Uongozi wa uswahiba hauna manufaa Afrika

Peter Stephano 809

Senior Member
Feb 29, 2020
120
162
Na: Peter Mwaihola.

Mapema baada ya kuchuguliwa Rais Wa DRC Felix Tshisheked alipata Kutiliwa mashaka kua Ni serikali gani angeiunda hii kutokana na chama chake kutopata wabunge wa kutosha ili kuunda Baraza la mawaziri huku chama Cha Rais mstaafu Joseph kabila kikivuna wabunge wa kutosha hivyo kua na sifa ya kuunda serikali.

Baada ya kuundwa kwa serikali Tshishekedi akamteua Swahiba wake wa karibu kisiasa Vital Kamerhe kua Mkurugenzi wa Ofisi ya Rais watu wengi waliamini kua hii ingekua faida kubwa kiutendaji maana walikua watu wenye maono sawa.

Baada ya Siku 100 kupita serikali ya Rais Tshishekedi iliandaa mpango wa kuadhimisha siku 100 za Uongozi huo sambamba na utekelezaji wa Mambo ya kimaendeleo.

Mtendaji Mkuu wa Maadhimisho hayo akawa Bw Vital Kamerhe hivyo bajeti yote ya shughuli hiyo Dolla 57 millioni zikiwa chini yake, shughuli ilienda kwa mashaka mipango ikakwama ikasemekana amefuja fedha hizo, Kisha akakamatwa na kuwekwa kizuizini kwa amri ya mahakama Kesi yake inaanzwa kusikilizwa huu mwezi uchungzi umekamilika.

Sina hakika Kama Ni kweli Kamerhe alifuja fedha hizo ama la! Ila Aina hii ya Uongozi wa uswahiba umeiponza pakubwa Afrika hasa katika nyadhifa kubwa.

Uongozi wa uswahiba Hauwezi kuwa wa kufuata sheria na taratibu maana Watu hufanya mambo kwazoea bila hofu kwakua waloteuliwa na Ndugu ama Swahiba zao.

Kuna visa vingi vya Uongozi wa uswahiba vilivyotokea Afrika Kama Mugabe alivyomteua mkewe katika serikali, Museveni kumpa Uongozi wa juu katika jeshi mwanae wa kiume Nk.

Hapa Nchini kwetu tunaona Namna Viongozi wa Kuteuliwa waliopatikana kwa kigezo Cha uswahiba wanavyoenenda vibaya pasipo kukemewa Wala kuonywa na mamlaka zilizo juu Yao.

Viongozi waliopatikana kwa kigezo Cha uswahiba hawana jema katika Afrika zaidi ya kua Wala rushwa, mafisadi, wakaidi, walanguzi, wababe na wakiuka Sheria.

Tangu ukoloni mpaka Sasa Viongozi wa namna hii hawana matunda na hawapaswi Kupewa kipaumbele wakati wa kuunda serikali.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom