chokambayaa
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 543
- 69
Aslam aleykum ma dokta wote wa humu ndani!
naomben ushauri wenu mke wangu amepata tatizo mwili hauna nguvu na anakuwa mchovu sana kapimwa na imeonekana damu imepungua ipo ml 8. Nn kinasababisha damu kupungua? Hosp. Gani naweza kupata matibabu ya kujua chanzo? Nn afanye damu iongezeke kwa haraka?
ahsanten wana JF nategemea msaada toka kwenu
kwani alikuwa anaumwa au mjamzito hivi karibuni? ulaje wake unauonaje?
Damu inaweza kupungua bila hata ya ugonjwa. Kwa mfano:
¤ uzalishwaji duni wa chembe nyekundu za damu, ikiwa mtu hakula mboga mboga na matunda;
¤ mwanamke kupoteza madini ya chuma mwilini kupitia hedhi, hususani kama alitoa damu nyingi;
¤ kuharibika kwa chembe nyekundu za damu kutokana na matatizo ya kurithi, au madhara ya utumiaji wa baadhi ya dawa, dawa zinazoathiri sehemu laini ya mifupa (borne marrow);
¤ kupoteza damu kwa sababu ya minyoo (Hookworms);
¤ mwanamke kuwa mjamzito. Ujaurito unapelekea mabadiliko makumbwa mwilini, ikiwamo kuongezeka kwa maji na kupungua kwa haemoglobini;
¤ N.K
Ale maini yaliyochemshwa kidogo yasiive sana,juice ya ribena,alovera,na maua
nafikil si 8ml. hata panya ana zaidi ya 8ml za damu. binadamu ana karibia litter 5 amabzo ni 5000ml za damu katika mwili. nafikiri unaongelea haemoglobin 8g/dl. mpeleke kwa daktari akamchunguze then utapata jibu kiurahisi. katika mtandao hu damu haitaongezeka. mpende mkeo.[/QUOTE
nampenda kuliko unavyofikiria na kuuliza huku haina maana kuwa sijaenda hosp. Ndo maana ktk JF kuna JF Dokta
kama huna majibu potezea!!!
kama hana appetite ina weza likawa tatizo, mtafutie vyakula vyenye madini ya chuma na folic acid kwa wingi
(google that!). nakushauri usimlishe maini yasiyoiva vizuri utamletea magonjwa mengine
pole sana mkuu,niende moja kwa moja namna ya kulizuia,ukiweza tafuta vifuatavyoAslam aleykum ma dokta wote wa humu ndani!
naomben ushauri wenu mke wangu amepata tatizo mwili hauna nguvu na anakuwa mchovu sana kapimwa na imeonekana damu imepungua ipo ml 8. Nn kinasababisha damu kupungua? Hosp. Gani naweza kupata matibabu ya kujua chanzo? Nn afanye damu
iongezeke kwa haraka?
ahsanten wana JF nategemea msaada toka kwenu