sbikore
JF-Expert Member
- Feb 13, 2015
- 535
- 191
Watanzania wote tulishuhudia figisufigisu nyingi na kwa wana siasa wengi hasa kwa kambi ya upinzani katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu 2015.Lakini pia hali hiyo iliendelea kutokea hata katika kipindi na baada ya uchaguzi huo mkuu.
Moja ya mambo makubwa yaliyojiri ni lile la kumfutilia uanachama ndugu zitto kabwe ndani ya chadema,na kwa wakati huo mashabiki wa chama walimwita msaliti wa chama kila kona ya nchi na ikampelekea kukaa kimya na kwa sehemu kubwa ukazikwa umaarufu wa muda alioupata akiwa chadema.
Lingine,ni katika kipindi cha uchaguzi,walijiengua nafasi zao baadhi ya viongozi katika nyadhifa zao ndani ya chama/vyama vyao vya siasa.
Ibrahim Lipumba alisambaratika katika nafasi ya juu ndani ya chama chake ikiwa ni pamoja na kuiuwa ukawa.Kwa hiyo halikuwa pigo dodo kwa muungano huo.Kama ilivyo ada ya mashabiki walimwita mchovu na kwamba alishapoteza ladha na hata kujiengua kwake hakuna madhara ndani ya chama na hata ukawa.
Dr.Wilbroad Petter Slaa naye alijiengua katika nafasi ya ukatibu mkuu chadema na kuamua kuachana nao baada ya yy kuapa kutokula matapishi yake(mnayajua wana chadema).Pamoja na umuhimu waliompa ndani ya chama kwa vipindi vyote,lakini hawakuisha kumdhihaki sana,na kwa kashfa kubwa na hata watumishi wa bwana walidiriki kutoa mikanda iliyoelezea siri za hata ndani kwake,japo wapo baadhi ya mashabiki waliumizwa sana na vitendo hivi alivyotendewa mzee huyu.
Sasa kinachonishangaza mm hapa ni hii style wanayotokanayo hawa wapinzani.Na zaidi siwashangai viongozi wa vyama,bali hawa mashabiki ambao naamin sasa hawana dira wala mwelekeo.
Zitto kabwe waliyemkataa,leo ni mtu maarufu anayejinasibu tena ikiwezekana hata kutumia sera za ukawa alimradi tu kutengeneza maslahi yake na baadaye yake ya kisiasa.Kanuni za bunge alizozishiriki kuzitunga,amezivunja mwenyewe kwa maksudi,zimemtupa nje ya uwanja na sasa anaona namna ya kujisafisha kwa mashabiki wajinga ni kuendesha mikutano hata chooni alimradi tu aeleze uongo alionao,na unashangaa hawahawa mashabiki wajinga waliomdhihaki wakati anaenguliwa chadema wanaishia kumshangilia na kumpa majina yote ya sifa;Mara ooo...zitto ni jembe...mara..ooo...zitto ni mchumi aliyebobea,na sifa nyingi kedekede kana kwamba hawakuziona enzi zile(.....).Sasa anafanya uchochezi baina ya serikali na wananchi,lakini pia taharuki kwa wananchi kutotulia na kunufaika na matunda ya chaguo lao(John Pombe Magufuli).Hata kitendo tu cha kuhojiwa na polisi basi wale madebe tupu utawasikia katika ubora wao....
Lipumba kwa ridhaa yake aliondoka baada ya kuchukizwa na kitendo cha chadema kumpokea mh.Lowasa,na kwamba yy hakuwa tayari kumuunga mkono maana ni fisadi(kama alivyosema).Aliandika barua kwa mkono wake na akaamua kujiudhuru nafasi yake ya uenyekiti wa chama,na sii hivyo tu,aliamua kukaa kimya mpaka bingwa wa uchaguzi anatangazwa kuwa ni Mh.John Pombe Magufuli.Kwa kipindi hicho alijitahidi kujikweza kwa karibu sana kwa kiongozi huyu wa nchi akidhani anawezateuliwa kwa nafasi yoyote(Presidential apointment).Kadri muda unasogea,ndoto yake imezima na wote tumemshudia jana kwa mara ya kwanza anaomba kutenguliwa kwa barua aliyoiandika ya kujiudhuru nafasi yake.Je anaweza kutupa majibu ya maswali haya;
1.Kama anarudi yuko tayari kuendelea na muungano wa kivyama(UKAWA)?
2.Kama jibu la hapo juu ni ndio,anaweza kituthibitishia kwamba aliyempelekea kuondoka wakati huo kwa sasa hayupo ndani ya chadema?na kma jibu ni hapana,sasa ameamua kula matapishi?
3.Licha ya kutengua maamzi ya barua yake,yuko tayari kuwa mwanachama wa kawaida ndani ya chama na sii kiongozi wa ngazi ya juu?kama jibu ni hapana asipokelewe maana dhahiri huyu ni mchumiatumbo.
Utatu wa viongozi hao juu ni taswira ya wapigania madaraka ya juu ya nchi hii na ndio maana kila iitwapo leo wao wanakila mbinu za hila kuhakikisha wanaidhoofisha serikali inayokuwa madarakani kwa lengo la kujiinua kisiasa.Hawana jema chini ya jua,hawatosheki na walichopewa na hawawatakii mema watanzania.
Wote kwa pamoja,kila mmoja kwa nyakati tofauti waliwahi kutangaza nia ya kugombea uraisi,na wengine wameendelea kuwa wagombea wa kudumu wa nafasi hii kupitia vyama vyao na wamepokea ruzuku nyingi na kwa vipindi tofauti wakijinufaisha na matumbo yao.Tumewachokaaa....
Nawazungumzia watatu hao c kwa maana wengine hawapo,hapana ni kwa sababu naona harakati zao na hasa kwa wakati huu,sii za nia njema na watanzani,na kama hatutakuwa makini zitatupelekea kwenye hatua nyingine.
Wanadai demokrasia ya kitaifa lakini kwa upande wa vyama vyao wamebana demokrasia vilivyo na ndio maana kila cku utawasikia wao tu.Hivi vyama vyenu hivi havina wanasiasa machipukizi?mbona hamjiulizi maswali haya?
Tofauti na ccm kila cku watu wanaachiana nafasi,na hatuna mmiliki wa chama ss.Hiki ni chama cha watu wote,chenye demokrasia pana ambapo kila mtu anaweza kukikosoa,kumkosoa kiongozi na mienendo yake alimradi tu asionewe,na hutosikia mtu kuvuliwa uanachama kwa sababu nyepesinyepesi tu kama walivyo chadema.
Nimeyasema haya kama fursa ya pekee ya kuwataka watanzania waamke/wajitambue,wawapuuze hawa wasakatonge.
Lakini zaidi waunge juhudi za rais wetu mpendwa katika harakari za ukombozi kiuchumi kuliko kupoteza muda mwingi kuwasikiliza wanasiasa uchwara waliopoteza mwelekeo(wasakatonge)
Mwisho niitumie fursa hii kuwaomba watanzania kukiunga mkono chama cha mapinduzi kwa misingi yake imara na kupata matumaini makubwa kwamba ndicho chama pekee kilichoweza,kinachoweza na kitakachozaa viongozi makini na wazalendo wenye nia ya kuwahudumia watanzani kwa maendeleo endelevu.
Viva magufuli
Viva ccm