Urais, Kongwa Jipya la Utumwa

Urais, Kongwa Jipya la Utumwa

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,768
Reaction score
49,934
Mataifa mengi Duniani, watu walipigana, watu walipoteza uhai na mali, walipoteza wapendwa wao, siyo kwa sababu ya kutaka kupata shule, barabara, hospitali, majumba, magari, umeme, maji n.k; bali kwaajili ya kuupata uhuru wao.

Wala hawakukubali kuyapitia magumu yote hayo ili wabadilishiwe mtu wa kuwanyima uhuru, yaani badala ya mzungu awe mweusi au wa kijani.

Watanzania, wazazi wao baada ya kuhangaikia uhuru. Uhuru huu ilimaanisha kuwa na maamuzi ya waongozwe namna gani, viongozi wapatikane kwa matakwa yao, maisha yao ya kila siku yamriwe na wao wenyewe, wajichagulie wanaowataka kuwaongoza, wapande taratibu za kupata haki zao pale miongoni mwao anapodhulumu, waweke utaratibu wa haki wa kuwatambua na kuwadhibiti wahalifu, n.k.

Kwa bahati mbaya, Watanzania, wamerudi kule kule kwenye ukoloni, tena ukoloni mbaya kuliko hata ule wa mzungu:

1) Mtanzania awe na kosa au hana kosa, polisi ana uwezo wa kumkamata, kumrundika ndani, na kwa kupitia DPP, anaweza kumfungulia mashtaka yoyote anayoyataka yeye, na mtuhumiwa akisota rumande hata miaka, huku polisi wakiendelea kusema uchunguzi unaendelea, bado haujakamilika. HIVI KUNA UKOLONI MBAYA KUUZIDI HUU?

2) Leo hii, mkuu wa Wilaya au Mkoa, anaweza kumwamuru Polisi amkamate raia yeyote kwenye eneo lake la uongozi na kumsweka ndani, hata kama sababu ni kwa sababu ya chuki za kugombania kimada. Utaswekwa ndani, akipenda, baada ya masaa 48, atamwamuru polisi akuachie. HIVI KUNA UKOLONI MBAYA KUUZIDI HUU?

3) Leo hii Rais akitaka anaweza kuwateulia watu wa kuja kuwatawala, mpende msipende, kuanzia mkoani mpaka wilayani (RC, RAS, RPC, DC, DAS, DED, OCD, n.k.). Wawe wana sifa za kuwa viongozi au hawana, iwe mnawataka au hamuwataki, mtataliwa kwa lazima. Hatukumchagua gavana, wala RC, wala DC, wakati wa ukoloni, je, leo tunawachagua? KUNA UKOLONI MBAYA ZAIDI YA HUU?

4) Leo hii, Rais anawateua majaji wote, Mwanashetia mkuu wa Serikali, jaji mkuu, jaji kiongozi, msajili wa mahakama, DPP, IGP, CDF, mkurugenzi wa TISS, n.k. Halafu unadanganywa kuwa eti unaweza kuishtaki serikali ila ili uishtaki, kwanza uombe kibali kwa serikali cha kuishtaki serikali. Na sisi tunaona ni sawa na inawezekana. Hivi kweli sisi tuna akili? Yaani unaenda mahakamani kabisa ukiwa na akili yako, kesi ipo chini ya jaji aliyeteuliwa na unayemshtaki, halafu eti unasubiria haki, hivi kuamini hilo kama linaweza kutokea, ni kwa sababu tumekuwa wajinga, wapumb.avu au wendawazimu? HIVI KUNA UKOLONI UNAOZIDI HUU?

Ukitizama kwa umakini, unaona dhahiri kuwa, Tanzania tulipigania kuwa huru kutoka kwenye ukoloni wa mwingereza ili tuwe kwenye ukoloni na utumwa wa weusi wenzetu, hata kama utakuwa mbaya zaidi kuliko hata ule wa mtu mweupe.

Leo kila kitu, ni Rais. Haulizwi, hashtakiwi, yupo juu ya sheria. Kwenye mazingira haya si afadhali hata gavana wa Kiingereza ambaye alikuwa anaweza kuhojiwa hata na malkia? Tuliutafuta uhuru au kongwa na utumwa wa kwetu wenyewe?
 
Ukoloni wa mtu mweusi kwa mweusi ni ukoloni mubaya, kuliko ule wa wazungu na makaburu
 
Kwa hiyo bora turudi kwenye ukoloni mkuu?
Kwa hali iliyopo sasa, kama tukihakikishiwa kuwa ndivyo itakavyoendelea kuwa, ni aheri kutawaliwa na watu wa nchi nyingine wenye dhamira njema.

Nini bora kwako, uambiwe uwe chini ya mtawala wa jamii yako, lakini hupo huru, unaweza kutengenezewa kesi wakati wowote, ukaozea jela au kuuawa AU uwe chini ya mtawala mgeni mwenye kukujali na kukupa haki zako zote kama mwanadamu?

Unakumbuka kile kisiwa ambacho wananchi walipewa uhuru wapige kura kuamua wawe huru au wawe chini ya Ufaransa, wakachagua kuwa chini ya Ufaransa? Unajua ni kwa nini? Waliona sisi waafrika wenzao tulio chini ya watawala weusi wenzetu, tunavyotendwa ovyo.
 
Ukoloni wa mtu mweusi kwa mweusi ni ukoloni mubaya, kuliko ule wa wazungu na makaburu
Ni kweli. Leo waafrika wanakimbia nchi zao ziluzo huru, kwenda Ulaya, kwa watu waliowatawala zamani.

Leo kukiwa na uchaguzi huru, wananchi waamue wanataka kuwa makoloni ya nchi za Ulaya au mataifa huru, wengi watachagua ukoloni.
 
Wakoloni sio wabaya, ila ndugu weusi wenzetu ni kirusi hatari sana, hata ofisini ma Team leader walikuwa wazungu, walikuwa fair, ila wabongo wenzetu ilikuwa mwendo wa Roho mbaya aisee
 
Mataifa mengi Duniani, watu walipigana, watu walipoteza uhai na mali, walipoteza wapendwa wao, siyo kwa sababu ya kutaka kupata shule, barabara, hospitali, majumba, magari, umeme, maji n.k; bali kwaajili ya kuupata uhuru wao.

Wala hawakukubali kuyapitia magumu yote hayo ili wabadilishiwe mtu wa kuwanyima uhuru, yaani badala ya mzungu awe mweusi au wa kijani.

Watanzania, wazazi wao baada ya kuhangaikia uhuru. Uhuru huu ilimaanisha kuwa na maamuzi ya waongozwe namna gani, viongozi wapatikane kwa matakwa yao, maisha yao ya kila siku yamriwe na wao wenyewe, wajichagulie wanaowataka kuwaongoza, wapande taratibu za kupata haki zao pale miongoni mwao anapodhulumu, waweke utaratibu wa haki wa kuwatambua na kuwadhibiti wahalifu, n.k.

Kwa bahati mbaya, Watanzania, wamerudi kule kule kwenye ukoloni, tena ukoloni mbaya kuliko hata ule wa mzungu:

1) Mtanzania awe na kosa au hana kosa, polisi ana uwezo wa kumkamata, kumrundika ndani, na kwa kupitia DPP, anaweza kumfungulia mashtaka yoyote anayoyataka yeye, na mtuhumiwa akisota rumande hata miaka, huku polisi wakiendelea kusema uchunguzi unaendelea, bado haujakamilika. HIVI KUNA UKOLONI MBAYA KUUZIDI HUU?

