Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,997
- 20,329
Binafsi nimejipa utaratibu kuwa vitabu vinavyohusu uafrika na waafri sitavitilia mkazo sana vile vilivyoandikwa na wazungu bali vilivyoandikwa na Waafrika wenyewe! Mfano ukisoma historia ya Mkwawa iliyoandikwa na wazungu wanasema mkwawa alijiua kwakujipiga risasi,
Ukweli wa historia ya kiafrika wazungu waliona aibu kusema walimshindwa Mkwawa, Mkwawa hakujiua bali aliwatoroka wazungu na kuelekea Songea ambapo alifia milima ya Lukumbulu kwakuliwa na Simba baada ya kuugua akiwa milimani peke yake. Nimpongeze kamanda Edwin Mwesiga huyu ni mtafiti wa mambo ya kiafrika na uafrika wetu.
Ni rahisi sana Vijana wa leo kuwadhalau wazee wanaokutana nao barabarani na kuwaona watu wasio na Elimu wakiaminishwa kuwa elimu ilianzia magharibi, Cha ajabu Ahmed Baba (1556-1627) karne ya 16 aliandika vitabu 60.Ni mingoni mwa wasomi wa Phd katika ufalme wa Mali.
Ni vizuri watu tuyasake maarifa kwakutumia maarifa, na kwakutokujua historia yetu Waafrika tumelidhika Bara letu la Afrika na yale machache tunayoyafahmu, tukidhani wazungu ndio wasomi wa mwanzo duniani kumbe wapo waliofanya mapinduzi makubwa katika Africa,ila wamefichwa na historia za kigeni zinazofundishwa mashuleni.
Ukisoma leo historia ya Tanganyika ni aibu, inaanza na Nyerere na kuishia na Nyerere jambo ambalo ni uogo mkubwa......Pamoja na kwamba 1927 Gavana Sir David Cameron kupiga marufuku mtu mweusi kukanyaga mjini (posta ya leo) hasa kwenye sherehe za wazungu ambazo zilikuwa maranyingi zinafanyikia ukumbi wao pale makao makuu ya NBC leo,
Gavana huyu aliwaundia chama cha kuratibu sherehe za weusi huko pembeni ya mji huko mtaa wa Stanley (leo Lumumba) na kuwapa ofisi mahali leo wanapojiita TANU ilizaliwa. Lakini historia ya Tanganyika haiwataji waasisi wa AA, Rais wa kwanza Mwalimu Cesil Matola (msomi wa mwanzo kabisa enzi za mjerumani kutoka kabila la Wayao), katibu mkuu wa kwanza Klest Sykes (Mzulu mateka wa vita vya kwanza vya dunia toka Afrika Kusini), Mwekahazina Ali Ramadhan (mzaramo na mvuvi maarufu wa pwani la Azania).
Hao ndio mwaka 1927 waliounda Chama cha kwanza kabisa cha kutetea maslahi ya weusi Tanganyika na shughuli zake zilikuwa ni kuratibu sherehe za waafrika tu. (Chama cha walevi kwa lugha nyingine). Mwaka 1933 Mwalimu Cesil Matola alifariki na nafasi yake ikakaimiwa na katibu mkuu wa chama hicho bwana Klest, mpaka ilipofika mwaka 1948 yakatokea mapinduzi yaliyoongozwa na mtoto wa Klest aliyeitwa Abdulwakil Sykes huyu alikuwa ametoka kupigana vita vya pili vya dunia, na aliporudi alikuwa na mawazo ya ujana toka vitani, akampindua baba yake kwa kumpiga ngumi puani. Kisha AA ikabadilishwa jina na kuitwa TAA, Rais wake wa Kwanza akawa Dr Vedasto Kyaruzi (Mhaya)huyu ndie dakitari wa binadamu wa kwanza kabisa wa kiafrika Tanganyika, Katibu mkuu akawa Abdulwakil Sykes na Mweka hazina akawa Dosa Azizi, utawala huo ulienda mpaka mwaka 1953 uchaguzi ulipofanyika na Nyerere akashinda pale kwenye ukumbi wa Anautoglo Mnazimoja leo, mwaka 1954 Nyerere akabadili jina la chama na kuwa TANU iliyokwenda mpaka mwaka 1977 na kisha kikazaliwa chama kiitwacho CCM ambacho kinalitafuna taifa leo..
Hili ndio chimbuko la AA, TAA, TANU na hii CCM.