Unga unapatikana, ila ukienda maduka ya kisuna huwa wanauza kijiko kimoja ni shilingi 1000, cha kukushauri ni kuwa Fanya namna upate mbegu za mlonge upande(uoteshe) maana ndani ya miezi mitatu tu unaanza kuvuna, katika familia yangu kuna miti miwili ambayo kwangu ni mhimu, wa kwanza ni huu mlonge kwa ajili ya tiba ya malaria na kuondoa sumu mwilini,
Lakini pia kuna mti Fulani ambao huwa nautumia kwa ajili ya kutibu UTI, kwa sasa haya magonjwa ni tatizo kwani mtu hawezi maliza mwezi hajaugua eidha malaria au UTI, hivyo nashauri kwa raia yeyote anayependa afya yake kuwa ni miti hii ili kujiepusha na matumizi ya Mara kwa Mara ya dawa za viwandani.
Mwisho mimi niko mbali toka hapo Shinyanga, ila kama utakwama sana naweza kukuagizia mbegu za mlonge uoteshe, nitakuagizia kupitia magari ya Mwanza lakini pia nikutakie pole kwa shida unayoipata juu ya afya yako na nikutakie pia uponaji wa haraka.