Unafiki na Usaliti wa Mwigamba dhidi ya tuhuma za ukomo wa madaraka katiba ya CHADEMA

Utetezi wa ajabu sana huu dhidi ya uvunjaji wa katiba ya chama
mtoi, iwapo viongozi wengine waliendelea kuchaguliwa ilihali uchaguzi wao ni kinyume cha katiba, haihalalishi uvunjifu huo wa katiba uendelee milele kama de facto justification.

Haijalishi mwigamba alikuwepo ndani ya vikao au hakuwemo ndani ya vikao, so long as msajili ameona kuna tatizo ndani ya katiba ya chadema, nguvu zenu zijengeni kumshawishi msajili na umma kwamba kweli katiba yenu haina tatizo, na kwamba marekebisho/mabadiriko yalifanyika kihalali.

Slaa amewahi kukana kwamba kipengele hicho hakijawahi kuwemo kwenye katiba ya chama, nyinyi mnatwambia kilikuwemo mwaka 2004, mnajichanganya.

Vyovyote vile kama stratergy yenu ni kupambana na kina mwigamba, they have nothing to lose for now, ila mbowe na slaa wana much to lose politically. So you are fighting the wrong enemy!
 


Nimefuatilia mjadala huu kwa muda mrefu sana,lakini kwa kusoma comments za wale wenye mlengo wa kukitetea CHAMA CHA KIJANI -CCM na kuwashambulia viongozi wakuu wa CHADEMA,chama tishio la mslahi yao ya kifisadinimeona niwaulize na nitake kufahamu haya kutoka kwao kwa nia njema tu kama watapenda kujibu maana hapa si tunajadiliana bhana,au siyo?


  1. Hivi nyie ni manachama/wapenzi/wafuasi wa CHADEMA na mna nia ya kukisaidia chama kifikie malengo yake ya kushika dola la Tanganyika na Zanzibar chini ya mwavuli wa Muungano na pia kuendelea kuwa tishio kwa uhai wa CCM,chama kinachoongoza serikali sasa?
  2. Au,Je, ninyi ni manachama/wapenzi/wafuasi wa CHAMA CHA MAPINDUZI? If that is the case,kwa nini mmeshupalia mambo yasiyokuwepo tena katika chama cha watu wengine ambacho kwayo sera,itikadi,imani, pamoja na mipango na mikakati na mifumo ya utekelezaji ili kufikia malengo yao huifahamu,huielewi na kamwe hutaweza kuitetea wala kuipigania huku mkiacha kwenu kukitekea na washkaji kujivunia raslimali za nchi hii kwa mgongo wenu?......Who is behind this foolish project... the so called ".....mission demolish CHADEMA?"
  3. Au, nyie ni wapigania demokrasia pasipo na demokrasia na kwa hiyo mnaingia na kushauri kila taasisi ya aina hii kwa lengo la kuikuza hii demokrasia ya aina yenu?........If that is it, then,ushauri wangu katika eneo hili mnalolifanyia kazi (kama ndivyo) la ushauri na kukuza demokrasia ni kuwa ili mueleweke ficheni rangi zenu halisi ya KIJANI KIBICHI ili msionenakane kuwa ni wanafiki.....kuweni wana demokrasia kwelikweli ikiwa ni pamoja kukosoa sera,mifumo na utendaji kwa maana ya mipango,mikakati ya utekelezaji wa kile chama mnachokipenda cha kwenu cha CCM!!!??? .....Au hii ndiyo mikakati na mipango ya CCM katika kutekelezaji ILANI YA UCHAGUZI YA MWAKA 2010?....

Na,hebu tu-assume kuwa mmefanikiwa kumvuruga msajili wa vyama katika hili la MABADILIKO YA KATIBA YA CHADEMA ya mwaka 2006 na akawapa na kupata mnachotaka (ila kumbukeni Jaji Mtungi ameshasema tayari amegundua kuwa kuna wabaya wake wanataka kumgombanisha na CHADEMA kwani hana tatizo na CHADEMA wala Katiba yao), je uanadhani malengo ya CCM yatafanikiwa? Yasipofanikiwa mtakuja na mpango makakati gani tena??

