upendo baina ya watu huwa haufi hata kidogo unless kama hujampenda mtu,kinachotokea ni kupanda ama kushuka kwa kiwango cha upendo baina ya mtu na mtu.
upendo unapokua katika kiwango cha juu wapendanao huwa katika fikra chanya kiasi cha kufikiria duniani kuna watu wawili tu ambao ni wao wenyewe,hapa ndo mmoja wao anapenda kumuona,kumsikia ama kupata ujumbe toka kwa mwenzi wake kila mara na lisipofanyika hilo hujiona hana umuhim wowote na hapendwi.
upendo unaposhuka wapendao huona dunia kama jalala vile na hapo mmoja wao anakua hana hamu ya kumuona,kumsikia ama kupata ujumbe toka kwa mwenzi wake,hali ikiwa hivi hata upige simu vipi haitapokelewa,kama ni msg haitajibiwa na ikitokea msg inajibiwa majibu yatakua negative.Hali hii hua ni ya muda tu kama ulimpenda mtu kwa dhati,ndo maana unaweza kugombana na mtu kufikia kuachana lakin baada ya miaka kadhaa kupita unashangaa x wako anakutafta na wengne kuendeleza mapenzi bila kujali wapo kwenye mahusiano mengne ama laa.
Tunapogombana na wenzi wetu hata kufikia kuachana tunatakiwa kutulia na kuusubiri upendo ulio chini uanze kuongezeka na mawasiliano kurejea
Haya ni machache niliobahatika kuyapata katika semina ya mahusiano,urafiki,uchumba na ndoa hapa Namibia.
Mmoja kati ya watoa semina alitudokeza kua upendo wa kweli huchukua muda na hupitia hatua tatu,UNAMPENDA MTU KWA KUMUONA KWA MACHO THEN MACHO YANATUMA UJUMBE KWENYE UBONGO NA MWISHOWE NI TENDO.KWA KIFUPI HATUA HIZI NI MACHO,UBONGO NA MWILI NA KILA HATUA INA MUDA WAKE.
Haya yametufanya wanasemina tutafakari mahusiano yetu tulipotoka na hatua tulizopitia japo mahusiano yana maelezo mengi na tofauti si mbaya nawe ukitafakari.............
N.B nimetumia simu kuwashirikisha ndugu zangu makosa ya kiuandishi yanaweza kuwepo