Vien
JF-Expert Member
- Mar 6, 2020
- 7,286
- 11,784
Kila mmoja wetu amepewa talanta na kipawa cha kipekee. Lakini wengi wanapoteza muda wao wakijaribu kufanya mambo ambayo hawana uwezo nayo. Matokeo? Maisha yao yote yanakua ya wastani tu, na hata wakiondoka katika uso wa dunia hawata acha historia wala alama yoyote katika huu ulimwengu
Angalia watu waliofanikiwa kweli. Wachezaji kama Cristiano Ronaldo au Lionel Messi walitambua kuwa mpira wa miguu ndio field yao. Walijituma kila siku, wakiboresha kila kitu walichokuwa nacho, na leo hii wako kwenye kiwango cha juu duniani.
Katika muziki hususani hapa africa,Wasanii kama Burna Boy na Davido na wengineo wengi waligundua vipawa vyao vya kipekee vya kuimba na kuandika nyimbo zinazogusa mioyo ya watu. Hawa hawakujaribu kuwa wanasiasa au madaktari; walijua nini kinawapa maisha yenye maana, na walifanya kazi hiyo kwa bidii kubwa leo hii ni watu wenye hadhi ya juu
Kama biashara, fikiria Elon Musk, Aliko Dangote au Oprah Winfrey. Walitambua uwezo wao, wakapambania ndoto zao katika field ambazo zilikuwa sahihi kwao. Matokeo? Dunia inakumbuka juhudi zao, na wameshika nafasi ambazo wengi hawawezi kufikia.
Kinyume chake, kuna watu wengi wanaokosa kujua wapi wana uwezo mkubwa mwishowe wanaingia katika mambo ambayo hawana uwezo nayo, wanaingia kwenye kazi ambazo hawajazaliwa kuja kuzifanya, au kujaribu biashara ambazo hazina uhusiano na talanta zao. Hii inapelekea maisha yao yote kuwa ya wastani tu, bila na alama kubwa hapa duniani.
Tunaona mfano hapa Tanzania: kuna watu wanaopenda sana soko la mitindo, lakini hawana ubunifu au mitindo yakipekee, wanacopy tu yale yanayofanyiwa wengine. Matokeo yake hawana impact kubwa, wanabaki tu watu wa kawaida.
Lakini wengine, kama Diamond Platnumz, walitambua talanta yao, wakawekeza katika muziki na ujasiriamali wao, na leo hii wana historia inayoonekana.
Hii ni sababu kwanini ni muhimu kujua field yako na kudumisha kipawa chako. Sio tu kwaajili yako, bali pia kwa vizazi vyako. Hii ndiyo njia ya kuhakikisha tunaunda maisha yenye maana, tunabaki na legacy, na hatutakuwa tu “watu wa wastani” duniani.
Tambua field yako, jitume kwenye kipawa chako, usiruhusu shinikizo la jamii au mabadiliko yasiyo sahihi kuvuruga ndoto zako. Ukiweka juhudi zako kwenye eneo sahihi, maisha yako hayatakuwa ya wastani tu, bali utaacha historia halisi.