Urambo, rais kikwete aamua kusema ukweli siasa za u-Sitta na u-Kapuya zinaangamiza wilaya

MotoYaMbongo

JF-Expert Member
Jan 7, 2008
2,146
884
Kitwete angalau umeondoa aibu na kujisemea ukweli unaouidumaza wilaya ya Urambo, hilo ni kweli kabisa wilaya híi ya Urambo ni kama haina wabunge kabisa kwani majukumu yao walishayasahau na kukalia maneno yasiyoleta tija kabisa kweli hii inasikitisha sana na hii nanukuu "NASHANGAA KUÖNA WATOTO WA BABA MMOJA HAWAELEWANI" Dr huyo wa heshima aliyatamka maneno hayo kwa uchungu sana na kuwaönea huruma watu wa Urambo, Haya watu wa Urambo na Kaliua mambo ndo hayo yamewekwa hadharani endeleeni kukumbatia nge mkidhania ni rafiki kumbe ana sumu kali inayoweza kuua, kwanza wabunge wenyewe wamekula kona hata Rais ameingia bila hata kukaribishwa na wenyeji wake Sita na Kapuya, badilikeni mpaka muambiwe nini ndio muelewe?
 
Huu uzi una kaj iukweli embu mleta mada tililika kidogo kuna nini Urambo mpka JK aseme hivyo?
 
Hakika hali ya Wilaya ya Urambo ni mbaya sana. Mwaka juzi 2011 mwezi Juni nilisafiri kwenda huko ambako nilikuwa sijafika tangu mwaka 1970. Nilidhani nitakuta barabara za lami zinazounganisha Tabora na Urambo, Tabora na Nzega. Salaaaleee!! Kwa mshangao nilikutana na barabara mbovu sijapata kuona. Kumbe ndiyo maana Kapuya alikuwa akienda na Helkopta ya Jeshi, aliogopa vumbi ila wananchi wake ni halali kula vumbi. Wilaya ya Urambo ina Wabunge wawili mashuhuri: Samwel Sita na Prof. Kapuya.
Wakati wa kurudi nilipanda basi kutoka Urambo hadi Tabora na nikaendelea hadi Nzenga. Lo!! Tulipofika Nzega abiria wote tulijaa vumbi hadi waliotupokea wakatuonea huruma na kutupeleka kwenye nyumba ya wageni tuonge na kubadilisha nguo. Ni ajabu, wananchi wa Tabora bado wanashabikia mafisadi katika hali mbaya namna hiyo.
 
Hawa Wanyamwezi sijui wanalaana ya Mungu sio bure, nilipita toka Manyoni hadi Tabora nikaja pita tabora hadi Nzega daa utafikiri jehanamu,. Hivi mi nauliza kwanini CCM imewachukia sn wana Tabora hivi
 
Kapuya na Sitta ni watoto wa baba mmoja! Kumbuka usemi wa mafiga matatu kwenye kampeni cha chama chao!
 
Kitwete angalau umeondoa aibu na kujisemea ukweli unaouidumaza wilaya ya Urambo, hilo ni kweli kabisa wilaya híi ya Urambo ni kama haina wabunge kabisa kwani majukumu yao walishayasahau na kukalia maneno yasiyoleta tija kabisa kweli hii inasikitisha sana na hii nanukuu "NASHANGAA KUÖNA WATOTO WA BABA MMOJA HAWAELEWANI" Dr huyo wa heshima aliyatamka maneno hayo kwa uchungu sana na kuwaönea huruma watu wa Urambo, Haya watu wa Urambo na Kaliua mambo ndo hayo yamewekwa hadharani endeleeni kukumbatia nge mkidhania ni rafiki kumbe ana sumu kali inayoweza kuua, kwanza wabunge wenyewe wamekula kona hata Rais ameingia bila hata kukaribishwa na wenyeji wake Sita na Kapuya, badilikeni mpaka muambiwe nini ndio muelewe?

Hivi yuko kwenye kampeni au ziara ya kikazi??

Inaelekea kama vile trip ya kumsafishia mtu njia ya 2015.............. Anyway, wanatwanga maji kwenye kinu!!
 
Hawa wanyamwezi sijui wanalaana ya Mungu sio bure, nilipita toka manyoni hadi tabora nikaja pita tabora hadi nzega daa utafikiri jehanamu,. Hivi mi nauliza kwanini ccm imewachukia sn wana tabora hivi

Mkuu umeuliza swali la msingi, ukizingatia hawa ndio wazalishaji wakubwa wa Tumbaku na Sigara inapanda bei kila siku kupitia kodi, Hivi kwa mtindo huu Mtwara wakisema gesi iwanufaishe wana mtwara kwanza nani atapinga??
 
mi naungana na wanamtwara kudai gesi yao haiwezekanik bagamoyo iwe inaunganishwa kwa rami kila sehem afu tabora ikawa choka mbaya vile,. Sera ya majimbo nafikiri mi itasaidia
 
Katika ziara yangu huko Urambo nilifika kwenye kijiji maarufu kwa kulima tumbaku kiitwacho Msimba. Kule kila nyumba ina picha kubwa ya Chagua Kikwete, Chagua CCM. Chagua Kapuya n.k Lakini nilikuta wanalalamika kuwa tumbaku yao waliyovuna imeshushwa bei na hainunuliwi kwa wakati. Kweli maghala ya tumbaku majumbani na ya kijiji yalijaa. Wakadai kuwa mwaka uliotangulia - 2010 - ilinunuliwa mapema na kwa bei nzuri. Kumbe ulikuwa mwaka wa uchaguzi. Hata hivyo ukiwagusa kuhusu mabadiliko bado walidai kuwa vyama vingine vitaleta vita. Hao ndio baadhi ya wana-Tabora. Wamesinzia kweli.
 
