Unahonga pakubwa, unakula padogo. Kasongo una nini wewe?

Unahonga pakubwa, unakula padogo. Kasongo una nini wewe?

gonamwitu

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2018
Posts
2,210
Reaction score
2,837
Mimi nawashangaa sana wanaume wenzangu ambao wanapata hela kwa tabu unabeba zege,unachimba msingi,unabeba tofali,unakuwa saidia fundi halafu ukipata hela unajinyima hata kula mlo mmoja ili ukamuhonge mwanamke huu ni ujinga na uzwazwa.

Kama unaipata hela yako kwa tabu hakikisha unapooza machungu kwa kuitumia hela yako wewe mwenyewe na siyo kuwanufaisha wengine.

Mwanaume unatakiwa uwe na P.H.D ya ubahili yaani kuhonga hata elfu 2 inabidi ukae kikao cha ukoo na ukoo wote ukubali ndio uitoe hiyo elfu 2 na sio kutoa kirahisi rahisi. Ukitoa hela kirahisi we ni bwege tu ndio nimekutukana wewe ni bwege tu kama umemaindi nipige.

eti bebi niletee chips mayai,kuku na take away nyooo nikuletee ukiwa hivo hivo na nguo zako? Wakati huo baharia umeshindia mihogo na maji.

Unapata laki unahonga elfu 80? Unakula padogo, unahonga pakubwa? Kasongo una nini wewe masikini wa akili wewe?
 
Kwa wale wanaopata kwa taabu waache ila walizo nazo watoe
 
Back
Top Bottom