Tembo2
JF-Expert Member
- Jan 1, 2014
- 492
- 811
Mkeo Anarudi Nyumbani kavimba vibaya usoni! Unamuuliza anakujibu kuwa kakutana na vibaka wamemvamia na kumpiga, lakini ukimcheki kwa makini unakuta kila kitu chake amerudi nacho na kiko salama. Unaanza kupeleleza, unagundua kapigwa na “Mchepuko” wake. Unaoneshwa mchepuko huo, nawe unakwenda moja kwa moja (straight) kwa huyo jamaa, unapomuuliza anakujibu kama ifuatavyo: ".....Bro mimi yule ni Mpenzi wangu wa muda mrefu hata kabla hujamuoa, tuna miaka mingi ni wapenzi wa siku nyingi sana. Mimi nakujua wewe kuwa huyo ni mkeo, ulimuoa wakati mimi sina uwezo kifedha, lakini hatukuwahi kugombana, tumeendelea na mapenzi Muda mrefu, na hata watoto unaodhani ni wako, Mimi mwenyewe tulipanga majira, sasa yawezekana nami yupo wangu, kwani huwa natoa matumizi ya mtoto mmoja yule Jenerose. So kuwa na amani, nakufahamu vema. "....Lakini kilicchoniuma mimi ni kwamba huyu Mwanamke mshenzi, nimegundua ananichet mimi, anatembea na njemba fulani, so iliniuma sana, nilitamani sana ufahamu hili, lakini ningeanzaje kukwambia wakati wewe hujui kama mimi mkeo ni mpenzi wangu. Mimi sina tatizo na wewe, na hata akiniambia jana mmefanya sijali, lakini kwanini atembee na mwanamume mwingine tofauti na sisi (wewe na mimi). Kwahiyo kweli nimemfumua hayo makonde, tena kajikanda hapa. "....Amebadilika sana huyu mwanamke, amekuwa na tabia chafu sana siku hizi, haiwezekani nichangie na mwanamme mwingine kwa mtu ninayempenda. Wee mwenyewe hujui tu ninavyoumia………” Swali
Kama ndo wewe, utafanyaje, utaanza na huyo jamaa au utarudi mdogo mdogo kwa mkeo? Je utamfanya nini Mkeo?
Kama ndo wewe, utafanyaje, utaanza na huyo jamaa au utarudi mdogo mdogo kwa mkeo? Je utamfanya nini Mkeo?