Unaona nini maishani mwako?

Unaona nini maishani mwako?

Showio

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2019
Posts
254
Reaction score
482
WEWE UNAONA NINI?Kila siku unapoamka asubuhi utakutana na “Negative Forces” (Nguvu Hasi) ambazo ni lazima ujifunze kukabiliana nazo ili usipoteze furaha yako. Mtu mmoja aliwahi kusema “Train Your Mind to see the good in EVERYTHING. Positivity is a CHOICE.The HAPPINESS of your Life DEPENDS in the QUALITY of your THOUGHTS”(Ifundishe AKILI yako kuona JAMBO ZURI katika KILA KITU.Kuwa na FIKRA CHANYA ni UCHAGUZI wako. Furaha katika maisha yako INATEGEMEA UBORA WA MAWAZO YAKO).

Kumbuka kuna TAARIFA utakutana nayo leo na usipokuwa makini itaifanya siku yako nzima iwe ya HUZUNI na ya KUKATISHA TAMAA. Kuna Mtu atakuambia NENO ambalo kama haujafanya maamuzi ya kuwa mtu wa furaha inaweza kukupotezea TUMAINI LAKO kabisa na ukaachana na ndoto yako, kuna jambo linaweza kutokea leo na likaleta DALILI zote kwamba umeshafika MWISHO.

Kumbuka: Kuona JEMA katika BAYA ni UAMUZI. Kumbuka kuna wakati ulishawahi kupitia HALI NGUMU na UKAPITA SALAMA. Pia katika kila CHANGAMOTO inayotokea Leo unaweza KUPITA kwa USHINDI pia.

Badala ya KUJISEMEA MANENO ya kushindwa ndani yako-“Nimeisha”, “Sina cha Kufanya”, “Mambo Magumu”, “Haitawezekana Tena” n.k Jisemee Maneno ya Ushindi UNAPOANZA SIKU YAKO.

LEO,CHAGUA KUONA JEMA KATIKA KILA BAYA!
 
Inspirational.. Huwa napenda kuona post Kama hizi zinazowapa watu tumaini kwenye Maisha. Tunategemeana Sana aisee na tukitaka Dunia iwe better place for everyone tunahitaji kuwa na mtindo wa kupeana Moyo na kufarijiana Kivyovyote inavyowezekana.

Changamoto za Maisha kila mtu zinamgusa kwa aina yake, shida Ni Kwamba huwa tuna ubinafsi wa kutaka kupambana kila mtu kivyake na kusahau we are only humans no less no equal, na hapo ndo frustration zinapoanza unapodhani wenzio wanawin we una lose kumbe we all struggle, but tukiishi kwa kuchukuliana, itakuwa win- win both sides.. "Happiness of life depends on the quality of thoughts".
 
inspirational talks, ulaya zinalipiwa hizi! lakini mdau katiririka bure kabisa!

tusifeli watz wenzangu jumbe inaeleweka!
 
Big up Brother! Optimistic statements like these, might advance the country to the middle economy country by 2025. Looking to hearing from you once a gain. Enjoy your Easter.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
inspirational talks, ulaya zinalipiwa hizi! lakini mdau katiririka bure kabisa!

tusifeli watz wenzangu jumbe inaeleweka!
Barikiwa sana! Happy Easter
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom