Upagani wa kale katika usasa

Upagani wa kale katika usasa

hamis77

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
18,250
Reaction score
26,641
UPAGANI WA KALE KATIKA USASA

Ibada ya hija bila kuvaa chupi

Wapagani wa Maka naam makureshi walikuwa wanafanya hija wakiwa watupu (uchi wa mnyama). Na Waislamu leo wanahiji bila kuvaa nguo za ndani. Mtume wa kislamu Muhamad alizaliwa katika jamii ya makureshi na tena babu yake alikuwa kuhani mkubwa wa mungu wa Maka aliyejulikana kama Allah ama Hubal. Muhamad alipozaliwa, babu yake alimpleka mbele ya alkaaba (lililopo jiwe jeusi) na kumweka wakfu kwa Hubal/Allah na kumpa jina Muhamad kwa utukufu wa Hubal. Hubali ndio mungu Baal katika Biblia aliyetolewa kafara za watoto.

Muhamad ameishi Maka kwa miaka 40 akishuhudia matendo yote hayo na akishiriki kutatua migogoro ya kikabila ya kugombania kuliweka jiwe jeusi baada ya marejebisho ya alkaaba. Akaliweka yeye. Muhamad alikuwa mkureshi na alishiriki elimu yao na tamaduni zao na mengineyo hadi pale alipoamua kuachana na aina hiyo ya ibada baada ya kuwa mtu mzima. Na baada ya kupokea wayhi katika jabar hila alianzisha dini mpya ambayo ikaleta upinzani mkubwa kwa wahenga.

Ila kwenye eneo la hija aliendana na wahenga kasoro kufanya tawaf uchi. Kuna muda waislamu waliingia mkataba wa hija na makureshi na walisali pamoja, waislamu wakiwa wamejifunika mavazi kama sasa bila chupi ndani huku wahenga wakiwa uchi ila wote walifanya sawa sawa katika tawaf (hijja). Wahenga walihiji hivi;

1) Kuzunguka Kaaba mara saba wakiwa uchi wakiamini nguo zinawapa uchafu (unajisi),

2) Kulibusu jiwe au kulipungia mkono na kuomba dua na kumpa utukufu Hubal allah

3) Kufanya Saayi kati ya Swafaa na Marwa mara saba,

4) Kisha kunyoa au kupunguza nywele.

5) Kuchinja wanyama baada ya hija

NB. Nao walikuwa na mwezi wa ramadhani. Rejea Maisha ya Muhamad Uk wa 16 kifungu cha 4 sura ya 4. Na katika Sahihi Bukhari vol 16, hadishi no. 28 ufafanuzi wake inasema majahili (wapagani) nao walikuwa wakifunga ramadhani kabla ya uislamu. Baada ya Muhamad kuiteka Maka na kuisilimisha, ibada ya hija ikabakia pale pale kama mwanzo kasoro kufanya hijja ama umrah uchi. Walifanya;

1) Kuzunguka Kaaba mara saba wakiwa wamevaa migolole miwili (iriham) bega moja likiwa wazi na bila chupi ndani wakiamini chupi zinawapa uchafu (unajisi),

2) Kulibusu jiwe au kulipungia mkono na kumpa Allah utukufu kwa kusema Allah ni mkuu.

3) Kufanya Saayi (kukimbia) kati ya Swafaa na Marwa mara saba,

4) Kisha kunyoa au kupunguza nywele.

5) Kuchinja wanyama baada ya hija

Hivyo Muhamad hakwenda tofauti na wahenga wake zaidi aliboresha ibada tu ya awali. Muhamad aliliheshimu sana jiwe jeusi na kuacha alama kwa wafuasi wake. Tunaposoma vitabu mbalimbali vya kiislamu tunaona namna ambavyo waislamu wanavyo fanya ibada ya kuliheshimu jiwe jeusi lililo katika msikiti mkuu wa makka uitwao Al-ka’ba unaofahamika kuwa ni “bait ullah” yaani nyumba ya Allah. Baadhi ya vitabu hivyo ni hivi…

Kitabu kiitwacho mkweli mwaminifu mtungaji sheikh Said Moosa Muhamed al-kindy kitabu cha 3-4 chapa ya 14 ukurasa wa 75 kuna maneno haya;

"Kasema mtume (s.a.w.).... Basi atakaye ligusa (jiwe jeusi) basi kafungamana na mwenyezi."

Na katika kitabu cha hadithi za Muhammad cha sahih al-bukhari vol. 2 ukurasa wa 397 hadithi na 682. katika hadithi hii tunaambiwa kwamba “kila wakati mtume s.a.w alipokuja kwenye jiwe jeusi alilielekezea kikidole na kusema Takbir maana yake Allah ni mkuu.

Na kuhusu ushahidi wa kuhiji bila chupi tunapata hapa;

Shaykh al-Islam ibn Taymiyah (Mwenyezi Mungu amrehemu) alisema:
"Vivyo hivyo, chupi ni (iliyokatazwa zaidi) kuliko suruali." (Majmu'al-Fatawa, 21/206)

Al-Muzni amesema

Kwa mfano, nabii (amani na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) alikataza Hija kwenye Ihram kuvaa shati, suruali, kifuniko cha kichwa na Khufuf, na hakuizuia kwa vitu hivi tu, badala yake alikataza pia kuvaa nguo ndefu ya kufunika mwili mzima, kofia, Kufis (kilemba cheupe cha pamba), soksi na chupi, nk.” (I’lam al-Muwaqqi’in, 1/205-207)

Maonyo ya Mungu wa Biblia

1) Ni maarufuku kuweka jiwe la kuabudia ama kuliabudu. Hii ni ibada ya sanamu. Imeandikwa;

Msijitengenezee sanamu au kusimamisha kinyago cha kuchonga, au mnara, wala jiwe la kuabudia, na pia msijiwekee jiwe lililochongwa katika nchi yenu na kusujudu mbele yake. Mimi ndimi Bwana Mungu wenu.Walawi 26:1 NEN

2) Kwenda nyumbani mwa Bwana bila nguo ya ndani. Kutoka 28:42,43.

Hivyo kwa utaratibu huu tukubali kuwa Muhamad sio miongoni mwa wajumbe/manabii wa Mungu bali wa Hubali mungu wa Maka. Maana ananena kinyume cha Mungu wa manabii.

Rafiki ukitaka kuliomba jiwe au kuliabudi basi usiabudu jiwe mfu bali omba au abudu jiwe lililo hai ambalo ni Kristo Mwana wa Mungu. Biblia inasema,

[11] Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni. [12] Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. Mdo 4:11-12 SUV

Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima. 1 Pet 2:4 SUV

Mungu akubarikie sana
 
UPAGANI WA KALE KATIKA USASA

Ibada ya hija bila kuvaa chupi

Wapagani wa Maka naam makureshi walikuwa wanafanya hija wakiwa watupu (uchi wa mnyama). Na Waislamu leo wanahiji bila kuvaa nguo za ndani. Mtume wa kislamu Muhamad alizaliwa katika jamii ya makureshi na tena babu yake alikuwa kuhani mkubwa wa mungu wa Maka aliyejulikana kama Allah ama Hubal. Muhamad alipozaliwa, babu yake alimpleka mbele ya alkaaba (lililopo jiwe jeusi) na kumweka wakfu kwa Hubal/Allah na kumpa jina Muhamad kwa utukufu wa Hubal. Hubali ndio mungu Baal katika Biblia aliyetolewa kafara za watoto. Muhamad ameishi Maka kwa miaka 40 akishuhudia matendo yote hayo na akishiriki kutatua migogoro ya kikabila ya kugombania kuliweka jiwe jeusi baada ya marejebisho ya alkaaba. Akaliweka yeye. Muhamad alikuwa mkureshi na alishiriki elimu yao na tamaduni zao na mengineyo hadi pale alipoamua kuachana na aina hiyo ya ibada baada ya kuwa mtu mzima. Na baada ya kupokea wayhi katika jabar hila alianzisha dini mpya ambayo ikaleta upinzani mkubwa kwa wahenga. Ila kwenye eneo la hija aliendana na wahenga kasoro kufanya tawaf uchi. Kuna muda waislamu waliingia mkataba wa hija na makureshi na walisali pamoja, waislamu wakiwa wamejifunika mavazi kama sasa bila chupi ndani huku wahenga wakiwa uchi ila wote walifanya sawa sawa katika tawaf (hijja). Wahenga walihiji hivi;

1) Kuzunguka Kaaba mara saba wakiwa uchi wakiamini nguo zinawapa uchafu (unajisi),

2) Kulibusu jiwe au kulipungia mkono na kuomba dua na kumpa utukufu Hubal allah

3) Kufanya Saayi kati ya Swafaa na Marwa mara saba,

4) Kisha kunyoa au kupunguza nywele.

5) Kuchinja wanyama baada ya hija

NB. Nao walikuwa na mwezi wa ramadhani. Rejea Maisha ya Muhamad Uk wa 16 kifungu cha 4 sura ya 4. Na katika Sahihi Bukhari vol 16, hadishi no. 28 ufafanuzi wake inasema majahili (wapagani) nao walikuwa wakifunga ramadhani kabla ya uislamu. Baada ya Muhamad kuiteka Maka na kuisilimisha, ibada ya hija ikabakia pale pale kama mwanzo kasoro kufanya hijja ama umrah uchi. Walifanya;

1) Kuzunguka Kaaba mara saba wakiwa wamevaa migolole miwili (iriham) bega moja likiwa wazi na bila chupi ndani wakiamini chupi zinawapa uchafu (unajisi),

2) Kulibusu jiwe au kulipungia mkono na kumpa Allah utukufu kwa kusema Allah ni mkuu.

3) Kufanya Saayi (kukimbia) kati ya Swafaa na Marwa mara saba,

4) Kisha kunyoa au kupunguza nywele.

5) Kuchinja wanyama baada ya hija

Hivyo Muhamad hakwenda tofauti na wahenga wake zaidi aliboresha ibada tu ya awali. Muhamad aliliheshimu sana jiwe jeusi na kuacha alama kwa wafuasi wake. Tunaposoma vitabu mbalimbali vya kiislamu tunaona namna ambavyo waislamu wanavyo fanya ibada ya kuliheshimu jiwe jeusi lililo katika msikiti mkuu wa makka uitwao Al-ka’ba unaofahamika kuwa ni “bait ullah” yaani nyumba ya Allah. Baadhi ya vitabu hivyo ni hivi…

Kitabu kiitwacho mkweli mwaminifu mtungaji sheikh Said Moosa Muhamed al-kindy kitabu cha 3-4 chapa ya 14 ukurasa wa 75 kuna maneno haya;

"Kasema mtume (s.a.w.).... Basi atakaye ligusa (jiwe jeusi) basi kafungamana na mwenyezi."

Na katika kitabu cha hadithi za Muhammad cha sahih al-bukhari vol. 2 ukurasa wa 397 hadithi na 682. katika hadithi hii tunaambiwa kwamba “kila wakati mtume s.a.w alipokuja kwenye jiwe jeusi alilielekezea kikidole na kusema Takbir maana yake Allah ni mkuu.

Na kuhusu ushahidi wa kuhiji bila chupi tunapata hapa;

Shaykh al-Islam ibn Taymiyah (Mwenyezi Mungu amrehemu) alisema:
"Vivyo hivyo, chupi ni (iliyokatazwa zaidi) kuliko suruali." (Majmu'al-Fatawa, 21/206)

Al-Muzni amesema

Kwa mfano, nabii (amani na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) alikataza Hija kwenye Ihram kuvaa shati, suruali, kifuniko cha kichwa na Khufuf, na hakuizuia kwa vitu hivi tu, badala yake alikataza pia kuvaa nguo ndefu ya kufunika mwili mzima, kofia, Kufis (kilemba cheupe cha pamba), soksi na chupi, nk.” (I’lam al-Muwaqqi’in, 1/205-207)

Maonyo ya Mungu wa Biblia

1) Ni maarufuku kuweka jiwe la kuabudia ama kuliabudu. Hii ni ibada ya sanamu. Imeandikwa;

Msijitengenezee sanamu au kusimamisha kinyago cha kuchonga, au mnara, wala jiwe la kuabudia, na pia msijiwekee jiwe lililochongwa katika nchi yenu na kusujudu mbele yake. Mimi ndimi Bwana Mungu wenu.Walawi 26:1 NEN

2) Kwenda nyumbani mwa Bwana bila nguo ya ndani. Kutoka 28:42,43.

Hivyo kwa utaratibu huu tukubali kuwa Muhamad sio miongoni mwa wajumbe/manabii wa Mungu bali wa Hubali mungu wa Maka. Maana ananena kinyume cha Mungu wa manabii.

Rafiki ukitaka kuliomba jiwe au kuliabudi basi usiabudu jiwe mfu bali omba au abudu jiwe lililo hai ambalo ni Kristo Mwana wa Mungu. Biblia inasema,

[11] Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni. [12] Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. Mdo 4:11-12 SUV

Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima. 1 Pet 2:4 SUV

Mungu akubarikie sana
Sawa,ngoja tusome!
 
Ndio maana walikuwa na bifu na wamasai wangororo ugonvi wao mkubwa kumbe kutovaa chupi.
 
Back
Top Bottom