Unamshauri nini mkuu wako wa mkoa? Mimi naanza na Makonda

Kambaresharubu

JF-Expert Member
Jan 5, 2014
335
449
Kwanza nakupongeza kwa utendaji kazi wako na hongera kwa kuteuliwa kwako kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.

Ombi langu kwako kama mkuu mpya wa mkoa wa Dsm ni kukuomba kuliangalia upya suala la route ya kinyonyaji ya magari ya kusafirisha abiria ya UDA, ile routi ya mabasi yanayoanzia mnazi mmoja - Ferry(Kivukoni) kwa shilingi 400.

Huu ni unyonyaji wa dhahiri kwa wavuja jasho wa hali ya chini.
tunaomba utusaidie ktk kuliangalia hili ili ututue mzigo.
 
Kwanza hongera na pole Mh Makonda.. Jukumu ulilonalo ni zito sana Dar es salaam ina changamoto lukuki.


Ushauri wangu kwako :

Elimu

Umeweza kujenga shule za kata mpya kwa ubunifu wako. Shule ziongezwe ila na quality ya elimu umejipangaje kuiongeza kwenye shule zetu za kata? Hii ni changamoto kubwa sana nafikiri hii ukae na walimu wenyewe watakupa mawazo mazuri zaidi sio awa wanaharakati so ili mimi ukiniuliza nitakwambia elimu ni motivation kwa mwalimu na mwanafunzi.

Ajira

Changamoto ya ajira ni ngumu kuikabili ila unaweza kuanza na vijana walio jiajiri. Kuwe na dawati maalum au chombo kwa ajili ya kuwaunganisha wajasiriamali na masoko. Kuna vijana wengi waliamua kujiajiri ila wakakata tamaa sababu ya kukosa masoko ya bidhaa zao na pengine ni kukosa connection.. Mfano leo hii ukienda Dubai spices, matunda na asali ni lulu zinaitajika sana lakini nani anajua atafikishaje huko hizi bidhaa kuna vijana wanauza viungo vya pilau pale jamhuri Street vinawaozea.. Kuna watu wanatoa asali mkoani wanakaa nazo ndani mpaka wanakata tamaa. Kuna soko kubwa la kandambili na vyombo huko Msumbiji nani anajua na ata akijua ataanzia wapi? Ni pakuanzia hapo . So napendekeza kuwe na kitengo au dawati maalum la kushughulikia connection za wajasiriamali na masoko hii itapunguza tatizo la ajira.

Usafi wa Mazingira

Kwanza ningependa tuwatambue waokota makopo mtaani kama mashujaa wa mazingira maana bila wao kuwepo sijui hii Dar es salaam ingekuwa katika hali gani.

Pili, ishu ya usafi wa mji inaanza na wapi uchafu unaozalishwa utapelekwa. Tunaweza kuwalaumu wakazi wa dsm kwa kutupa uchafu hovyo ila tujiulize kuna vifaa vya kukusanyia uchafu mitaani kama garbage cans? Nafikiri ili kupunguza tatizo la uchafu kuwe na vifaa vya kukusanyia uchafu kila baada ya mita 100 na vifaa viwe vya plastic ili kuepusha kugeuzwa screpa. Pia tender za ukusanyaji uchafu zitolewe kwa wenye vifaa vya kueleweka sio haya magari yanayomwaga uchafu njia nzima.

Ujambazi na wizi

Ili la ujambazi ni zito kidogo ila la wizi wa kawaida unaweza kulishughulikia kwa kuwabana wanunuzi wa vifaa vya wizi mfano tatizo sugu la wizi wa power windows kila mtu hapa mjini anajua power windows za wizi zinauzwa wapi.

Karibuni kwa ushauri you never know unaweza kusomwa na kutumika.. Badala ya kukaa chini na kungoja kulaumu, tuwe watu wakutafuta majawabu itatusaidia sana.
 
Ushauri huu ni mzuri endapo tu hatokuwa na uongozi wa mzuka.
 
vijana tunategemea makubwa kutoka kwako mana unazijua changamoto zetu kama kijana mwenzetu..ukifaeli itakua umetufelisha vijana wa kitanzania katika suala zima la uongozi.
 
jiwe angavu ni juu yetu kumtumia makonda tuache siasa watu wanalalamika sana ila wanasahau manunguniko hayajawai kuwa suluhisho kwenye maisha yako binafsi. Kama tumepata kiongozi mwenye positivity ndani yake tumtumie akifeli ndio tulaumu.. Hakuna kiongozi atayekuletea mtaji nyumbani wala trekta ukalime.
 
Afanye Mchakato Mvua zinyeshe Dar Maana jua kimezidi sana
 
jiwe angavu ni juu yetu kumtumia makonda tuache siasa watu wanalalamika sana ila wanasahau manunguniko hayajawai kuwa suluhisho kwenye maisha yako binafsi. Kama tumepata kiongozi mwenye positivity ndani yake tumtumie akifeli ndio tulaumu.. Hakuna kiongozi atayekuletea mtaji nyumbani wala trekta ukalime.
ni kweli kabisa, suala kubwa ni kwajinsi gani atatutete na kutusimamia vijana katika utekelezaji wa sera ya vijana ili wengi waweze kujiinua kiuchumi.
 
Mifuko ya plastiki ni chanzo kikubwa cha uharibifu wa mazingira, ipigwe stop. Hili linaonekana ni jipu lililoiva kwa NEMC.
 
Akae chini na wabunge na madiwani wa upinzani wajenge Dar pamoja.Hakuna sababu ya kunyang'anyana fito.
 
Back
Top Bottom