Uongozi ni karama kutoka kwa Mwenyezi Mungu, asiyekuwanayo asiung’ang’anie!

sulphadoxine

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,257
645

Dunia nzima viongozi wema huunda sera za kuwafanya watu wao wawe na umoja, upendo na mshikamano ili kuidumisha amani miongoni mwao, hapa kwetu ni kinyume. Kwa udhaifu walio nao, viongozi wetu wameshindwa kuwakabili maasimu wao wenyewe.
Wanakimbilia kuwachanganya wananchi kwa kutumia uelewa wao mdogo. Neno ufisadi liliposhindwa wakawaletea lingine, gamba. Mawazo ya kishetani kutoka kwa wanaomtumikia yameshindwa kuwasambaratisha Watanzania walioungana. Iweje waliotenda dhambi ya mauti, wakakisaliti chama chao na viongozi wao wa kitaifa ndiyo hao hao wapewe jukumu eti kuwaonyesha wananchi watu wengine kuwa wale ndiyo mafisadi na siyo wao waliothibitika?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom