Urais roho juu CCM, UKAWA

mcubic

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2011
Posts
10,310
Reaction score
6,548
Joto la kuwatangaza wagombea urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), linazidi kupanda huku kila upande ukimvizia mwenzake aanze kutangaza mgombea wake.

Hatua hiyo imekuja baada ya viongozi wa Ukawa katika mkutano wao na wanahabari kueleza mgombea wao atatangazwa Machi mwaka huu, lakini hadi sasa imepita miezi miwili bila kujulikana.

Wakati hayo yakiendelea ndani ya Ukawa, CCM nayo hadi sasa imeshindwa kueleza ni lini atapatikana mgombea wake pamoja na kutangazwa kwa hatima ya makada sita wa chama hicho wanaodaiwa kuanza kampeni kabla ya wakati.

Nchi ikiwa imebakiza miezi mitano ili kufika Oktoba utakapofanyika Uchaguzi Mkuu, hadi sasa vyama vya upinzani hasa vile vinavyonda Ukawa pamoja na CCM vimekuwa vikitegeana nani aanze kutangaza mgombea wake jambo ambalo linaelezwa limekuwa tofauti na miaka iliyopita.

Akizungumzia taratibu za uteuzi wa mgombea ndani ya CCM hivi karibuni alipokuwa akizungumza na MTANZANIA, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye, alisema amekuwa akisikia maneno ya baadhi ya wanachama wakilalamika kuchelewa kuanza mchakato wa uteuzi wa majina ya wagombea ndani ya chama hicho wakati utaratibu bado haujafika.

"Maneno hayo nimekuwa nikiyasikia tukilaumiwa CCM kuchelewa kuanza mchakato wa uteuzi wa mgombea wa urais, lakini wanasahau kwamba muda wa uteuzi wa wagombea kwa taratibu za chama chetu bado haujafika," alisema Nape.

Aliongeza hali hiyo pia ilijitokeza katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2005 na 1995. Nape akatolea mfano wa uchaguzi wa mwaka 2005, ambapo alisema mgombea wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete aliteuliwa kuwania nafasi hiyo Mei 4, 2005.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, alisema muda wa kumtangaza mgombea wa urais ndani ya chama hicho bado haujafika.

"Kwa mujibu wa katiba ya chama chetu, muda wa kumtangaza mgombea wa nafasi ya urais ndani ya chama bado haujafika, jambo ambalo limetufanya hadi leo tushindwe kumtangaza mtu yeyote kuwania nafasi hiyo," alisema Dk. Slaa.

Alisema Chadema inaendeshwa kwa misingi ya sheria na kanuni, na kwamba hawawezi kufuata utaratibu wa vyama vingine ili waweze kumtangaza mgombea wao.
Dk. Slaa alisema kutokana na hali hiyo, wanachama wa chama hicho wanapaswa kusubiri muda uliopangwa ili waweze kumjua mgombea wao.

"Chama kina utaratibu na misingi yake, hatuwezi kukurupuka kufanya uamuzi bila ya kufuata utaratibu uliopo ambao unatupa mwongozo ili tuweze kutekeleza majukumu yetu kisheria na kikanuni," alisema.

Alisema hata kama CCM itaamua kumtangaza mgombea wa nafasi hiyo, wao bado wataendelea kusimamia misingi ya chama hicho inavyowataka.

Dk. Slaa alisema kila chama kinafuata utaratibu wake waliojiwekea, hivyo basi muda utakapofika watamtangaza mgombea wao. "Hata kama CCM wataamua kumtangaza mgombea wao leo, kama sisi muda wetu bado hatuwezi kumtangaza," alisema Dk. Slaa.

CUF waibuka
Akizungumzia uteuzi wa mgombea urais kupitia Ukawa, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Bara, Magdalena Sakaya, alisema kwa upande wao tayari wameshapendekeza jina la Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba kuwa mgombea wa urais ambaye anasubiri kupitishwa jina lake na vikao vya uamuzi vya chama.