.......Kwa sababu nina uhakika wa 1000% kuwa hawa viongozi mnaowaogopa wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa (Party National Executive General Secretary) na Freeman Mbowe (Party National Chairperson) wataendelea kuwepo na kukiongoza chama iwe kwa mvua au kwa jua mpaka tuingie katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015 tuwagaragaze tena ili mtumie tena ile mbinu yenu ya "kuchakachua" kwa kudhani kuwa MUNGU ni ATHUMANI kwamba ataendelea kuvumilia tu uharamu na uchafu ulioletwa na mfumo chini ya CCM tena na tena!!...

Kwa sababu hata sisi wanachama na wapenzi tumegungua kuwa kumbe hawa viongozi wetu wa kitaifa wanaopigwa vita kwa mbinu mara wala ruzuku ya chama kwenda Dubai na Marekani na hawara zao.......utadhani CHAMA CHA KIJANI.....CCM na viongozi wake hawana "michepuko" na hakipati ruzuku tena kubwa kuliko ya vyama vingine vyoooote na utadhani kwayo iko salama salimini wakati ndiko wizi na ufisadi ulikozaliwa,kulelewa na kukulia na utadhani kila mwanachama wa CCM anapata ka-ruzuku kake na labda pengine utadhani ile ruzuku wanayopata ma CCM inatumika kutujengea madaraja,shule na madarasa ya watoto wetu,......mara ooh Mbowe amejibadilishia katiba tena eti tangu mwaka 2006, mara ooh eti Dr Slaa mbeba wake za watu, mara oooh eti mbowe hakusoma,kilaza......na hapa unashindwa kupata picha kwa nini watani zetu CCM wamwogope kilaza asiye na shule!!,.....Mara oooh viongozi wa CHADEMA ni magaidi wa Al-shaabab au Boko-haramu tunashindwa kuelewa kuwa Maboko haram,ma al shaabab, na ma-drug dealers ni yale yaliyoko serikalini na katika chama tawala na kutumia mfumo walioujenga kwa miaka mingi kufanya uharamia wao, ndiyo maana yanaona ni hatari kwayo chama chao kuondoka katika mfumo maana woote wanaweza kuja kuishia magerezani kulipa dhambi zao ikiwa ni pamoja na kufilisiwa vyoote walivyoiiba kwa kuutumia mfumo wao haramu

Kwa sababu kumbukumbu zangu zinanirejesha na kuona kuwa karibu kila njia na mbinu zile zilizotumika nyakati zile kina NCCR na CUF wako katika fire kisiasa imeshindikana na kilichopo kwa sasa CHAMA CHA MAPINDUZI ili kiendelee kushika hatamu za uongozi wa taifa hili kinatumia mtindo wa Trial and Error (na huku kunaitwa kutapatapa) na hii ni mbaya sana kwa uhai wa chama hiki na mbaya zaidi kwa sababu hiki ndicho chama kinachoongoza nchi na siku zote siasa ni sayansi hutakiwi kubahatisha ili kufanikiwa kuendelea kutamalaki na kukubalika na umma wenye maamuzi ya kuendelea kukuweka katika utawala au kukuondoa!!

Mimi ningepewa nafasi ya kuwa mshauri wa chama hiki kizee ambacho sasa kimeshaanza kupoteza kumbukumbu, ningewaambia kuwa ili tendelee kukubalika na ili tuendelea kuaminiwa na wenye nchi basi sisi chama tawala CCM tunaongoza serikali hii sikivu na tulivu ni lazima tutekeleze ahadi zetu zilizotokana na sera zetu tulizozinadi katika ilani yetu ya CHAMA CHA KIJANI - CCM ya uchaguzi ya mwaka 2010 ambazo zote zimefungwa katika kabrasha moja linaloitwa MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA WA BARA NA VISIWANI kwa njia ARI MPYA ZIDI,KASI MPYA ZAIDI na UFISADI MPYA ZAIDI!!....Ningewaambia kuwa wananchi wataona tofauti ya CHADEMA/UKAWA na sisi CCM tunaongoza serikali kwa kuwatengezea mazingira ya kufanya masiha yao yawe rahisi!!

Kabisaaaa, ningewaambia ku deal na mtu tena mmoja Mbowe kwa jina la chama chake anachokiongoza cha CHADEMA ni kumpaisha na kukipaisha hicho chama na kamwe wananchi hawa wa kizazi hiki hawawezi kutuelewa kwa sababu hawa watanzania wa enzi hizi si wale wa enzi za ujana wa CHEYO mzee wa mapesa au Lyatonga Mrema mzee wa siku saba au enzi Ngangari na Ngunguri za CUF na Mahita......hawa ni watanzania wanaoamini katika NGUVU YA UMMA........PEOPLE'S POWER

Kabisaa, ningewaambia wana CCM wenzangu kuwa,wananchi wanatambua kwa CCM ndiyo inayoongoza serikali na ndiyo yenye jukumu la kuhakikisha kuwa kila mwananchi yu salama, anapata mkate wake wa kila siku,mfumko wa bei unakuwa chini ili kila mtu amudu kuuza na kununua,barabara za vijijini na mijini zinapitika mwaka mzima,watoto wetu wanasoma katika shule bora zenye miundo mbinu bora na yote pamoja na walimu wa kutosha na wenye ujuzi,wakulima wana motisha wa kuifanya kazi ya kilimo kama ni uti wa mgongo wa taifa hili...................

Mwisho ningewaambia wana CCM wenzangu kuwa tatizo letu si Mbowe wala Dr Slaa wala Katiba yao aidha waliibadilisha au vipi kwa sababu haituhusu, wala tatizo letu si UKAWA (CHADEMA,CUF na NCCR)......Bali tatizo letu la msingi ni kukosa mbinu na mikakati ya kuwaonesha wana wa nchi hii tofauti ya chama kinachoongoza serikali na kile kilicho nje ya serikali kama hawa sasa wanaoitwa COALITION OF OPPOSITION PARTIES FOR PEOPLES' CONSTITUTION - UKAWA......Tatizo letu kama chama kinachoongoza serikali na ambalo kila mwananchi analijua na kamwe hatuwezi kumdanganya ni ubinafsi wetu,uroho wetu,ufisadi wetu na dhuluma ya haki kwa wananchi wa nchi hii na haya ndiyo yakayotupiga chini na milele hayawezi kufunikwa funikwa kwa kila kikao chetu kumfanya FREEMAN MBOWE na CHADEMA yake kuwa ni ajenda kuu.....kwa sababu siku zote watu wanaokaa na kujadili mtu/watu ni wambea tu na ni watu walioishiwa sera....watu wa maana siku zote hujadili issues na si watu....sembuse chama chetu dume cha CCM!!?

Na ningewaambia chama chetu kinaelekea kufa lakini tuna nafasi ya kukiingiza THEATRE na kukifanyia OPERATION babu kubwa bila ya hata ya gharama ya UKAWA au MBOWE!!

CC;Ifweero,Lizaboni,MwanaDiwani,Assadsyria,Simiyuyetu, T2015CCM na Adharusi
 
Sisemi namchukia #Mwigamba ,sisemi nawachukia wasaliti (yeyote awe ndani ya CUF,NCCR,CDM,CCM,ACT,TLP,e.t.c).Ninachosema ni kuwa if he died in a train accident,i wish,I should be the one driving it!
 