2) Leo hii, mkuu wa Wilaya au Mkoa, anaweza kumwamuru Polisi amkamate raia yeyote kwenye eneo lake la uongozi na kumsweka ndani, hata kama sababu ni kwa sababu ya chuki za kugombania kimada. Utaswekwa ndani, akipenda, baada ya masaa 48, atamwamuru polisi akuachie. HIVI KUNA UKOLONI MBAYA KUUZIDI HUU?

3) Leo hii Rais akitaka anaweza kuwateulia watu wa kuja kuwatawala, mpende msipende, kuanzia mkoani mpaka wilayani (RC, RAS, RPC, DC, DAS, DED, OCD, n.k.). Wawe wana sifa za kuwa viongozi au hawana, iwe mnawataka au hamuwataki, mtataliwa kwa lazima. Hatukumchagua gavana, wala RC, wala DC, wakati wa ukoloni, je, leo tunawachagua? KUNA UKOLONI MBAYA ZAIDI YA HUU?

4) Leo hii, Rais anawateua majaji wote, Mwanashetia mkuu wa Serikali, jaji mkuu, jaji kiongozi, msajili wa mahakama, DPP, IGP, CDF, mkurugenzi wa TISS, n.k. Halafu unadanganywa kuwa eti unaweza kuishtaki serikali ila ili uishtaki, kwanza uombe kibali kwa serikali cha kuishtaki serikali. Na sisi tunaona ni sawa na inawezekana. Hivi kweli sisi tuna akili? Yaani unaenda mahakamani kabisa ukiwa na akili yako, kesi ipo chini ya jaji aliyeteuliwa na unayemshtaki, halafu eti unasubiria haki, hivi kuamini hilo kama linaweza kutokea, ni kwa sababu tumekuwa wajinga, wapumb.avu au wendawazimu? HIVI KUNA UKOLONI UNAOZIDI HUU?

Ukitizama kwa umakini, unaona dhahiri kuwa, Tanzania tulipigania kuwa huru kutoka kwenye ukoloni wa mwingereza ili tuwe kwenye ukoloni na utumwa wa weusi wenzetu, hata kama utakuwa mbaya zaidi kuliko hata ule wa mtu mweupe.

Leo kila kitu, ni Rais. Haulizwi, hashtakiwi, yupo juu ya sheria. Kwenye mazingira haya si afadhali hata gavana wa Kiingereza ambaye alikuwa anaweza kuhojiwa hata na malkia? Tuliutafuta uhuru au kongwa na utumwa wa kwetu wenyewe?
Mkuu kwanza hongera kwa mada nzuri na inafikirisha. Hivyo ni jukumu letu sisi wa Tanzania kupigania katiba yenye kujali matakwa ya wananchi kuliko hii inayowapa watu wachache mamlaka makubwa.
Hivyo tupaze Sauti zetu, nguvu na juhudi mpaka ipatikane na uhuru wa kweli utakuwa umepatikana.
Ahsante!
 
Bahati mbaya, hawataki hata sauti za kudai katiba nzuri, zisikike. Kila anayepaza sauti lazima ukitane na mkono wa chuma.
 
Mkuu kwanza hongera kwa mada nzuri na inafikirisha. Hivyo ni jukumu letu sisi wa Tanzania kupigania katiba yenye kujali matakwa ya wananchi kuliko hii inayowapa watu wachache mamlaka makubwa.
Hivyo tupaze Sauti zetu, nguvu na juhudi mpaka ipatikane na uhuru wa kweli utakuwa umepatikana.
Ahsante!
Kizazi cha ajabu kabisa hiki.Hata maana ya kudai Uhuru haipo tena.Cha ajabu utaona kila ukifika 9 December watu wanajazwa uwanja wa Uhuru ili eti wajulishwe mafanikio tuliyoyapata utafikiri wao hawana macho ya kuona hayo mafanikio kama kweli yapo.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Mkoloni mweupe alituletea maendeleo akatunyima UHURU, mkoloni mweusi akupi vyote
 
Primitive society, bado sisi wote ni maprimitive.....ndani ya kundi la maprimitive huwezi kupata kiongozi asiye primitive..
Mimi,wewe na wengine tukijichunguza tutajiona pia maprimitive na kama sio sisi basi ndugu zetu ambao hata wala sio viongozi,wapo huku mtaani ni maprimitive tu...

