umeshusha nondo za kufa mtu kuliko uwezo wangu wa kuzichakata mkuu.
hebu nipe kwa ufupi hitimisho japo nimepitia.
Adui wa mwafrika ni mwafika mwenyewe.
Hakuna mkoloni mzungu au mnyonyaji bila waafrika wenyewe kutengana
Jambo la Msingi ni kuimarisha umoja na mshikamano wetu.
Kazi ya kujenga umoja wetu kwa asilimia kubwa ipo mikononi mwa serikali.
Serikali ikiamua kulisambaratisha taifa ni dakika moja. Serikali ikiamua kuwagawanya watu ili iwe rahisi kwao kutawala ni dakika moja. Ni kugawa hela tu na vyeo kwa yule aliye tayari kuwakomoa wenzake.
Hakuna mkoloni anayeingia mahali bila watawala kufanya makosa ya kuwagawa wananchi.
Kuwa na Taifa Imara ni lazima kwanza tuwapende waafrika wenzetu tunaoishi nao. Huwezi kuwapenda waafrika wa nchi jirani kama unawachukia waafrika walioko ndani ya nchi yako.
Naamini katika mshikamano na umoja wenye kumjali kila mtu.
Sio kila anayepinga au kukosoa basi anastahili kipigwa mabomu na marungu na kuumizwa tu hata bila kutafakari yale anayokosoa kama yana msingi.
Wakati mwingine wale wanaokosoa au kupinga ingekua vizuri wakaitwa wakakaa meza moja na watawala na kujadili kwa kina hata wiki nzima kujadilo tu mstakabali mwema wa nchi kwa pamoja bila kupigana marungu na kuwekana ndani wakati mtawala amepewa tu mamlaka ya kuongoza watu waishi maisha bora yenye furaha na amani moyoni.
Kukaa meza moja na ndugu zako mliohitilafiana sio unyonge wala kupoteza heshima au mamlaka na sio woga Bali ni kujenga umoja na mshikamano.
Tunaweza kabisa kujenga taifa bora lenye kupingana kwa hoja na kukubaliana kutokukubaliana.
Kwa nini waliopewa nguvu ya kidola wasiwe wepesi kuunganisha watu ambazo ni ndugu moja kwa upendo bila kutoa mwanya kwa wa wengine kukimbilia kwa Wazungu ili kuhitaji msaada na kuonewa huruma.
Hivi unafikiri mtu ambaye amepoteza ndugu,wazazi na marafiki wakati huo huo anatafutwa awekwe gerezani tena kwa kipigo kikali kama cha Bob Wine kwa sababu ya kukosa haki ya kulindwa na kuwa huru unategemea ataona umuhimu gani wa amani wakati amani inakuwa kama ina wenyewe. Mtu huyo ni rahisi kuungana na maadui kutoka popote.
Kuna Mtu kwa ujinga tu anamwona Mchina aliyevaa vazi tu la chama chake kuwa ni bora kuliko Mtanzania na mwafrika mwenzake ambaye huenda hata wajukuu zake wataoana na kuwa familia moja!
Turejeshe upendo wetu kama watanzania na waafrika ili tujenge uzalendo kwa nchi zetu.
Hakuna cha Muzungu wala Muchina atakayekuja kupora utaifa wetu na kutujengea uhasama.
Sent using
Jamii Forums mobile app