CHADEMA YAANZA KUWAGAWA WAjUMBe WA BARAZA KUU wASihuDHURIe MKUTANO WA UCHAGuZI TAIFATuwasaidie wajumbe wa baraza kuu CHADEMAWanademokrasia na wananchi kwa ujumla!Kuna mipango miovu inayopangwa na wahafidhina na wasioitakia mema nchi yetu kuwazuia wajumbe halali wa baraza kuu CHADEMA kuhudhuria mkutano wa baraza kuu hapo Julai 18. Mipango hii inahusisha kuweka vikwazo vya fedha kwa wajumbe hasa masharti ya kuwarejeshea wajumbe posho ya usafiri na kujikimu kipindi chote mkutano. Hii inatishia afya ya demokrasia kwani wajumbe waliopangwa tayari akaunti zimecheka na wengine wameanza kujisogeza eneo la tukio.Hivyo basi mnaombwa kuwasaidia wajumbe kwenye maeneo yenu kwa michango ili waweze kuhudhuria mkutano huu muhimu unaokwenda kuibadilisha historia ya nchi hii. Kwa wajumbe wa baraza kuu walioathirika na unyanyasaji huu mnaombwa kutoa taarifa zenu hapa ili wana JF wawasaidie._----hizi ni mbinu za kuzidi kuchakachua katiba

Ungekuwa makini kufuatilia raslimali za nchi zinavyoliwa kama unavyopoteza muda kufuatilia wajumbe wa baraza kuu la chadema,tungekupa bigup ,jf haijawa cc ya chadema!!
 
Fungua macho kidogo walau uone! Hoja unazosema hazijabjibiwa ni zipi?!

mkuu. kwa chama kinachojinasibu kuwa ni cha demokrasia ni sawa kwa kutokuwa na ukomo wa uongozi? ina maana hamna kabisa mwanachama anaeweza kuongoza chama zaidi ya mbowe?
 
mkuu. kwa chama kinachojinasibu kuwa ni cha demokrasia ni sawa kwa kutokuwa na ukomo wa uongozi? ina maana hamna kabisa mwanachama anaeweza kuongoza chama zaidi ya mbowe?

Hakuna anaekataa au kulazimisha kuwa Mbowe na Dr slaa ,wapumuzike.chadema kama chama kinachojali miono na utashi wa binadamu kimetengeneza katiba ambayo is soo authentive participation.
Viongozi waliopo kwa mujibu wa katiba kifungu cha 6:3:2 kikowazi kuwa anaetaka kugombea tena ni ruksa,lakini kuna kanuni,miongozo na taratibu ambazo zinamtaka awe ametimiza( tizama sehemu ya maadili na miiko)
Wanaodai Mbowe aondoke tena wakitoka nje ya chadema mnalenu jambo,haiwezekani kabisa!!
Mwaka 1995-2009 mlikuwa mstari wa mbele kumtaka Lipumba aachie ngazi,Maalim seif aachie ngazi anag'ang' ania madaraka,baada ya kuleta vurugu kubwa na ccm kupita suala la ukomo wa madaraka kwa viongozi hawa mkaachana nalo,
ccm inajulikana,mnatafuta kila namna kukimaliza chadema kwa kisingizio cha Mbowe na Slaa waondoke,na kama wakiondoka hamtaishia hapo mtamtafuta Lissu,Mnyikank
Gazeti la Tazama kwa mfano kila wiki hupansikiza chuki kwa Halima Mdee na Joshua nasary lakini tatizo kubwa ni kwamba chadema iko imara na mmeacha kuisema cuf,TLP,Nccr,UDP na vyama vingine kwa kuwa mmevizoofisha
Mmeacha kumwandama Mrema kwa kuwa siku hizi ni kibogoyo.
Ccm propaganda hazitasaidia kama elimu hovyo,afya hola,kilimo hola,umeme hola ,maji hakuna wakati tuna mito?, pamoja ba propaganda chadema inakufa,mbowena slaa wezi nk hamtawaeleza kitu watanzania,si wa 1992!, nyimbo zote za propaganda mmeimba hakuna atakayezisikia mwaka 2015!!!!!
 
Wakuu.

Nimeamua kuandika kidogo kikombe kisinipite ili kuanika unafiki wa Mwigamba na marafiki zake (Kitila na Zitto), Mwigamba na maswahiba zake (viruka njia wa usaliti) ambao walisaliti ndani ya CHADEMA na baadae kuibuka na uzushi kuwa kipengele cha 6.3.2 (c) kinacho zungumzia muda wa uongozi kwenye katiba ya chama kuwa kimewekwa kinyemela. Kipengele hicho (6.3.2 (c), kinasema "kiongozi aliye maliza muda wa uongozi ana haki ya kugombea na kuchaguliwa tena mradi awe anatimiza masharti ya kuchaguliwa kuwa kiongozi"

Mwigamba anasema kipengele hicho kimeongezwa kinyemela huku akijua alishiriki/wameshiriki kwenye kuifanyia mabadiliko katiba ya chama ya 2004 na kuanza kutumika rasmi kwa katiba ya 2006 iliyokuja na kipengele hicho. Mwigamba pamoja na wajumbe wengine akiwemo rafiki yake (MM) tarehe 13/8/2006 wakiungana na wajumbe wengine wa mkutano mkuu kwa pamoja walisema "...Sisi wajumbe wa mkutano mkuu tumeamua kuifanyia mabadiliko katiba ya 2004 ya chama chetu cha siasa kinachoitwa CHADEMA ili kuipa sura inayoendana na mtazamo na msukumo mpya wa falsafa yetu ya nguvu na mamlaka ya umma na dira na dhamira ya chama kuanzia 2006 na kuendelea. Kuanzia sasa CHADEMA kitaendeshwa kwa mujibu wa katiba hii sambamba na kanuni, taratibu na maadili ya chama...". Mwigamba na Zitto walitamka kwa pamoja maneno hayo wakiwa na wajumbe wengine wa mkutano huo.

Msijiulize kwa nini kwenye hili nawaongelea wote wakati aliyepeleka malalamiko kwa msajili alikuwa Mwigamba peke yake! ukweli ni kwamba utatu huu wa kisaliti nauongelea pamoja kwenye sakata hili kwa kuwa nyendo zote chafu za kisaliti kwa sasa huwezi kuwatenga! Wanaruka pamoja, wanakutana na kupanga pamoja na mawasiliano yao makubwa pamoja na mataniboi wao wa kisiasa ni kuidhoofisha CHADEMA kuliko kuimarisha chama chao kinacho undwa na viongozi walio saliti CHADEMA. Uhakika nilio kuwa nao, watashindwa kama walivyo shindwa kupitia walicho kiita "Mkakati wa mabadiliko 2013".

Mwigamba kupitia gazeti la Mtanzania la tarehe 2/7/2014 alinukuliwa akimshukuru Mungu kwa ofisi ya msajili kwa alicho kiita "..kusimamia na kueleza ukweli wanachama wa CHADEMA kuhusu kuondolewa kinyemela kwa kipengele cha ukomo wa madaraka.." akanukuliwa zaidi akisema "...CHADEMA walinifukuza uwanachama wakiamini kuwa hoja ya kuvunja katiba niliyo iwasilisha kwa msajili itatupwa na hatimaye amejiridhisha kuwa walikuwa wamevunja katiba ya chama chao..."

Maelezo ya Mwigamba yamejaa unafiki na hadaa zilizotawaliwa na dhambi ya usaliti! Usaliti wa kukisaliti CHADEMA na sasa anajisaliti na yeye mwenyewe! Hebu msome katikati ya mstari hapa "...hatimaye msajili amejiridhisha kuwa walikuwa wamevunja katiba ya chama chao..." utadhani marekebisho hayo yamefanyika yeye akiwa tayari kashasaliti na kwenda ACT!

Kuna haja watu wajue, huyu Mwigamba alikuwa nani ndani ya CHADEMA kabla ya kufukuzwa chamani kwa dhambi ya usaliti kupitia mkakati wa mabadiliko na unafiki wa kumsifu mwenyekiti Mbowe kwa kuendesha chama kwa ufanisi na ubunifu kwenye mkutano wa kanda ya kaskazini pale Corridor Spring (Arusha) Novemba 2013 akiwa anawasilisha ripoti ya mkoa wake (Arusha) huku robo saa baadae akimkashifu na kumtukana Mh Mbowe kupitia akaunti yake bandia ya 'Mkulima maskini' kwenye mtandao wa jamiiforums.