Alisema jina la Profesa Lipumba litakwenda kupambanishwa na wagombea wengine wanaowakilisha Ukawa ili kuweza kupata jina la mgombea mmoja ambaye atapambana na wagombea wa vyama vingine katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba.

"Chama chetu kina jina moja la mgombea urais ambaye ni Profesa Lipumba ambaye atakwenda kupambanishwa na wagombea wengine wa Ukawa," alisema Sakaya.
Alisema Ukawa wamekubaliana kufanya mkutano mwishoni mwa mwezi huu ili waweze kupitisha jina la mgombea wa nafasi hiyo.

"Tuna vikao vyetu mwishoni mwa mwezi huu ambapo kila chama kitatangaza jina la mgombea wake ili waweze kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kumpata mgombea mmoja atakayewakilisha Ukawa katika uchaguzi mkuu," alisema Sakaya.

NCCR-Mageuzi na fomu
Akizungumzia uteuzi wa mgombea urais, Katibu Mwenezi wa Chama cha NCCR-Mageuzi, David Kafulila, alisema chama chao kimetoa fursa kwa wanachama wao kuchukua fomu kuanzia mwanzoni mwa mwezi huu.

Alisema wanachama wataendelea kuchukua fomu hadi Mei mwaka huu ambapo watafanya kikao kujadili majina ya waliojitokeza kuwania nafasi hiyo.

"Hadi sasa aliyejitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya urais ni Dk. George Kahangwa ambaye anasubiri wanachama wengine waweze kujitokeza ili waingie kwenye mchujo," alisema Kafulila.

Wakati CCM na Ukawa wakiendelea na mchakato wa kupata mgombea urais, tayari Chama cha Tanzania Labour (TLP) kimemtangaza Macmillan Lyimo kuwa mgombea wao.

Chanzo: Mtanzania (Fikra yakinifu)
 
kwa jinsi hali ilivyo kwa sasa ni kwamba UKAWA na CCM wanaviziana kutangaza wagombea wao wa urais,kila upande unataka mwenzake aanze kutangaza than wao wamalizie,alipouliza katibu mwenezi wa CCM nape nauye.alisema wao hawajatangaza mgombea kwa sababu taratibu zao za chama hazijakamilika na zitakapokua tayari watamtangaza mgombea wao hivyo wanachama wa CCM wasiwe na shaka alitolea mfano mwaka 2005 kuwa chama kilichelewa hivi hivi kupitisha mgombea na baadae april 2005 ndipo akapitishwa mh.jakaya kikwete kama mgombea wa CCM, Kwa upande wa pili UKAWA alipoulizwa ndugu slaa nae alikua na majibu kama ya nape kwamba nao hawajakamilisha mchakato wa kumpata mgombea wao na wanacho subiria ni kila chama kinachoundwa UKAWA kipendekeze jina la mgombea wake than majina hayo yatafanyiwa mchujo maalum na kumpata mgombea moja kwa tiketi ya UKAWA.ikumbukwe CUF wameshampitisha mh.lipumba kugombea urais. Ila ikumbukwe kuwa huu ni mwezi wa 4/5. kwani nini CCM na UKAWA wanaviziana?
 
Mkuu waache waviziane tu, ila naamini Ukawa hawatauangusha watanzania wengi tunaowaamini, mimi nina imani na Ukawa
 
CCM wanatafuta jinsi ya kumtosa Lowasa ili asishinde kwenye uchaguzi wao wa ndani kitu ambacho mpaka sasa kinawawia tabu kubwa kwani jamaa lina miguvu kuliko hata zaifu.
 
Ukawa wanasubili asimikwe makongoro nyere wamusimikie vicenti nyerere
 
ccm watajamba cheche tu no way out maana unaweza kujifanya unabana ushuzi katikati ya kadamnasi ukiogopa aibu ila mwisho wake ni kwamba ukipata njia inakuwa ni zaidi ya bastola
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…