Kagondo
JF-Expert Member
- Jun 6, 2016
- 296
- 79
Muda sahihi wa kupata mwenzi mpya, baada ya kuachana na wa zamani inafaa mtu atulie kwa muda gani kwanza?
Umeleta mada nzuri ila umeshindwa kuijazia wigo sahihi ili wachangiaji wakupe jibu mujarabu. Hebu tafakari katika nyigo hizi ya kwako ipo eneo gani
1a- Ni muda gani sahihi wa kupata mwenza baada ya kufiwa na mume/mke?
1b - Ni muda gani sahihi wa kupata mwenza baada ya kuachana/kutalikiana na mke au mume?
2- Ni muda gani sahihi wa kuwa na mwenza baada ya kuachana na mchumba tuliyekuwa tukielekea kwenye ndoa?
3- Ni muda gani sahihi wa kuwa na mwenza baada ya kuachana na by/girlfriend?
4- Ni muda gani wa kuwa na mwenza baada ya kuachana na mlupo/one-night stand?
Kwa nyigo hizo hapo juu nadhani majibu yatakuwa tofauti ukianzia na sababu ya kuachana, muda wa mahusiano yenu kabla ya kuachana na mwisho malengo ya mahusiano yenu kabla ya kuachana.