Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,221
- 2,425
Nazani umeshawahi kusikia neno Roboti kwenye maisha yako sio ndiyo !!!!
Okay sasa neno "Robot" kwa mara ya kwanza ilianza kuonekana kwenye tamthiliya ya kubuni ya kisayansi ya 1920 RUR (Rossum's Universal Robots_) na mwandishi anaitwa Karel Capek.
Neno ili liliundwa na kaka Karel ambaye anaitwa Josep Capek katika nchi ya Czech neno Robot inamaanisha "uchovu" au kazi ya kulazimishwa. Mara nyingi ikielezea kazi ya wakulima chini ya mifumo ya ukabila yani Force labour.
Imepita zaidi ya miaka 105 ambapo neno roboti rasmi ni kitu kilichotengenezwa kwa ajili ya kufanya kazi kwa ajili ya binadamu haswa watumwa-hivyo ndivyo neno lilivyobadilika na kuwa maana yake ya kisasa.