Mwigamba alikuwa nani kabla ya kusaliti CHADEMA?

1. Mwigamba aliwahi kuwa mwanachama na kiongozi wa CHADEMA mkoa wa Arusha mpaka alipo vuliwa nafasi zake zote za uongozi Novemba 2013.

2. Aliwahi kuwa mhasibu wa chama makao makuu kuanzia 2011 hadi 2012 alipo simamishwa kazi na makao makuu kutokana na matatizo mbalimbali moja kubwa likiwa kushindwa kuleta ripoti ya matumizi ya fedha alizopewa wakati wa uchaguzi mdogo wa Igunga ambapo zaidi ya milioni 210 zilitumika.

3. Alishiriki kwenye mkutano mkuu wa tarehe 13/08/2006 uliopitisha mabadiliko ya katiba toleo la mwaka 2006 akiwa mjumbe kutoka mkoa wa Arusha (kwa mujibu wa kumbukumbu za mahudhurio).

4. Amekuwa mjumbe wa vikao vya baraza kuu la chama toka 2009 alipo chaguliwa kuwa mwenyekiti wa mkoa wa Arusha na amekuwa akishiriki vikao mpaka Nov 2013 alipo vuliwa nyadhifa zote ndani ya chama.

5. Amekuwa mjumbe wa vikao vya mkutano mkuu wa chama toka 2006 na amekuwa akishiriki kwenye mikutano mikuu mpaka Novemba 2013 alipo vuliwa nyadhifa zote ndani ya chama.

Lakini kubwa la muhimu ni kwamba, yeye na Kitila Mkumbo ndio walikuwa wanamtandao wakubwa na waandaji wa mkakati wa mabadiliko 2013 kinyume na maadili, itifaki, miongozo na katiba ya chama kwa ajili ya rafiki wao anaye kamilisha UTATU wao wa wasaliti. Lakini pia hawaja wahi kulalamika kwenye kikao chochote kuhusiana na kipengele cha ukomo wa ungozi ndani ya kikao chochote cha kikatiba.

Usaliti na hadaa za Samson Mwigamba na utatu wao wa kisaliti ni upi?!

Pamoja na kujua kuwa alishiriki mchakato mzima wa mabadiliko ya katiba ya chama yeye na rafiki yake anajua kuwa:

1.0 wapo viongozi ndani ya CHADEMA ambao waliweza kuwa na haki ya kugombea na walichaguliwa upya kwa zaidi ya vipindi viwili na hakuja wahi kuwa na mgogoro kwani katiba ya chama ilifuatwa kwa ukamilifu wake.

Viongozi hao ni nani na wanatokea mikoa na kanda ipi?

1.1. Alhaji Ramadhani Kasisiko - mwenyekiti wa mkoa wa Kigoma na rafiki mkubwa wa Zito Kabwe. (Inasemekana hata Hijjah alimpeleka yeye).

1.2. Kansa Mbarouk - mwenyekiti wa mkoa Tabora, huyu ni ndugu na Athuman Balozi (Tabora) aliyesoma tamko fake la waliojiita wajumbe wa baraza kuu na mkutano mkuu pale Lamada Hotel na baadae wakaandamana kwenda kwa msajili na CAG.

1.3. Msafiri Wamalwa - Katibu mkoa wa Kigoma.

Viongozi hawa wote watatu hapo juu wanatokea kanda ya Magharibi (Tabora, Kigoma na Katavi) ambako pia ni kanda aliyokuwa anatoka MM na Mzee Said Arfi.
Kwa maana hiyo, kama Mwigamba angekuwa na dhamira safi angemuuliza rafiki yake wa makakati wa mabadiliko aliyempa jina la MM au ange muuliza mzee Said Arfi uhalali wa viongozi hao ambao walichaguliwa zadi ya vipindi viwili.

