Tigershark
JF-Expert Member
- Oct 9, 2018
- 7,051
- 12,560
Sasa kuna watu nawashangaa wanakuja na hoja nyepesi kuwa hata Chato ni Tanzania! Mimi nilitegemea mtu aniambie hata Rais asingekuwa JPM basi miradi kama hiyo ingefanyika Chato kutokana na potential iliyoko huko kiuchumi!Ni jambo baya tulikemee.
Hoja yako imekaa kama mtu mwenye upeo na uwezo wa kujenga hoja.Sasa kuna watu nawashangaa wanakuja na hoja nyepesi kuwa hata Chato ni Tanzania!Mimi nilitegemea mtu aniambie hata Rais asingekuwa JPM basi miradi kama hiyo ingefanyika Chato kutokana na potential iliyoko huko kiuchumi!
Mtu akinishawishi kuwa Miradi inayoendelea Chato haina uhusiano na Rais kuwa mzawa wa Chato,nitamwelewa!
Umeongea ukweli mtupu japo hao jamaa wataweka pamba masikioni!Hoja yako imekaa kama mtu mwenye upeo na uwezo wa kujenga hoja.
Ni upumbavu wa hali juu kutetea huo uchafu unaoendelea huko Chato kwa hoja eti Chato nako ni Tanzania. Nina uhakika hoja ya namna hiii inatolewa na watu waliopungukiwa kichwani.
Sent using Jamii Forums mobile app
Labda wanataka ije kuwa Mkoa wa Chato na Geita iwe wilaya ndani ya Chato!😁😁Awamu hii lolote linawezekana!Cha kushangaza, miradi kama hii tulitegemea kama kuna ulaxima wa kufanya hivyo iwe Geita/mkoani, na si wilayani. Nini basi faida ya kuwa na mkoa ilhali miundo mbinu yote ipelekwe wilayani
Bandari kubwa inakaribia kukamilika Chato!Kinachofanyika sasa Chato, ni aibu kubwa kwa Rais, CCM, Serikali na kwa Taifa letu. Lazima uwe mwendawazimu hasa kuonga mkono uchafu huu unaoendelea sasa:
1) Bohari kuu ya madawa ya kanda MSD Chato
2) Hospitali ya ya Rilufaa ya Kanda Chato
3) Uwanja wa ndege wa kimataifa Chato
4) Uwanja wa mpira Chato
5) Mbuga ya wanyama ya kutengenezwa Chato
6) Kivuko cha kisasa Chato
7) Taa za kuongozea magari Chato
Sent using Jamii Forums mobile app
Akili wamezikali, wanasema Chato inapaswa kuwa kama Wuhan China!Hii nchi ni ya kipuuzi wana, wasomi wetu na PHD zao wanaunga mkono kinachoendelea Chato.
Hakuna wa kumfunga paka kengeleCCM NI TATIZO
BASHIRU NA TEAM YAKE WAPO USINGIZINI
Duh! Tumepatwa na laana. Ngoja niongeze kwenye list.Bandari kubwa inakaribia kukamilika Chato!
Bohari kubwa ya madawa MSD Chato, bandari nayo inakaribia kukamilika!Kwakweli no jambo baya sana. Hivi kila Rais afanye kwao kwa upendeleo hiyo nchi itakuwaje. Yafuatayo kwake
1. Uwanja wa ndege wa kimataifa
2. Hosptali kubwa ya Rufaa
3.uwanja mkubwa wa mpira
4. Daraja kubwa la busis Trilion 4
5. Chuo kikubwa ca Veta
6. Mbuga kubwa ya wanyama burigi
7. Mataa ya kuongoza magari
8. Kiwanda cha minofu ya samak
9. Majengo makubw CRDB,NMB, TRAA
10. Mkoa wa Chato, wakat wowote
Hayo yote wenzake waliomtangulia hawakufanya, maake Azimio la Arusha lilisema " CHEO NI DHAMANA, SITATUMIA CHEO CHANGU KWA MANUFAA BINAFSI" Waliogopa maadili, leo tunaona Chato imekuwa IKULU ya kupokelea mpk Maraisi, TUPAZE SAUTI , viningevyo atapeleka mpk Reli kwake. Tuamuke
Ndiyo maana mtu kama Kabudi namwona ni mjinga kumzidi aliyeishia darasa la 7 lakini ana akili. Hana faida kwa Taifa. Ni mbinafsi mkubwa. Yupo tayari kusifia haramu alimradi ashibishe tumbo lake.Hii nchi ni ya kipuuzi wana, wasomi wetu na PHD zao wanaunga mkono kinachoendelea Chato.
Hatari mojawapo kubwa ninayoiona iwapo tabia hii ya kupendelea Chato kunakofanywa na serikali, ni kwamba tutaanza kuchagua kiongozi kutokana na uzawa!
Mfano mimi ni wa Kusini, akigombea Rais wa kutoka kusini basi nitamchagua nikiamini atafanya upendeleo na kuelekeza miradi mingi kusini kuliko maeneo mengine! Hivyo kigezo cha kwanza itakuwa kabila na vingine ndio vitafuata!
Kinachofanywa na serikali ya JPM cha kuelekeza miradi mingi Chato ni cha kupigiwa kelele na kila Mtanzania kwa mustakabali wa umoja wa taifa letu!
Sio kwamba waliomtangulia hawakutamani kupeleka maendeleo walikozaliwa ila miiko na maadili ya kazi zao iliwasuta! Kodi tunalipa wote hivyo vipaumbele vipangwe kwa haki.