Upinzani Tanzania una safari ndefu sana

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
24,501
28,703
Hebu angalia matokeo ya uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa uliofanyika wilayani KASULU leo hii:

1. Kata ya ya H/juu-Mtaa wa Nyakelera, CCM 202, ACT 80

2. Kata ya Nyumbigwa-Mtaa wa Tumaini, CCM 79, Chadema 65 na ACT 5

3. Kata ya RUHITA mtaa wa Mungoma, CCM 48 na ACT 5.

4. Kata ya Murusi - Mtaa wa Kwizera, CCM 68 na NCCR 4.

My Take Yaani wamepigwa 4-0, huu ni mwendelezo wa magoli baada ya 20 - 1ya uchaguzi mdogo.

Watanzania huwa wana maamuzi magumu na ya busara sana, mpaka unaweza kudhani hakuna vyama vya upinzani nchini.

Asante wananchi wa Kasulu kwa heshima kubwa mliyoionyesha kwa Chama Cha Mapinduzi
 
Everything credible in life is earned by sweat....upinzani kama unataka kujitofautisha lazima uwe na watu wanaomaanisha wanayofanya....napata shida sana n.a. hawa wana siasa wanaokula wasipofanyia kazi....as if this life is a free riding game
 
Everything credible in life is earned by sweat....upinzani kama unataka kujitofautisha lazima uwe na watu wanaomaanisha wanayofanya....napata shida sana n.a. hawa wana siasa wanaokula wasipofanyia kazi....as if this life is a free riding game
Upinzan kwa Tz Upo kuongeza kura za uraisi ili kupata ruzuku ,haupo kuweka mikakati ili kushinda uraisi.
 
Unasafi ndefu kama vile CCM ilivyowapitisha Watanzania kwenye safari ndefu ya mateso (miaka zaidi ya 40) bila mafanikio yoyote
 
Serikali gani duniani watu wake walipitishwa kwenye raha ? Hebu acheni uvivu fanyeni kazi
You must be drunk or on drugs. Chama chakavu hakijafanikiwa kumjengea mtanzania mazingira ya kujikwamua for as long as i can remember. Serikali yako ya chama chakavu haina sera nzuri kutumia rasilimali kuitoa hii nchi kwenye lindi la ufukara. Go and tell your masters
 
Tatizo aina ya watu wanaosimamishwa na upinzani ni shida ndio maana Watanzania wanafanya maamuzi magumu ya kuipa kura CCM.
 
Back
Top Bottom