Unakumbuka mapigano ya milima Meru?

Khlala

Senior Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
170
Reaction score
123
Mnavikumbuka vita vilivyopiganwa mwanzoni mwa miaka ya tisini?
Nan mwenye dukuduku lolote kuhusu chanzo cha mapigano hayo?
Binafsi nlikua mdogo sana ila ninakumbuka watu walikua wabakimbia nyumbani na wanawake walikua wanapiga yowe. Walikua wanaulizana upo upande gani kati ya kaskazini na meru.
MAJIRANI WALIKUA HAWAAMINIANI TENA NA UKIMCHOKOZA ANAKUCHOMEA NYUMBA.
NAOMBA KUJUA PIA SERIKAL ILIKUA WAPI HADI MAPIGANO YAKATOKEA NA KUSABABISHA MAAFA MAKUBWA KWA JAMII YA WAMERU
 
Ugomvi mkubwa ulikuwa kwenye kudai dayosis ya mlima meru, ambayo ilikuwa itengwe kutoka dayosis ya kaskazini. Ilikuwa ugomvi mkubwa sana, watu waliuana ndugu kwa ndugu, walichomewa nyumba na kuua ng'ombe. Watu wengi hawakuweza kurecover kiuchumi baada ya hiyo fiasco.

Baadae ilikuja kutolewa dayosis ya meru. Wale wa mlima meru walishajitenga jumla na kuanzisha makanisa yao. Viongozi wote walipofulia automatically mgogoro ukafa.
 
Serikali ilikaa kimya kwa muda, kwa madai kuwa haina dini. Lakini baadae alienda mrema lyatonga kama sikosei, akawasikiliza pande zote na kuamuru waliotaka dayosis ya mlima meru wakasajili kama dhehebu na kujitenga. Habari ya mapigano ikaishia hapo.
 
Kumbe ndo maana meru kuna makanisa mengi na kila mtu anadai ameokoka
 
King'asti ulichosema ni sahihi kabisa bila kukosea! Waliojitenga walianzisha makanisa mapya mojawapo likiwa AMEC = AFRICA MISSION EVANGELICAL CHURCH, ambalo nadhani liko Meru tu! Wameru wakare!
 
Last edited by a moderator:
Hiyo vita ilinikuta katika eneo hilo na nakumbuka mgogoro ulianzia siku ile Askofu Kweka alialikwa kuja Usa River kuweka jiwe la msingi, nilikuwepo siku hiyo katika eneo la tukio, lakini kulikuwa na minong'ono ya chini kwa chini watu wakipinga ujio wake. baada ya kuweka hilo jiwe la msingi msafara ukaondika kwenda katika kumbi wa sherehe kwa ajili ya maakuli.

huku nyuma wahafidhina wakaling'oa lile jiwe la msingi na kulifunga kwenye bahasha na kulipeleka nyumbani kwake na kumkabidhi mkewe kuwa ni mzigo wa mzee. Askofu Kweka aliporudi nyumbani kwake jioni ndio akakutana na hilo jiwe la msingi alilotoka kuliweka. ikabidi mkakati wa ulinzi madhubuti ufanywe na jiwe la msingi likawekwa chini ya FFU na ulinzi ukaimarishwa hadi likakauka.

Kimbembe ndio kikaanzia hapo na watu kuanza kuchomana mishale na kukatana kwa mapanga. Nakumbuka alikuja Waziri mkuu mzee Malecela baada ya kutumwa na Raisi wa wakati huo Ali Hassan Mwinyi. Wakati akiwa mkoani Arusha akijaribu kutatua mgogoro huo, ndipo ilipotokea ile ajali mbaya iliyohusisha Familia ya mzee mmoja tajiri niliyemfahamu kwa jina moja la RIMOY ambapo familia yake ya watoto watano kama sikosei na mkewe walipoteza maisha katika eneo la njia panda ya MOMELA ikihusisha basi na gari dogo la huyo mzee. Ni bahati tu, ni yule mzee pekee aliyenusurika katika ajali hiyo na alilazwa katika hospitali ya KCMC. Ni wakati huo akijaribu kususluhisha mgogoro huo Mzee Malecela alikwenda kumjulia hali huyo mzee na kumpa pole kwa kupoteza familia yake katika ajali hiyo.

Alikuwa ni waziri wa Mambo ya Ndani pekee aliyeweza kutatua ule mgogoro. Chanzo cha mgogoro huo ni kuonekana kwamba makao makuu ya dayosisi yaliyokuwa mkoani Kilimanjaro yamejaa wachaga na misaada mingi inaelekezwa kwenye makanisa ya mkoani Kilimanjaro na yale ya Meru yakiwa yametelekezwa. Walikuwa na malalamiko mengi sana wakati huo na walikuwa wanapinga uongozi wa Askofu Kweka waziwazi....


Nawasilisha.............
 
nimekupata mzee ila japokua ililenga dini lakini nahisi pia watu waliokua na uhasama walitumia fursa hiyo kuwaangamiza maadui zao.
 
Yaah, migogoro ya aina hii sio mizuri maana watu wanatumia nafasi hiyo kulipa kisasi ki urahisi kwani watu wanafahamiana vizuri hata mapito yao.
nimekupata mzee ila japokua ililenga dini lakini nahisi pia watu waliokua na uhasama walitumia fursa hiyo kuwaangamiza maadui zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…