2.0. Kama dhamira ya Mwigamba ingekuwa haiteswi na dhambi ya usaliti angejiuliza uhalali wa viongozi wengine ambao ni

2.1. Aliyekuwa mwenyekiti wa mkoa wa Singida na rafiki wa MM ambaye anaitwa
Nobert Kitundu japo alikuja kujiuzuru kutoka na sakata la MM (huyu baadae aliomba kurudi kuwa mwanachama wa kawaida baada ya kukiri kuwa alipewa hela ili ajiuzuru kwenye ule upepo wa kujiuzuru ambao baadae ulikwama).

2.2. Mwingine ni Mzee Stephen Massawe wa mkoa wa Dodoma ambaye mpaka sasa ni katibu wa mkoa wa Dodoma na alipasifa za kugombea tena baada ya mabadiliko ya katiba 2006 ambayo Mwigamba naye alishiriki mchakato wa mabadiliko yake.

Viongozi wote hapo juu wanatokea kanda ya kati yenye mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singida, kanda ambayo anatokea Dr Kitila Mkumbo ambaye ni rafiki mkubwa wa Mwigamba waliye shirikiana kuandaa mkakati wa mabadiliki 2013 na ndio wanaunda utatu wa kisaliti wakishirikiana na MM.

Kama Mwigamba hakuwa na nia ovu, kilicho mzuia asimuulize rafiki yake kwenye utatu wa kisaliti (Dr Kitila) ni nini?!

Itoshe kusema kuwa, pamoja na viongozi hao hapo juu lakini pia wapo viongozi wengine kama marehemu Philiph Magadula Shilembi ambaye naye alishika uongozi kwa kuchaguliwa zaidi ya vipindi viwili, kama mtakumbuka huyu marehemu alisha wahi kuandikiwa makala nzuri sana na MM na Mwigamba mara baada ya kifo chake. Yupo pia mzee Shilungushela kutoka Shinyanga ambaye pia mwenyekiti taifa baraza la wazee ambaye naye alichaguliwa kwa kipindi cha tatu, Shilembi na Shilungushela wanatokea kanda ya ziwa Mashariki yenye mikoa ya Shinyanga, Simiyu, na Mara.

Viongozi wengine walio chaguliwa kwa vipindi zaidi ya viwili ni pamoja na mzee Ndesamburo mwenyekiti wa mkoa wa Kilimanjaro na Mh Conchester Rwamlaza (MB) ambaye ni katibu wa mkoa wa Kagera.

Nabaki najiuliza?!

1. Kwa nini Mwigamba na utatu wake mtakatifu pamoja na mataniboi wao wa kisiasa hoja yao iwe kwa viongozi wa chama taifa wakati kipengele cha ukomo wa madaraka kama kingekuwepo kingehusu viongozi wote mpaka kwenye ngazi ya misingi, matawi, kata, wilaya na hata mikoa na si mwenyekiti na katibu mkuu taifa pekee?!

2. Kwa nini Dr Slaa ahusishwe na kushambuliwa wakati nafasi yake ya ukatibu mkuu na manaibu wake ni nafasi ya uteuzi na si nafasi ya kugombewa na kupigiwa kura?! Nini kimejificha kumuongelea Dr Slaa na wakati huohuo kumuongelea Mh Mbowe wakati mmoja anapigiwa kura na mwingine anateuliwa?! Kumbuka hata rafiki wa Mwigamba kwenye utatu wa usaliti (MM) hakuchaguliwa bali aliteuliwa na mwenyekiti kwenye miongoni mwa majina yaliyo wasilishwa kwake kwa uteuzi na hivyo akawa naibu katibu mkuu bara.

3. Kwa nini rafiki na collegemates wa MM pale udsm ambaye naye ni rafiki na Sisty Nyahoza ambaye ni mhudumu wa ofisi ya msajili waongee lugha moja na kundi lote la utatu wa usaliti kuhusu kipengele cha ukomo wa uongozi?! Lugha moja wanayoongea nikwa bahati mbaya au kuna ka mpango nyuma ya pazia kampango ambako msajili wa vyama jaji Mutungi amejikuta anaingizwa king na ameshtuka akiwa kwenye kilinge cha tope?!

