MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,255
- 8,027
Hili ni swali ambalo kwa watu wenye akili nyepsi(Simple minds) hulipatia majibu ya haraka haraka bila kufikiri kwa kina, wazungu hunena kwa usemi usemao " Simple minds discuss people" yaani akili nyepesi huishia akizungumza watu, kwa kiswahili huitwa ni majungu!
Kwa watu wenye akili thabiti huongelea matukio( Complex minds discuss events) yaani hapa kwa akili nyepesi unaweza kufikiri kwauda huu mfupi ambao Rais mteule Ndg Mafuli ameingia madarakani kuamua kufumua fumua Yale ambayo miaka yote hua hayapendi ndo kunaweza kuleta sura mpya ya Chama cha mapinduzi, hapa watu walipaswa waangaliie matukio zaidi na sio kuishia kulijadili jina la Magufuli muda wote! Hapa sio kuifufua CCM pekee!
Ikumbukwe kwamba Rais huyu anayo mitihani mikubwa sana ndani na nje ya chama chake kwani anajua siku zote "kikulacho ki-nguoni mwako" Hapa la kutazamwa kubwa ni kwamba wengi wanaomzungumza kwa wema ni wale wamaccm wa ukweli pamoja walio nje ya CCM! hawa ndio friends of Magufuli wa kweli.
Magufuli kukamilisha ahadi zake alizoahidi kwa Wananchi ni lazima akubaliane na baadhi ya mambo ambayo upinzani imekua ukiyalilia siku zote na ambayo kimsingi wale CCM kindaki (CCM maslahi) hawayataki tena kwa bahati mbaya sana CCM kindaki ndaki si watu wadogo hata kidogo!Tena ni wale ambao baadhi yao ameshaanza kuona ngozi na Rangi zao kwenye matukio yake haya ambayo Wananchi wanayashangilia.
Faida kubwa kwa upinzani ni pale Magufuli kapoamua kuwasikilaza zaidi wananchi kwa kujali maslahi ya taifa zaidi kuliko ya kichama, hapa itambidi sasa atekeleze baadhi ya mambo ambayo upinzani umekua ukiyalilia miaka yote na CCM kindaki ndaki hawataki kuyasikia hata kidogo. Mfano hili suala la kuwazuia viongozi wa nchi kusafiri nje ya nchi na kuwazuia wabunge kua wajumbe wa bodi liwaumiza zaidi wamaccm wengi kuliko ilivyotegemewa, haijawahi kutokea ndani ya awamu zote za utawala chini ya CCM akatokea mtu wa kulipigia hili jambo kelele zaidi ya upinzani,hapa Magufuli amewachoma baadhi ya watu.
Upinzani sasa unapata nguvu sasa hata ya kuwaambia wamaccm tena kwa kujiamini ni kwanini haya miaka yote wamekua wakiyafumbia macho? Magufuli atakapozidi kutumbua majipu mengi zaidi ndiko kunapowapa wapinzani nafasi ya kutengeneza hoja nyingi zaidi kuendelea kuibua mazito zaidi ambayo hata kwa hakika Magufuli atawaunga mkono kwa maslahi mapana ya taifa. Hii hali ya kuona Magufuli anaenda pamoja na matakwa ya wapinzani inaweza kuleta migongano na hatimaye migawanyiko mingi ndani ya CCM.
Kwa vyovyote vile endapo Magufuli atasikiliza na kuzingatia zaidi maagizo ya chama chake hataweza kuendana na kasi yake anayoitaka maana atafungwa na minyororo ya chama chake na kuanza kushindwa kutekeleza Yale aliyoyaahi kwa watanzania na hali kurudi kule kule alikotoka Mtangulizi wake! hapa itaanza ninong'ono mingi kama ilivyokua kwa Mtangulizi wake na kuwapa wapinzani nguvu ya kujipanga zaidi.
Pamoja na baadhi ya wapinzani kusifu juhudi za Magufuli sio kwamba wao hawapendi kuongoza laahasha! Katika kipindi ambacho CCM wanatakiwa kujipanga kuliko hata nyuma ni hiki maana kwa haya anayoyafanya Magufuli wapinzani wako makini sana kufuatilia nyendo zake mguu kwa mguu kutafuta madhaifu yake ili baadaye wapate cha kuwaambia Wananchi, pia hiki ni kipindi ambacho CCM wanaweza kubweteka kutokana na Magufuli kuaminiwa na wananchi wakidhani atakua Rais milele.
CCM wanachofikiri zaidi kwa sasa ni kua kasi ya Magufuli ndiyo itakayoua upinzani huku wao wakiweka mikono mifukoni, wanasahau kwa sasa ndio kipindi hasa ambacho wapinzani wako field kujiimarisha zaidi kutafuta mwarobaini wa CCM! Inawezekana kabisa kwa sasa anayezungumzwa zaidi ni Magufuli kuliko CCM, wamesahau kua CCM ni taasisi yenye mfumo wake,utendaji ndani ya Chama pia unahitaji mtu kama Magufuli, kama kuna kitu kibaya CCM wanataka kukijaribu ndani ya chama wasimpe Magufuli uenyeketi wa chama taifa! Anatakiwa apewe nafasi ndani ya Chama apewe rungu aibue na madudu mengine huko.
Kwa akili ya mtu anayefikiria kwa kutumia "Complex mind" kwa kuangalia matukio hawezi kusema sasa ni muda wa upinzani unakufa! Ikumbukwe kua kuna viongozi wa upinzani nchini ambao wanapata mafunzo ya kuviendesha vyama kutoka vyama washirika vya nchi ambazo upinzani umekomaa na umeongoza dola mara nyingi, hapa wanafundishwa hata namna ya kumaintain siasa za ushindani hasa pale kunapokua na changamoto kubwa ya ushindani.