Haya maneno ya kiingereza, Civilization na Primitive society yapo kwa sababu hizi jamii zipo...Africa yote bado iko kwenye primitive stage na itachukua miaka miiingi kuingia kwenye civilization society...

Leo hii tunawalalamikia sana walio kwenye system kwa maana ya Serikali na CCM lakini ukiangalia wengi wao ni ndugu zetu na huku mitaani tunashangilia mafanikio yao pamoja na kuwezeshwa koo zetu kimaisha, Tabia zile zile walizo nazo walio kwenye mifumo na CCM ndio tabia zilezile tulizonazo ambao tuko nje ya mfumo kwa maana mitaani na vyama vya siasa...Ni tabia zilezile za hovyohovyo, wizi, ubinafsi, umalaya, uzinzi, ufisadi, udikteta, unafiki, udini, ukabila nk....Tabia zote hizo ni mali ya WaAfrica..

Bado natafuta nchi moja ya Africa yenye WaAfrica weusi ambayo imeendelea na watu wake hawana tabia sawa na WaAfrica wengine walio Tanzania...Binafsi Africa naiona sawa na watu wake wako na tabia zilezile zinafanana na hii chanzo chake ni UPRIMITIVE WA WAAFRICA..
 
Udini, Watanzania wengi ni wadini...angalia wapo wakristo ambao wanabagua waislam kwa siri na hawawezi kutoa opportunity kwa muislam na wana mipango ya siri dhidi ya waislam ambao ni weusi wenzao..
Wapo Watanzania ambao ni waislam wanabagua watanzania wenzao wakristo ilihali wote ni weusi na wako tayari hata wamnyime opportunity mweusi mwenzie kwa kuwa ni mkristo na kumpa Muarabu au mhindi eti muislam mwenzie...HILI LIPO KWA WATANZANIA...na ndio maana ha UPRIMITIVE..

Ukabila,.. Watanzania wengi ni makabila na hata akipewa taasisi aiongoze atajaza watu wa kabila lake hata kama ni taasisi ni nyeti, itakuwa hivyo mpaka wasaze... HUU NI UPRIMITIVE..
 
Juzi nimepita sehemu moja London nikaona vijana kama kumi hivi wakiwa wanapita barabarani
Mimi nilikuwa na mwezangu tukitokea hotel ya jirani
Walikuwa hawaongei English bali lugha yao ambayo nimewahi kuisikia mara nyingi Amharic

Walikuwa ni vijana wadogo wa ki Ethiopia wakiwa na furaha sana
Tukajiuliza na mwenzangu kuwa hawa ndio wale vijana waliopita mpaka kwetu na wengine wakakamatwa na kuibiwa mali zao na wengine kuitwa majina ya kila aina kama wakimbizi, wahamiaji haramu nk

Leo wamepita France na kuingia wakiwa na furaha kibao tofauti na huko walikopita kwa so called ndugu zao na kadhia walizokutana nazo

Badala ya kuwahurumia na kuwasaidia ndio kwanza wanafungwa

Kwa kweli bora ukoloni kuna nidhamu

Sisi tumekataa kubadilika na bila kuwa mwizi na katili unaona hujawa mtu

Mpaka Rais anasema kwanini wengi wanataka ajira polisi? Why
 
Mataifa mengi Duniani, watu walipigana, watu walipoteza uhai na mali, walipoteza wapendwa wao, siyo kwa sababu ya kutaka kupata shule, barabara, hospitali, majumba, magari, umeme, maji n.k; bali kwaajili ya kuupata uhuru wao.

Wala hawakukubali kuyapitia magumu yote hayo ili wabadilishiwe mtu wa kuwanyima uhuru, yaani badala ya mzungu awe mweusi au wa kijani.

