Unapompenda asiyekupenda ni Utumwa wa mapenzi

youngsharo

JF-Expert Member
Jan 8, 2015
2,491
500
Wanajukwaa,

Niliombwa ushauri na ndugu yangu mmoja humu ndani, ila naomba ushauri huu niuweke public najua utasaidia na wengine,

mapenzi yaweza kuwa
bora kwa kila aliye katika
mahusiano, huwa ni vyema
kila mmoja kuiona thamani
ya mwenzake. Ukipenda
kujiangalia mwenyewe si ajabu mwenzako kupata
hisia za kuwa humthamini
wala humjali.
Muunganiko wenu katika
mapenzi maana yake tayari
mmekuwa kitu kimoja. Katika mimi unaweka sisi. Ila pia ni vyema
ikakumbukwa ladha na
maana halisi ya mapenzi ipo
kwa anayekupenda na
kukuthamini. Unapokuwa na
uhakika kama anakupenda na kukuthamini hapo ndipo nafsi
yako itatulia na kuwa na
amani. Ndani ya mapenzi na
mtu wa aina hii ni amani na
utulivu kwa kwenda mbele.
Hakuna majuto wala majonzi ya kila siku.
Unapoamua kuwa katika
mahusiano na mtu ambaye
hakupendi, bali unakuwa
naye kwa kuwa tu
unampenda jua umejiingiza katika utumwa. Mapenzi ni
suala la kihisia zaidi.
Mwenzako anapokosa hisia
na wewe maana yake hata
uwepo wako hauthamini
inavyopaswa. Na hapo ndiyo tunaona yale mahusiano ya
kingono yanapozaliwa na si
ya kimapenzi kwa maana
halisi.
Yaani mwenzako
anapokuwa na mihemko ya kingono ndipo anapokutafuta
na si vinginevyo.

Niliwahi
kuongea na msichana mmoja
aliyewahi kuniambia
anampenda kijana mmoja
ambaye anauhakika kabisa yeye hampendi. Alinambia
uhakika huo kaupata
kutokana na kijana huyo
kumtakia kuna msichana
yupo anampenda na kumjali
ila si yeye. Kuonesha zaidi kumpenda
msichana yule mwingine,
jamaa aliwahi kumwambia
kama ikitokea hata huyu
msichana akagombana na
yule mpenzi mwingine wa yule jamaa, kijana yule
alikuwa radhi kumdhuru huyu
msichana.
Hata kwa matazamo wa
haraka hapo unaweza
kugundua ni kwa namna gani huyu msichana alikuwa
haitajiki. Ila cha kushangaza
msichana huyu(aliyeongea na
mimi) alimwambia mvulana
husika yuko radhi kuwa naye
hivyo hivyo. Aliamua kuwa hivyo
akiamini ipo siku jamaa
atamuelewa. Kweli
walikuwa pamoja. Ila unajua
kinachomkuta sasa?
Kila jamaa anapogombana na yule msichana mwingine
anamtumia huyu kingono na
mambo mengine yasiyo ya
kimapenzi, na bila kutafakari
mara mbili huyu msichana
anafanya kwa kile anachoamini hali hiyo
itamfanya huyu jamaa
amfikirie zaidi. Kuna kitu cha
kuangalia hapa.
Suala la mapenzi si suala la
kuoneana huruma wala aibu. Mapenzi ni hisia. Unapojitoa
kwa mwenzako kwa kila
jambo na unamuona haelekei
ujue hana hisia na wewe.
Kwanini unakubali kuteseka
na kuumia kila siku kwa kumuangalia yeye tu?
Ndiyo, unampenda sana,
unamjali sana na unamuhitaji
sana, ila kama yeye hakutaki
wa kazi gani? Ni muda wa
kujiangalia na wewe sasa. Ona thamani yako kama
binaadamu, jionee huruma
jinsi unavyoteseka kila siku
kwa mtu asiyeona thamani
yako.
Wewe ni binaadamu mwenye hadhi na thamani,
bila kujali muonekano wala
rangi yako. Unahitaji
mwenye kukuthamini na
kukujali na si anayekufanya
kama mdoli wake ngono au kadi yake ya pesa. Kataa
utumwa wa mapenzi kwa
kuiona thamani yako.
Ni vyema ukalia kwa
kumkosa kuliko kuonekana
unaye wakati moyoni siyo wako. Hakuna sifa ya kuwa
na mtu mwenye fedha au
muonekano mzuri ikiwa
hakujali wala haupo moyoni
mwake. Mapenzi ni amani na
raha. Mapenzi hufanya watu
wafurahi na kusahau shida
zao. Ila jiulize kwanini
kwako hayako hivi? Unaenda
kwa mwenzako badala
afurahie uwepo wako, yeye anaona unajipendekeza.
Unampigia simu na kumpa
maneno mazuri ya faraja,
yeye anaona unamsumbua.
Sasa wa kazi gani?

Ni hayo tu ndugu yangu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom