Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,324
- 152,136
Binadamu ni kiumbe mnafiki sana katika mambo mengi ila unafiki wa kiwango cha juu uko katika imani zetu za kidini na pengine katika siasa.Hata hivyo, leo hii nitaongelea zaidi unafiki katika imani zetu.
Wanadamu wa leo wengi wetu tunasali kama fashion tu na zaidi tunasali kwa mazoea lakini miyoni mwetu hatuna mungu bali ni wanafiki wakubwa ingawa wapo wachache wanaoheshimu imani zao.
Wakristo na Makanisa:Mtu yuko kanisani Ibada inaendelea yeye yuko busy na simu.Ibada inaendelea yeye akili haipo kanisani anawaza yake anangoja tu muda wa ibada uishe arudi zake nyumbani ilimradi tu naye leo ameonekana kuwa amefika kanisani!
Watu,wake kwa waume,baada ya ibada ndio wanapata nafasi ya kupeana namba za simu,kupanga appointment wakafanye yao.Mtu anatoka kusali akifika nyumbani kwake anakwenda kumnyanyasa mwanae wa kambo au yatima.Hawa ndio waumini wa leo ambao ukigusa imani yake atatamani akukate na shoka lakini matendo yake ni bora hata ya mpagani au mnyama.
Siku hizi makanisani michango imetamalaki na hata sadaka zimepoteza maana.Mtu anahubiri hukuu watu wanatoka mbele mmoja mmoja na kukambidhi mchungaji hela eti hii ndio sadaka au huku eti ndio kumtolea mungu!
Yanoyohubiriwa makanisani mwetu siku hizi sijui hata kama baadhi yako katika kitabu kitakatifu cha Biblia.Siku hizi kila mtu ni Mchungaji na kila mtu anajiita Nabii!Hakuna biashara inayolipa kama kuanzisha huduma za kiroho!
Baadhi ya waimba kwaya wamegeuza makanisa wanayofanyia mazoezi ya kwaya kama meeting place za kupanga appointment zao na kufanya wanayoyajua wao.
Kwa kifupi huyu ndio mkiristo wa leo ambae ukigusa imani yake iwe hapa mtandaoni au kwingineko atatokwa na povu utadhani anataka kukata roho lakini matendo yake bora hata ya ibilisi!
Waislamu na Misiki:Hawa nao wana yao ikiwemo kuzingatia swala tano.Utamkuta mtu anazingatia swala tano lakini matendo yake bora hata ya mpagani.
Mtu yuko busy na swala tano lakini mtu huyo ni mchoyo,mbinafsi,mpiga majungu,mshirikina na wakati mwingine hata kutupia wengine majini na mapepo!
Hawa waheshimiwa ikifika kipindi cha Ramadhani wanajitahidi kweli kuzingatia wanayopaswa kuyafanya lakini ngoja mfungo uishe utadhani ndio wameruhusiwa kufanya yao.
Swali ambalo huwa najiuliza ni hivi wao kuzingatia maagizo ya mwenyezi mungu ni wakati tu wa kipindi cha Mwezi Mtukufu au ni wakati wote wa maisha yao?
Hawa waheshimiwa wakati mwingine hutumia hata imani ya dini yao kudhuru wengine wakiaminiwa wako sahihi kufanya hivyo katika mazingira fulani.Kwa mfano kujilipua, n.k.Kuna mahali Mungu ameturuhusu kutoa uhai wa wengine kwa kutumia jina lake?!
Yako mengi sana ambayo binadamu huyu anaejifanya kuumia sana pale imani yake inapoguswa lakini kumbe ni binadamu huyu huyu ambae matendo yake ni mabaya na maovu kupindukia.
Kwa mfano, hapa JF ikiletwa mada ikawa na element za udini,basi watu watajifanya kutetea imani zao na kujionyesha wanaumizwa sana pale imani yake inapoguswa lakini ni binadamu huyu huyu anaetenda mambo mabaya na maovu kinyume kabisa na imani yake pasipo hata kushituka.
Hapa hapa JF,kama ilivyo huku mutaani,kuna watu kutukana na kukejeli kwa sio tatizo ila ni hao hao wanaojidai wao ni wacha mungu na wako kutetea imani yao ili hali matendo na dhamira zao ni za hovyo kabisa!
Binadamu wengi wa leo(sio wote) tunaenda misikitini na makanisani kusali kama fashion tu na zaidi ili tuonkane tunasali lakini miyoni mwetu hatuna mungu na ndio maana utakut mtu anatoka kanisani au msikiti anapita guest au masaa machache baada ya ibada anaenda kusaliti ndoa yake kwasabubu mtu huyu alikwenda kusali kama kutimiza wajibu tu lakini sio kwenda kusali kwa maana halisi ya kusali.
Mimi nasema bora hata wapagani kuliko sisi wenye dini tunaojaribu kumdanganya mungu kumbe tunajidanganya wenyewe.
Angalieni wanasiasa hawa wanaoapa kwa kutumia Biblia au Msahafu mienendo na matendo yao baada ya kuingia madarakani ndio ujue kuwa imani hizi leo hii tumezigeuza kuwa ni fashion tu ambayo kila mtu anajaribu kwenda nayo ili asionekane yuko nyuma(amepitwa na wakati).
Ni bora hawa wanyama wasio mjua mungu kuliko sisi binadamu tuliojaa unafiki mbele ya macho ya mwenyezi mungu.
