Aaah! Kama ni hizo mkuu nimekuelewa na una haki ya kujua!!
Sijui kwa nini utendaji wa Bodi ya mikopo uko kivile bwana. Yaani kuna watu majina yametoka tangu mwezi uliopita kila wakiulizia kwa afisa wa mikopo hapa chuoni wanapambwa kwa maneno matamu tu bila utekelezaji (mara oh majina watu watasaini ijumaa mara oh sijui imekuwaje). Sijui serikali nayo ina hamu sana kushuhudia migomo maana naona zimepita siku nyingi hawajapambana na migomo ya kufa mtu!!