Unene huu wa waheshimiwa wetu unasababishwa na nini?

kula mlo bila mpangilio mzuri kwa afya,kuto fanya mazoezi yoyote,elimu ndogo ya afya kwa ujumla ndio inachangia haya yote.


wao wanaona sifa kunenepeana hovyo bila kujua madhara yake.
 
wanajamvi aliyelala usimwamshe,mfuko wa kuhudumia majimbo tayari sasa mwataka waanzishe pia mfuko wa kuhudumia matumbo yao sa na sa au uk? waachen wapunguzwe na mastrok pengine watabaki wanaofanana nasi
 
misosi hiyo, inatandikwa misupu,mishikaki,mibia,mikachumbari,chachandu,ugali nakadhalika nakadhalika vyote vinasukumizwa kwenye tumbo iloilo moja...sijui wanalaleje? itakuwa kukorome kwenda mbele.
 
tusiwaseme wabinge peke yao .................hivi watanzania wangapi wanajijua kama wako overweight au obese?

watanzania wangapi wanakula mboga mboga na matunda ya kutosha kila siku?

wangapi hawali chakula zaidi ya saa tatu ya usiku?

wangapi wanafanya mazoezi japo ya kutembea kwa mguu kwa dakika 20 kwa siku?
 
Hivi lile jengo lote, na ukubwa wake, na ujenzi wa kiasia hawakufikiria hata kuweka dojo (gym)?

Spika itabidi awafokee wabunge wake waondoe hayo matumbo, kwani ni mfano mbaya kwa wananchi.

Hawezi...Koz nae analo.....labda sema waziri mkuu mstaafu Joseph Sinde Warioba ndo anaweza kuwapiga biti.....Koz jamaa yeye safiiiiii.....na am sure bado anakamua fegi ....
 
Ni kodi zetu na misaada inayotelewa kwa ajili ya maendeleo ya majimbo na Taifa letu kwa ujumla.
 

I am convinced,
 
Wanachama wa chama cha mafisadi wamewapumzisha wote wawili, Mwichumu na Mwenegoha; kwani wote wawili waliangukia pua kwenye kura za maoni!!
 
Wanachama wa chama cha mafisadi wamewapumzisha wote wawili, Mwichumu na Mwenegoha; kwani wote wawili waliangukia pua kwenye kura za maoni!!

...Subiri sasa uone watakavyoanza kupungua fasta!!:becky:
 
Jamani hawa watu wanakulaga nini? Huyu Leonidas Gama anaweza fanya hata push ups mbili kweli


Huyu Gama alikuwa mwalimu wangu pale Mfaranyaki Primary School Songea ,alikuwa mwalimu wa UPE na alikuwa ni kijana mwembamba maridadi sana ,alikuwa pia mwalimu wa ngonjera (za kusifia CCM),baada ya kumaliza hapo sikumuona tena hadi alipoukwaa ukuu wa wilaya ya Kyela kwa kweli sikuamini macho yangu nilipoona kanenepeana kupita kipimo ,nikajiuliza au ndio raha ya uheshimiwa,Gama alikuwa ni mwembamba sana na huo unene nafikiri ni wa kula hovyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…