaji standard of living itakayotuwezesha sio tu kula na kushiba, bali pia kupanga mikakati ziada ya kimaendeleo kama vile ni vipi tutakabiliana na mazingira yetu.
 

Mkuu! Hii ni kama vile tunavyofyeka mapori kutafuta kuni na mkaa wa kupikia. Baada ya kupika, kula, kushiba na kukitoa tena, tunastuka kuwa mvua hainyeshi, nchi imekuwa jangwa na hatuwezi kuvuna hicho chakula tulichokuwa tunatafutia kuni kwanza! Kilichobaki ni kungoja Oxfam na wakina Bob Geldorf kutubebea bango kutuombea chakula kwa wale waliotuuzia mashoka na mapanga ya kukatia hiyo miti! Mbona hatutaki kujifunza?
 
Tupo busy na "mafisadi" wa BOT hayo mambo ya heritage no-one alie tayari kuyaangalia...

Naelewa huko busy, lakini kwa takwimu zilizopo sasa urithi wenyewe ndio unaochangia pato kubwa kwa taifa kuliko sisi wenyewe. Mchango unaotolewa na sekta ya madini na utalii inatoa pato kubwa kuliko kazi na akili zetu.
 

Mgogoro wa Darfur chanzo chake ni resources.
 
Kwa bahati mbaya hatutambui hilo!

FM,

Huu ndio ugonjwa mkubwa sana tulio nao watanzania UVIVU WA KUFIKIRI.

Sio ss tu wan JF hata viongozi wetu ndio kabsaa.....
Nimesoma article leo hii kwenye Raia Mwema kuhusu UJengwaji wa Kiwanda cha magadi kwenye ziwa Natron kwamab ni hatari kwa mazingira lakini Waziri wetu mmoja hafikiri hivyo!
Yeye anawaza fedha zitakazo lipwa na muwekezaji kuhusu athari yeye hapana taka sikia unless kama kuna mwananchi/wananchi watato fedha kiasi kitakacho tolewa na mwekezaji ndio ujenzi utasitishwa.

sasa niambie kama sisi tunashindwa kuchangia haya mambo ya msingi tunategemea MAFISADI (mawaziri) watatu fanyia?
 

Kinachosikitisha si waziri peke yake hata Mheshimiwa mbunge wa sehemu hiyo ( ipo kwenye jimbo la karatu)kanayeongoza mapambano dhidi ya tunaowaita mafisadi hafikiri hivyo! Haoni umuhimu wa kuhifadhi hao flamingoes. Sasa kama hawa ambao wanadai wanatofauti na hao walioshika usukani sasa hivi hawaoni umuhimu wa kutunza mazingira katika jimbo lao kuna matumaini kweli? Mimi nilidhani kwa vile wamo humu jukwaani na kuna wakati walifikia kuomba ushauri kuhusu dira au utume wangechangia kwenye hii mada. Wote tupo kwenye ufisadi wa BOT, machimbo kitu ambacho kinanifanya nifikiri kuwa pengine kinachogombewa ni kushiriki kwenye huo ulaji! Inakatisha tamaa. Mungu inusuru nchi yetu. Mungu inusuru Tanzania.
 
Wakuu heshima mbele.... Nakubaliana na mawazo ya article hii, kwa kweli panapojiri sifa lazima tuweke mbele. Mimi naomba kabla sijasema nimpongeze JK kwa kuanzisha Wizara ya Mazingira (huyu ni Profesa, narudia ni profesa kabisa ndiye waziri) lakini haya yote yanatokea naona waziri labda ameamua kufumbia macho, au kuna justification to allow it, au basi hatekelezi majukumu yake!!! Naona kwenye other threads kuna wawajibikaji wa Serikali wakiwemo kina ZM wameshikiwa bango kwa kufumbia macho mambo pale BOT lakini bado huyu mheshimiwa hajakamatiwa bango katika issue ya ziwa Natron, na mengine mengi (zikiwamo nyayo za watu kale, si utani mwanangu ni rasilimali hizo hata zangu nadhani in a million years itakuwa dili so be careful!!) mpaka leo!!! sishangai sana lakini nina mengi ya kujiuliza kama wenzangu "WATANZANIA PRIORITIES ZETU ZIPO WAPI??"

kwa hili la Darfur, nadhani tuangalie ramani (topo map) tutaona kuwa waheshimiwa wanaosema ni resources hawajakosea sababu kule major resource, MAJI hakuna na ndio ksheshe lenyewe hilo..... hapo sasa
 
Profesa (?) ndiye aliyembele kupigia debe ujenzi wa mahoteli Ngorongoro, barabara za lami na kuongeza air strip. Mtu yeyote anayetaka kujua madhara ya lami aangalie jinsi wanyama wanavyobamizwa kwenye barabara iendayo Iringa inayokatisha Mikumi. Mimi hawa maprofesa, madaktari (Ph.D) sina hamu nao.
 
Kibaya zaidi ni kuwa kwa sababu makampuni ya magharibi yanadai Environmental na Social Impact Assessment ifanyike kabla ya kujitumbukiza tumewakumbatia wale wanaotoka uarabuni, India na China kwa sababu wao hiyo awajali. Kwa mawazo yetu finyu tunaona ndiyo wanautupenda kwa sababu wanaheshimu uhuru wetu wa kujiangamiza. Hicho kiwanda cha ziwa Natron kinasukumizwa na Tata kutoka India, mahoteli ya mbugani yumo huyo mwarabu aliyenunua Kilimanjaro na barabara karibu zote sasa hivi zimeshikwa na makandarasi wa kichina.
 
Fundi, yaani unajua kuna vitu mtu unakaa unaangalia na unashindwa kusema chochote kwa kweli.... Nilisoma kitabu kinaitwa "Dragon and an Ostrich - Sino African Relationship" (nadhani nimepatia hiyo title)!! Kwa kweli sijui tuendapo...
 
Fundi, yaani unajua kuna vitu mtu unakaa unaangalia na unashindwa kusema chochote kwa kweli.... Nilisoma kitabu kinaitwa "Dragon and an Ostrich - Sino African Relationship" (nadhani nimepatia hiyo title)!! Kwa kweli sijui tuendapo...


kuna mengi ya mfano huu ila hayana washabiki hapa.
Nadhani ili kuleta tofauti nimuhimu kuendeleza mapambano na kumulika bila ya kuangalia nani anachangia na nani hachangi labda iko siku watageuka upande huu nakuona ni muhimu.

Wengi wetu tunadhani hapa ni kuzungumza tu lafu unaachana nayo
 

Hata mchina, mwarabu au muhindi kabla ya kuja kwetu walifanya juhudi nyumbani kwao. Matumizi mazuri ya mali asili zao na vipaji vyao ndio vilivyofanya wao wapate nguvu ya kuja kwetu. Na wanavyovifuata vikiisha wataondoka lakini sisi hatuna pa kukimbilia.

Wakati wa Clinton, kulikuwa na mkataba wa kusaidia viwanda Africa. Wachina wakajenga kiwanda Botswana au Swazi na wakatumia mkataba huo ku-export nguo Marekani na sasa wameshaingia mitini na kuwaachia watu majengo.

Kama sikosehi kipande cha barabara kutoka ubungo kwenda Tazara (11 Km) kilisuburi mhisani.
 

Angalau kuna watu wanajitahidi kutusemea ingawa sijui kama watasikilizwa. Mbona mbunge wa hiyo sehemu yuko kimya? au naye anaunga mkono mradi huu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…