Uongozi Tanzania tiketi ya uovu

Msambichaka Mkinga

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
1,649
2,911
Hivi karibuni Rais Magufuli alitoa maelekezo ya Polisi wa Usalama Barabarani, kupandishwa cheo kutokana ni kutimiza wajibu wake wa kuhakikisha kila mtu anatii sheria, bila ya kujali kuwa aliyekuwa ametenda kosa alikuwa ni dereva wa mke wa Waziri Mahiga.

Jambo hili linaonekana ni dogo lakini ni kubwa sana maana kwa jamii ya Tanzania, ukiwa kiongozi au na cheo kikubwa cha kiutendaji, basi wewe, na wakati mwingine familia yako, wote mnakuwa tayari na haki ya kutenda makosa bila ya kuguswa na yeyote, yakiwemo makosa ya usalama barabarani.

Tanzania ni nchi ya ajabu, yenye serikali ya ajabu, yenye viongozi wa ajabu na askari wa ajabu. Kiongozi anatakiwa awe mfano wa kufuata sheria ili awe kioo cha wale anaowaongoza.

Siku hizi ukiwa unasafiri, utashuhudia askari wenye kamera za kuangalia mwendokasi wa magari ili kuwabaini madereva wanaokwenda mwendokasi wa zaidi ya inavyoruhusiwa kwenye maeneo maalum, mara nyingi maeneo ya makazi ya watu. Jambo la kushangazi, na hiyo nimeshuhudia mara mbili mimi mwenyewe, askari anakusimamisha wewe unayekwenda mwendokasi wa 55km/hr lakini ataiacha gari ya Waziri, Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Kamishna wa Wizara, mkurugenzi wa wizara inayokwenda kwa mwendokasi wa 140km/hr. Mara mbili niliwahi kusimamishwa maeneo ya Singida baada ya kwenda umbali wa karibia 10km bila ya kuona kibao cha kusitisha marufuku ya zaidi ya mwendokasi wa 50km/hr, na mara moja nilikamatwa kwa kuanza kuongeza mwendo nilipokuwa nakaribia kumaliza eneo la marufuku ya kutozidisha zaidi ya 50km/hr. Nilikamatwa nikiwa na mwendokasi wa 68km/hr na 63km/hr. Nikiwa nimesimamishwa nilishuhudia magari yenye namba STK yakipita kwa mwendokasi wa juu kabisa, kwa makadirio nadhani ilikuwa 120-140km/hr, nilimwuliza askari kwa nini hasimamishi magari yale yaliyokuwa yakienda kwa mwenokasi wa kupindukia, aliniambia ni magari ya serikali. Nilivyoendelea kubishana naye, akaniambia kuwa, je, wewe unajilinganisha na hao?

Nilishangaa sana, nikasema kweli hii ni Tanzania! Nchi ambayo ukiwa kiongozi una ruhusa ya kufanya chochote badala ya kuwa mfano.

Kwa Tanzania, magari yanaoendeshwa kwa mwendo kasi wa juu bila ya kujali ni eneo gani yanapita, ni magari ya viongozi wa serikali, magari ya jeshi na magari ya polisi wenyewe. Sheria za barabarani zimewekwa ili kulinda usalama wa abiria ndani ya chombo chako, watumiaji wa vyombo vingine vya usafiri, na usalama wa waenda kwa miguu. Ninachojiuliza, Je, ajali huangalia kuwa gari hili yumo mheshimiwa au afande? Kama wao waliomo kwenye magari hayo hawaogopi kufa au kupata ulemavu, hawaogopi kuwaua watumiaji wengine wa barabara?

Magufuli, asiishie kumpandisha cheo yule askari aliyemwadhibu dereva wa mke wa Waziri badala yake atoe maelekezo kwa askari wote nchini kuwa ule wakati wa viongozi na watunza sheria kuhodhi haki ya kuvunja sheria umekwisha. Sasa ni wakati wa viongozi na watunza sheria kuwa mfano wa kutii sheria. Kiongozi yeyote atakayevunja sheria au kuruhusu aliye karibu naye kuvunja sheria apewe adhabu kali, na ikiwezekana kumwondolea sifa ya kuendelea kuwa kiongozi. Na msimamizi wa sheria atakayethibitika kutokumchukulia sheria kiongozi au msimamizi wa sheria, afukuzwe kazi mara moja kwa kushindwa kutimiza wajibu wake.
 
Umeandika vizuri sana mkuu, hongera sana kwako.

Hii kitu imejikita mizizi sana katika kila sekta ya kimaisha, kuanzia ngazi ya familia mpaka huko kwa wakubwa.
Kifupi mindset za Kitanganyika ni "ukubwa ni ukuu".

Sasa kuvunja hio kitu sio kazi ya siku moja, hata Magufuli mwenyewe akiamua kulivalia njuga suala hili litachukua siku nyingi sana kuweza kuzaa matunda tunayoyataka.
 
hii ni Tanzania! Nchi ambayo ukiwa kiongozi una ruhusa ya kufanya chochote badala ya kuwa mfano
mkuu, hongera sana kwa kuwa hapa umejijibu mwenyewe tatizo kubwa linaloikabili nchi hii na watu wake kama si afrika nzima......the only way to survive tanzania ni kwa wewe kuwa mpole tu na mtazamaji. viongozi wetu hawataki kukosolewa na ukiwa muongeaji sana wanakupoteza ama kukuundia mauza uza yasiyokuwa na mbele wala nyuma......
 
Kuna wakati niliona mkuu wa police UK amekamatwa mara mbili kwa mwendokasi. Alilipa fine and kuondolewa point kwenye driving lecence yake. Hii inaonyeshe wenzetu wanavyojua kuzifuata sheria, lakini Tanzania ukiuliza utaambiwa hatujafika huko bado. Najiuliza line tutafika huko kama tunaendekeza ujinga wa kulindana.

Speed camera police chief caught...speeding
 
Tanzania ukiuliza utaambiwa hatujafika huko bado. Najiuliza line tutafika huko kama tunaendekeza ujinga wa kulindana.
and how many dollars does it take to get us there??? mkuu, haya mambo ya kujishusha huwa yanaanza na malezi bora ya kifamilia pamoja na taasisi zetu za kidini na tangu mtoto akiwa mdogo sana na sio kusubiri mtu aende kozi ya miezi 9 kufundishwa nidhamu, hapo atakuwa na nidhamu ya uoga tu kwa bosses wake.......
 
Magufuli, asiishie kumpandisha cheo yule askari aliyemwadhibu dereva wa mke wa Waziri badala yake atoe maelekezo kwa askari wote nchini kuwa ule wakati wa viongozi na watunza sheria kuhodhi haki ya kuvunja sheria umekwisha.
jambo la msingi sana.......
 
Siyo Tanzania tu. Nchi nyingi za kiafrika, gharama za kutokuwa na cheo/wadhifa ni kubwa sana. Ndio maana watu wanasaka ukubwa ili kuepuka gharama za kutokuwa nao. Cf: Chinua Achebe.,"The Trouble with Nigeria", Sole Soyinka., "The Man Died",,Nurredin Farah .,"The Fate of a Cockroach" au Ngugi wa Thiong'o,."The Writer's Prison Diary"..nk, nk
 
Back
Top Bottom