Kwa mlionikejeli katika ule uzi mwingine wa "wanaosajili Jumuiya na wacheza pool" msomeni na Baba Askofu hapa itawasaidia maana in yale yale tu niliyokuwa nawajibu katika comment zangu huku mkinilaani na kunitolea lugha chafu.
Askofu wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Dar es Salaam, Dk. Valentino Mokiwa
Askofu wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Dar es Salaam, Dk. Valentino Mokiwa, ametaja majipu 10 yaliyoko makanisani na kuwataka Watanzania kujisafisha kwa kuacha mambo yasiyompendeza Mungu, ikiwamo migogoro ndani ya makanisa.
Askofu Mokiwa amesema ndani ya makanisa kuna mawe makubwa aliyoyafananisha na majipu ambayo hata Yesu Kristo anasononeshwa nayo.
Hayo aliyasema jana katika ibada ya Pasaka iliyoadhimishwa kitaifa katika Kanisa la Mtakatifu Albano, Upanga jijini Dar es Salaam.
Askofu Mokiwa alitaja jipu la kwanza kuwa ni uwapo wa mashindano makanisani, huku akisema siku hizi makanisa yanashindana kwa kuangalia kanisa lipi kubwa kuliko lingine na kanisa linamiliki shule ngapi.
Alisema: "Ushindani wa kanisa gani ni kubwa kuliko lingine, kanisa gani lina mali kuliko lingine, askofu anayeongoza kanisa fulani ni kabila fulani, na kanisa gani lina waumini wengi kuliko lingine na kanisa gani lina vituo vingi vya kulelea watoto yatima kuliko lingine.
“Imefika wakati sasa makanisa yajitathmini na kuanza kupunguza kuzungumza mambo ya nje ya kijamii na badala yake waelekezane uovu unaopatikana ndani ya makanisa,” alisema.
Jipu lingine alilitaja kuwa ni maaskofu kupigana vita. Alisema kuna tabia ya askofu mmoja kumchimba askofu mwingine, kupanga mapinduzi dhidi ya askofu mwenzake, pamoja kutukanana.
Alisema kuna tabia ya askofu kuacha eneo lake na kuingia katika eneo la askofu mwingine na kusababisha misuguano.
Jipu lingine alisema ni mapinduzi ndani ya makanisa, kuwa kuna ugumu wa moyo na kusalimiana kwa badhi ya waumini wa makanisa na kwamba waumini siku hizi wanasemana na kusingiziana, hivyo kumekuwapo kwa uongo ndani ya taasisi hizo ambazo dhima yake ni kuleta amani na furaha miongoni mwa waumuni.
Askofu Mokiwa alitaja tatizo lingine kuwa ni chuki baina ya waumini, huku watu wakiwa hawasalimiani na hawapendani, jambo ambalo hata askofu anapojaribu kuwaita na kuwapatanisha, wanakimbia kwa kutoa udhuru.
Alisema jipu lingine ni uwapo wa nguvu ya pesa kanisani au nguvu ya mtu ndani ya kanisa, ambayo inasababisha kuvurugika kwa kanisa.
Askofu Mokiwa alisema: "Kuna watu makanisani wanatumia pesa kwa manufaa yao wenyewe. Mbona hujitolei kusaidia watoto yatima? Mbona hujitolei kuwasaidi kikundi cha uinjilisti kwenda kuhubiri? Watu wa namna hiyo wana lengo la kuvunja amani."
Alitaja jipu lingine kuwa ni wizi na ulaghai na kwamba katika makanisa kuna ulaghai uliokithiri.
Jipu lingine alisema kuwa ni uwapo wa roho ya uchochezi kwa baadhi ya waumini makanisani, huku pia akitaja uwapo wa injili za kibiashara kwa baadhi ya makanisa kutumia injili kujiingizia kipato kwa kufanya miujiza.
Askofu Mokiwa alisema jipu lingine ni uwapo wa wivu na uzushi ndani ya makanisa.
“Siku hizi hayo mambo yanaitwa majipu ambayo yanasababisha kanisa kushindwa kuendelea, wakristo wanashindwa kumwona Mungu kwa sababu kuna watu waliotofauti ndani ya makanisa,” alisema Mokiwa.
MAKONDA: ATAKAYEOMBA ULINZI KANISANI KUSWEKWA NDANI
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda katika ibada hiyo aliliomba kanisa kumsaidia kutimiza wajibu wake kwa kunyoosha mienendo ya waumini wake, huku akitumia nafasi hiyo kusisitiza agizo lake la kuwataka wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhakiki silaha zao ndani ya siku 90.
“Kuanzia Julai Mosi, mwaka huu mimi mwenyewe nitaongoza msako wa kukagua silaha ambazo hazijahakikiwa. Sitakuwa na huruma, wala sitamwangalia mtu usoni,” alisema Makonda.
Makonda alisema kwa sasa jiji la Dar es Salaam haliko salama kutokana uwapo wa silaha ambazo hazieleweki.
Aliwaomba waumini wa Kikristo, ambao jana walikuwa wanaadhimisha Sikukuu ya Pasaka, kujitolea kuchangia maendeleo ya mkoa ikiwa ni pamoja na kumaliza tatizo la madawati.
“Juzi kuna mama mmoja Kimara, ni kiongozi wa kanisa, anasema kuna shughuli kanisani, anaomba ulinzi. Nikamuuliza wa nini, akasema unajua huku kuna rushwa. Nikashangaa kusikia eti kanisani napo kuna rushwa, hadi leo siamini. Sasa nasema yeyote atakayepiga simu kuomba ulinzi wa polisi kanisani namweka ndani,” alisema Makonda.
CHANZO: NIPASHE