Samedi Amba
JF-Expert Member
- Nov 13, 2018
- 227
- 178
Habari za mchana wapendwa,
Laptop ni mojawapo ya vifaa ambavyo vinarahisisha kazi zetu za kila siku. Na sio kila mtu anaweza kuafford laptop mpya. jambo hii hulazimisha baadhi ya wadau kutafuta laptop ambayo imeshatumika, na hili sio kosa. Sasa, nisikuchoshe, niende moja kwa moja kwa kile unachopasa kukuzingatia.
Jambo la kwanza: Unanunua laptop wapi?
Unaweza ukanunua laptop popote pale. Mtandao umerahisisha sana kazi, na ukienda kwenye websites kama kupatana, zoom tanzania na OLX, utakuta vimeorodheshwa pale, na ni hela yako tu inahitajika. .
Mojawapo ya sababu zilizonifanya niandike hili ni baada ya kuona tangazo kama hilo nililoliweka hapo chini:
Na nikakumbuka uzoefu wangu katika zungukazunguka za hapa mjini. Swali ni: Je, unawezaje kuepuka matapeli wa mtandaoni? je, unawezaje kuhakikisha kuwa kile unachouziwa ni kizuri?
Fanya utafiti wa kutosha
Hii ni pamoja na kuhakikisha kuwa una data za kutosha za yule anaye kuuzia laptop. Angalia listings zake na ikiwezekanajaribu kumtafuta mtandaoni e.g kwenye twitter, FB, insta nk. Jua kuwa ni mtu wa aina gani. Ukiona roho inakataa, acha.
Usisahau kumuuliza maswali ya kutosha: yeye ni nani, anapatikana wapi, mnaweza kukutana wapi, kifaa hicho amekuwa nacho mda gani, specs zake zikoje. Ukisikia "Subiri kwanza ntakupigia baadaye", au "(kigugumizi) eee... ni core i3, hapana core i5, hapana subiri niulize" fanya maamuzi sahihi...
Bei halisi ya kifaa
Ni muhimu kujua kile unachokinunua, , na kama kile alichokiposti muuzaji kinaoana na makadirio yaliyopo sokoni. angalia bei katika masoko mbali mbali ya vitu used ndani na nje ya nchi. utagundua kuwa bei haziachani sana. kwa mfano, bei ya mac used huanzia laki nane hadi milioni na nusu. sasa jamaa akiwa anauza mac corei5 mpya kwa laki 3, jiulize mara mbili mbili
Siku ya kuchukua kifaa
Umehakikisha kuwa bei ya kifaa ni sahihi kwa mujibu wa soko, umemuuliza muuzaji maswali ya kutosha mpaka akadhani wewe ni polisi mpelelezi. sasa imefika siku ya kuchukua kifaa. zingatia yafuatayo:
1.Usikubali kwenda nyumbani kwa mtu. kutana naye mahali ambapo kuna watu wengi, ili kikitokea cha kutokea, usalama wa raia unao. mgahawa, sheli, au stendi ya basi ni baadhi za sehemu kama hizo.
2. Nenda na mtu mwingine. sio lazima, ila kama una uhakika sana...
3. Fanya majaribio kabamabe: jamaa aliwahi kunituma nimtafutie computer. binafsi ni fundi, kwa hiyo sikuwa na haja ya kwenda na mwingine. nikaenda kwake, computer ilikuwa na muonekano mzuri, ila kuna baadhi ya keyboard zilikuwa haziko vizuri. nikaona itanisumbua. akanipa nyingine, sauti haikuwa poa - nikaipiga chini. mwisho wa yote, computer zote sita nilizotesti zilikuwa na kasoro. nikaondoka bila bila.
kama huna uhakika nenda na fundi. ili ujue endapo kuna issue usije ukalia kilio cha mbwa mdomo juu...
4. Ikiwezekana, beba pesa kwenye simu, au kadi ya benki, hasa kama hela ni kubwa. usije ukabeba milioni 3 kesh, kumbe jamaa kakuwekea jicho la 3...
Kama bado humwamini sana, fanya naye escrow service kwa wakili (mnawekeana saini ya yeye kupokea hela baada ya wewe kutesti kifaa, na wakili anakuwa shahidi na kusimamia zoezi zima) ili hata akikupa kitu kibovu, una haki ya kukirudisha. unaweza pia ukatumia protected sites kama ebay, ambao wana 30-day money-back guarantee - unarudhishiwa pesa zako ndani ya siku 30 endapo kifaa kitagundulika kuwa ni kibovu.
Kama huwezi kununua kifaa kipya, baadhi ya niliyoyaainisha yanaweza yakakusaidia katika kupata kile kilicho bora.
Je, kuna mbinu nyingine? Umewezaje kununua kifaa used bila kutapeliwa? Au umewahi kutapeliwa? Uzoefu wako utatupa taadhari...Naomba kusukia kutoka kwako