Unakumbuka jambo gani shule ya Msingi

bnhai

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2009
Posts
2,848
Reaction score
2,404
Shule ya msingi ni mengi yalijitokeza na huenda yamepotea na ambayo yapo bila shaka hayajabadilika au yapo kisasa zaidi.
Kumbukumbu yangu shule ya msingi ni pale ambapo wakaguzi wanakuja kututembelea. Siku hizo, tulikuwa tunahimizwa usafi lakini pia darasa la siku ya ukaguzi linafundishwa siku moja kabla.
Ninakumbuka mwalimu alituagiza vizibo vya chupa ya soda-visoda au ndude. Bahati mbaya mtoto mmoja akaibiwa vyake. Alilia mpaka yule mkaguzi akafahamu story nzima, kule ofisini hatujui kilichoendelea.
 
Basi Bwana nakumbuka tukiwa darasa
la pili,kuna mwanafunzi aliibiwa
kichongeo cha kalamu.Kipindi hicho
vilikuwa adimu wengi wetu
tulikuwa tunachonga kalamu
zetu kwa kutumia viwembe.

Aliyeibiwa alitoa taarifa kwa mwalimu
wa darasa na msako wa mwizi ulianza.
watu wote tukapekuliwa bila kikipata kichongeo.
Binti mmoja akamshtukia kijana mmoja aliyeitwa Levis
kuwa mbona yuko kimya muda mrefu na si kawaida yake?
Mwalimu akamsemesha Levis,Levis anakodoa macho tu.

Kumbe aliiba kile kichongeo akaweka mdomoni.
Mwalimu akamlazimisha aachame,
mara alipoachama,kile kichongeo kikadondoka chini.
kwa mshangao na kicheko yule mwalimu
hakumuadhibu,alimwambia asirudie tena
kwani adhabu aliyoipata ya kukaa kimya
na aibu aliyoipata vilimtosha.Maana kila mtu alicheka kwa sauti.
 
Reactions: iw8
Nakumbuka kuona nyuzi za Facebook JF.
 
Kuweka vioo chini ya madawati ya warembo wa darasa na kucheki movie LA nandy chupi
 
Mimi na genge langu tulificha kengele aisee ilikuja kupatikana siku ya Jumatano tangu ilipoonekana mara ya mwisho Ijumaa. Tulibaki kuwa watu wasiojulikana japo kuna wengine walikuwa wanajua mchongo wote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado ndoto nyiingii zinanijia kuwa nasoma shule ya msingi mugabe pale japo miaka 20 imepita tangu nimalize pale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…