Unlocking Galaxy Note II: Kuna njia mbadala?

Kwameh

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2011
Posts
1,793
Reaction score
2,162
Wakubwa,

Nina Galaxy Note II, imekuja na sim lock ya Verizon. Ku unlock kwa mafundi naambiwa dola 120. Natafuta njia mbadala kama zipo.

Hivi je, niki flash simu kwa kutumia custom ROM mpya, sim lock itatoka?

Na kama haitoki ni kwa nini haitatoka wakati nitakuwa nimebadilisha firmware nzima iliyoko kwenye simu, au tuseme hiyo lock iko wapi kama siyo kwenye software/firmware iliyokuja na simu?

Ku flash Custom ROM nishawahi fanya kwa SII Skyrocket, naweza, japo ni siku nzima au mbili kwa mimi, lakini it is worth saving $120.

Maoni tafadhali. Ahsanteni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…