Huwa nashangaa sana ni kwanini watu wanategemea sana umeme wa TANESCO hasa wale wasio kuwa na matumizi makubwa, hapa namanisha matumizi madogo ya nyumbani kama kuwasha taa, TV, redio na kuchaji simu. Ni kwanini watu wasinunue Solar na kuweka majumbani badala ya kutegemea huu umeme wa TANESCO ambao tangu nimejitambua haujawahi kuwa wa uhakika.
Mwanga tunao wa kutosha, bei za solar si kubwa kiviiile, ila bado unakuta mtu analia lia na umeme wa TANESCO. Nchi za ULAYA wameendelea na umeme haujawahi kukatika kizembe, ila utakuta nyumba nyingi tu zina Solar pia. Ila sie ....ngoja niishie hapa.