Baada ya kuutafuta ukweli kwa wana Urambo kwa kile ninachokiamini mimi kusoma habari zinamwagwa hapa JF nyengine ni za kweli na kuna nyengine si za kweli na iki ndicho nilicho bahatika kukipata
Endeleaaaaa
wabunge hawa ni maadui wa damu kiasi cha uadui huo kudumaza maendeleo ya Urambo. Ni zaidi ya uadui wa Nape na Dr.Slaa, mfano

  • Katika vikao vya madiwani, Sitta akigundua kama Kapuya atakuja, basi yeye hawezi kamwe kuhudhuria hicho kikao, sio tetesi, ni attendace register ya vikao vya madiwani inasomeka hivyo
  • Kapuya aliwahi kuleta mradi wa maendeleo jimboni kwake, ambao ungepita mpaka kwa Sitta lakini aliukwepesha makusudi
  • Wamefanikiwa kutengeneza makundi kwa madiwani wa Urambo, kuna madiwani wa Sita na Kapuya
  • Ndio maana kugawa na ulazima wa kugawa wilaya ili Urambo abaki Sita na Kaliua abaki Kapuya

Nadhani kudumaa kwa maendeleo Urambo inachangiwa sana na huu uadui, Kwa taito zao na ''uzee'' wao CCM& Mjengoni ilitosha kabisa kwa umoja wao kuiweka Urambo juu.

Haya wana Tabora kumbukeni maendeleo ya yenu yataletwa na nyinyi wenyewe kwa kuonyesha kujijali na sio kuwajali
 
Tabora tunaongoza kwa majungu,uvivu na unafiki Tanzania nzima,ndiyo sababu hatuendelei.mtu akiona unafanya chochote cha maendeleo yko radhi aende kwa mganga kujua kama unamtumia kishirikina n.k TUBADILIKENIvinginevyo koo na koo zitakuwa masikini.
 
Tatizo la tabora ni kukumbatia ccm na sifa kubwa ya ccm ni kuwafanya wananchi wasijitambue ili itawale kirahisi. Angalia, maeneo mengi yanayoongoza kwa kuishabikia ccm ndio hayo hayo yanayoongoza kwa umasikini na yako nyuma kielimu.
 
siku zote shetani atafuti watu alio nao tayari.Ni ngumu kwa ccm kupeleka maendeleo kwa sehemu ambapo ina uhakika na majimbo yote ni yake hivyo inauakika!mikoa mingi yenye upinza inakuja juu saana..Tabora BADILIKENI Kigoma hao wana Leka tutigite.
 
Mimi nilisoma Tabora Boys Secondary School kati ya mwaka 1988-1994. Wakati huo wa Chama kimoja mchepuo wa shule hiyo (pamoja na Tabora Girls) ulikuwa Siasa na Ulinzi, ila ilizoeleka kama Taboara Boys Military Secondary School, na hata baada ya kutoka pale, JKT tulikuwa haturudii kwata.

Mji wa Tabora ulikuwa ni mji wa Academics. Tabora Boys and Girls secondary schools, Kazima, Mirambo, Uyui, Chuo cha Ardhi, Chuo cha Uhazili, Chuo cha Nyuki, Kipalapala Seminary, Tabora TTC, Chuo cha Reli. Sekondary nyingine nje ya mji wa Tabora kama Itaga Seminary, Sikonge, Uchama, Chuo cha Ualimu Urambo, nk.

Kiufupi, Tabora ilikuwa inapata uhai kwa sababu karibu 60 percent ya mji ilikuwa ni sekondari na vyuo.

Shule na Vyuo hivi vyote vilikuwa na maeneo makubwa sana for future expansion au upgrading. Ninachojiuliza mpaka leo watawala walishindwa nini kuufanya mji wa Tabora ukawa mji wa kielimu kwa kupanua sekondari zili na kuvikuza vile vyuo? Kieneo, Tabora Boys ingeweza hata kuongezewa uwezo kutoka wanafunzi 600 mpaka hata 6,000. Mbona shule binafsi kama St Maries zina uwezo wa kuhimili kufundisha maelfu ya watoto, tena kwenye vieneo vilivyo finyu kabisa?

Chuo cha Ualimu Tabora hivi kweli hakikustahili kuwa kimefikia level ya kutoa shahada (together with the likes of Butimba)? Waliopita pale watakubaliana na mimi kuwa kilikuwa ni chuo chenye facilities nyingi, majengo na eneo kubwa la kutosha kuaccomodate mahitaji mengine ya kukiwezesha kutoa huduma ka wanafunzi wengi zaidi, na kwa madaraja mengi zaidi.

Chuo cha Uhazili kilikuwa ndo tegemeo la kuzalisha ma-secretary hapa Tanzania. Kama kungekuwa na mipango endelevu, labda kingekuwa kwa sasa kinatoa hapa BBA.

Hata kisiasa mji wa Tabora ulikuwa hauko nyuma. Nadhani kuna maamuzi fulani enzi za ukoloni yalifanywa na kina Nyerere Tabora (kura tatu??). No wonder Nyerere alipenda sana kutembelea Tabora (nilikuwa darasa la pili/tatu, wakati huo Msekwa Mkuu wa Mkoa Tabora, na majaji wa mahakama kuu kanda ya Tabora walikuwa Chipeta na marehemu Rubama).

Well, all in all, nilichotaka kusema ni kuwa fursa za kuufanya mji wa Tabora (na mkoa kwa ujumla) kukuwa zilishaawekewa misingi muda mrefu wa watawala waliotangulia. Sasa hao waliofuata (walikwemo mawaziri wawili wa elimu Kapuya na marehemu Kabeho) hawakutimiza wajibu wao!!
 
Back
Top Bottom