Watanzania, wazazi wao baada ya kuhangaikia uhuru. Uhuru huu ilimaanisha kuwa na maamuzi ya waongozwe namna gani, viongozi wapatikane kwa matakwa yao, maisha yao ya kila siku yamriwe na wao wenyewe, wajichagulie wanaowataka kuwaongoza, wapande taratibu za kupata haki zao pale miongoni mwao anapodhulumu, waweke utaratibu wa haki wa kuwatambua na kuwadhibiti wahalifu, n.k.

Kwa bahati mbaya, Watanzania, wamerudi kule kule kwenye ukoloni, tena ukoloni mbaya kuliko hata ule wa mzungu:

1) Mtanzania awe na kosa au hana kosa, polisi ana uwezo wa kumkamata, kumrundika ndani, na kwa kupitia DPP, anaweza kumfungulia mashtaka yoyote anayoyataka yeye, na mtuhumiwa akisota rumande hata miaka, huku polisi wakiendelea kusema uchunguzi unaendelea, bado haujakamilika. HIVI KUNA UKOLONI MBAYA KUUZIDI HUU?

2) Leo hii, mkuu wa Wilaya au Mkoa, anaweza kumwamuru Polisi amkamate raia yeyote kwenye eneo lake la uongozi na kumsweka ndani, hata kama sababu ni kwa sababu ya chuki za kugombania kimada. Utaswekwa ndani, akipenda, baada ya masaa 48, atamwamuru polisi akuachie. HIVI KUNA UKOLONI MBAYA KUUZIDI HUU?

3) Leo hii Rais akitaka anaweza kuwateulia watu wa kuja kuwatawala, mpende msipende, kuanzia mkoani mpaka wilayani (RC, RAS, RPC, DC, DAS, DED, OCD, n.k.). Wawe wana sifa za kuwa viongozi au hawana, iwe mnawataka au hamuwataki, mtataliwa kwa lazima. Hatukumchagua gavana, wala RC, wala DC, wakati wa ukoloni, je, leo tunawachagua? KUNA UKOLONI MBAYA ZAIDI YA HUU?

4) Leo hii, Rais anawateua majaji wote, Mwanashetia mkuu wa Serikali, jaji mkuu, jaji kiongozi, msajili wa mahakama, DPP, IGP, CDF, mkurugenzi wa TISS, n.k. Halafu unadanganywa kuwa eti unaweza kuishtaki serikali ila ili uishtaki, kwanza uombe kibali kwa serikali cha kuishtaki serikali. Na sisi tunaona ni sawa na inawezekana. Hivi kweli sisi tuna akili? Yaani unaenda mahakamani kabisa ukiwa na akili yako, kesi ipo chini ya jaji aliyeteuliwa na unayemshtaki, halafu eti unasubiria haki, hivi kuamini hilo kama linaweza kutokea, ni kwa sababu tumekuwa wajinga, wapumb.avu au wendawazimu? HIVI KUNA UKOLONI UNAOZIDI HUU?

Ukitizama kwa umakini, unaona dhahiri kuwa, Tanzania tulipigania kuwa huru kutoka kwenye ukoloni wa mwingereza ili tuwe kwenye ukoloni na utumwa wa weusi wenzetu, hata kama utakuwa mbaya zaidi kuliko hata ule wa mtu mweupe.

Leo kila kitu, ni Rais. Haulizwi, hashtakiwi, yupo juu ya sheria. Kwenye mazingira haya si afadhali hata gavana wa Kiingereza ambaye alikuwa anaweza kuhojiwa hata na malkia? Tuliutafuta uhuru au kongwa na utumwa wa kwetu wenyewe?
NAMLAUMU BABAKO KUTOKUTUMIA KONDOM WAKATI WA MIMBA YAKO, HUKUTAKIWA KUZALIWA..
 
Back
Top Bottom