Upotoshaji wa ukweli haufai

NOTBOOK

Member
Joined
Sep 7, 2013
Posts
6
Reaction score
4
UPOTOSHAJI WA UKWELI HAUFAI
Ndugu zangu watanzania napenda kuwapa pole kwa kazi nzuri mnazozifanya ili kuakikisha Taifa letu linasonga mbele.Pili napenda kuwasuta watanzania wenzetu ambao kazi yao imekuwa kutapanya mali ya umma(Kama panya) kwa manufaa yao na pindi taarifa zinaposikika masikioni wa watanzania wema na kuanza kuhoji watu hao (watanzania wasaliti) hutafuta kila namna kuakikisha wanavumisha maneno mengi ili kuakikisha jamii husika inabaki kujadili maneno hayo badala ya kujadili kuhusu wezi na wanafiki wakubwa hao, mbinu hii imekuwa ikifanyika kwa utaalamu wa hali ya juu
Mfano kuyafungia baadhi ya magazeti,kuua waandishi wa habari,kuficha wezi na kusema wamekufa kumbe bado wanaishi n.k lakini pamoja na jitihada zao za kishetani bado wapo watanzania ambao wamekuwa wakingamua kwa kuchambua mchele na pumba na kuendelea kuhoji walengwa na huku watanzania walio wengi hasa waishio vijijini ambao wao mara nyingi hushindwa kupata taarifa za kweli,mbinu hizi chafu zimesababisha hupotevu wa mabilioni ya watanzania na kuiweka nchi katika tabia ya kuombaomba jambo ambalo mimi binafsi silipendi kuanzia ngazi ya kifamilia hadi ya kitaifa.Hivyo nawaomba watanzania wema tuendelee kuutafuta ukweli na kuuweka adharani bila kumpa nafasi mtu yoyote asiyeitakia mema Tanzania kupotosha umma wa watanzania na huku wakiendelea kutapanya mali zetu.
“UKWELI UTAKUWEKA HURU DAIMA”
 
Nakuunga mkono mkuu ingawaje ni kilio cha samaki machozi........!!!!!!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…