Habari zenu wana Jamvi,
Ninakuja kwenu tena na sasa ni kama kichwa cha habari kinavyosomeka Hapo juu.
Kwa kweli kumekuwa na mtokea mbalimbali ya unyanyasaji kwa watoto,iwe wale wa majumbani na wazazi au walezi au wale watoto wasio na wazazi na makavi,watoto wa mitaani.
Jana kulikuwa na debate katika kituo kimoja cha radio,kwamba watoto wa majumbani wanakutana na unyanyaswaji wa hali ya juu kama mfano kubakwa na walezi au ndugu,kwa kutokana na ile uaminifu ambao umejengeka miongoni mwa familia as you know watoto walioko majumbani wanaonekana kuwa salama zaidi ya watoto walioko mitaani pasipo wazazi au walezi wa kuwatazama katika ukuaji wao. Hivyo watu mbalimbali wanachukulia advantage hali hiyo na kuwatendea watoto wengi unyama na aina mbalimbali za manyanyaso.
Wakati Huo wengine wanasema watoto walioko mitaani ndio ambao wana experience manyanyaso ya hali ya juu sana,kwa sababu wao wenyewe Ndio wanajiongoza katika maisha yao ya kila siku,yaani hakuna wazazi au walezi wa kuwatazama na kuwaepusha na matukio mbalimbali dhidi yao.
Mimi ninalileta hapa kwenu wana jamvi,tunaweza kujadili na kuchangia Uzi Huku kwa namna ya kipekee kabisa tukilitazama kwamba unyanyasaji unatokea katika jamii tunazoishi,katika mazingira ya kila siku na hawa watoto haijalishi wa mitaani au wa majumbani lakini kama watoto wana kutana na manyanyaso ya aina mbalimbali.
Karibuni tuchangie