Unyama : Mbaroni Kwa Kumtupa Mtoto Mchanga Chooni.

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
Ule unyama wa kiwango cha hali ya juu kwa baadhi ya wanawake umeendelea tena baada ya mtoto ambae hata utambuzi hana kutupwa chooni na mfanyakazi wa Hotel ya Landmark.
Rosemary Khiwili (23) amekamatwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumtupa mtoto mchanga kwenye choo cha shimo katika nyumba aliyekuwa akiishi Kimara jijini Dar es salaam.
Mtoto huyo aliyeokolewa na kikosi cha zimamoto, aligundulika kutupwa katika choo hicho baada ya mwenye nyumba hiyo kuingia chooni na kutaka kumwaga maji machafu na ndipo aliposikia mtoto huyo analia.
Habari zinaelezwa kuwa mtoto huyo aliyeokolewa akiwa hai amehifadhiwa katika hospital ya Mwananyamala kwa uangalizi zaidi..!

Rai yangu: enyi mama zetu na dada zetu kuna njia nyingi ya kuzuia kupata ujauzito, na si mfanyavyo,huo ni unyama kwa mtoto asiye na hatia au kwanini usipemleke kwa watu wenye ubinadamu maanake nyinyi ubinadamu haupo..badilikeni.

Nawasilisha.
 
Mwanamke ana huruma sana.ila mwanamke ana roho yakikatili sana.
 
Back
Top Bottom