Tigershark
JF-Expert Member
- Oct 9, 2018
- 7,051
- 12,560
Hatari mojawapo kubwa ninayoiona iwapo tabia hii ya kupendelea Chato kunakofanywa na serikali ni kwamba tutaanza kuchagua kiongozi kutokana na uzawa!
Mfano mimi ni wa Kusini, akigombea Rais wa kutoka kusini basi nitamchagua nikiamini atafanya upendeleo na kuelekeza miradi mingi kusini kuliko maeneo mengine! Hivyo kigezo cha kwanza itakuwa kabila na vingine ndio vitafuata!
Kinachofanywa na serikali ya JPM cha kuelekeza miradi mingi Chato ni cha kupigiwa kelele na kila Mtanzania kwa mustakabali wa umoja wa taifa letu!
Sio kwamba waliomtangulia hawakutamani kupeleka maendeleo walikozaliwa ila miiko na maadili ya kazi zao iliwasuta! Kodi tunalipa wote hivyo vipaumbele vipangwe kwa haki.