4. Mbona utatu wa usaliti hauongelei mabadiliko ya bendera ya chama pamoja na mabadiliko makubwa yaliyo huisha mfumo wa chama kizima na wamejikita kwenye kipengele kimoja tu ambacho bado ni halali kama vipengele vingine wasivyo taka kuviongelea vilivyo halali?! Nashangaa kwa nini hawaongelei mabadiliko ya bendera, organisation ya chama pamoja na Redbrigade iliyopigiwa kelele na CCM ambayo haikuwemo kwenye katiba ya 2004?!

5. Kama wameamua kusaliti uwepo wao na ushiriki wao kwenye mabadiliko ya chama wakiwa na akili timamu, nani anaweza kusema kuwa watu hawahawa kuwaita kuwa ni wenye kuungana na kuunda utatu wa usaliti na kuanzisha chama chenye kuundwa na viongozi walio saliti CHADEMA hawapaswi kuitwa kwa jina lingine kuwa wao ni Alliance for Cowards and Traitors yaani kwa kifupi ACT?!

Hivi nyinyi chadema mnao udumavu wa fikra kwani nilazima kusiwepo na ukomo wa uongozi katika vyama vya siasa?
 
Hakuna anaekataa au kulazimisha kuwa Mbowe na Dr slaa ,wapumuzike.chadema kama chama kinachojali miono na utashi wa binadamu kimetengeneza katiba ambayo is soo authentive participation.
Viongozi waliopo kwa mujibu wa katiba kifungu cha 6:3:2 kikowazi kuwa anaetaka kugombea tena ni ruksa,lakini kuna kanuni,miongozo na taratibu ambazo zinamtaka awe ametimiza( tizama sehemu ya maadili na miiko)
Wanaodai Mbowe aondoke tena wakitoka nje ya chadema mnalenu jambo,haiwezekani kabisa!!
Mwaka 1995-2009 mlikuwa mstari wa mbele kumtaka Lipumba aachie ngazi,Maalim seif aachie ngazi anag'ang' ania madaraka,baada ya kuleta vurugu kubwa na ccm kupita suala la ukomo wa madaraka kwa viongozi hawa mkaachana nalo,
ccm inajulikana,mnatafuta kila namna kukimaliza chadema kwa kisingizio cha Mbowe na Slaa waondoke,na kama wakiondoka hamtaishia hapo mtamtafuta Lissu,Mnyikank
Gazeti la Tazama kwa mfano kila wiki hupansikiza chuki kwa Halima Mdee na Joshua nasary lakini tatizo kubwa ni kwamba chadema iko imara na mmeacha kuisema cuf,TLP,Nccr,UDP na vyama vingine kwa kuwa mmevizoofisha
Mmeacha kumwandama Mrema kwa kuwa siku hizi ni kibogoyo.
Ccm propaganda hazitasaidia kama elimu hovyo,afya hola,kilimo hola,umeme hola ,maji hakuna wakati tuna mito?, pamoja ba propaganda chadema inakufa,mbowena slaa wezi nk hamtawaeleza kitu watanzania,si wa 1992!, nyimbo zote za propaganda mmeimba hakuna atakayezisikia mwaka 2015!!!!!

mkuu.. chadema ya sasa hivi sio sawana ile ya mwaka 2010. Chadema ya akina zitto, slaa na mdee enzi hizo wakiwa bungeni ilikuwa.kivutio skwa watanzania wengi.. nikiri wazi tu slaa, zitto na mdee ndio wanasiasa walionifanya nifuatilie siasa, lakini baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 pamoja na kupata wabunge na madiwani wengi imebadilika kabisa, zile hoja za kusisimua zimeyeyuka, imebaki matusi ,kejeli, vurugu , unafiki , ukanda..n.k..hapo ndio shida ilipoanzia, siasa za chadema zikatoka kwa watu makini akina slaa, zito ,halima zikahamia kwa wanaharakati wakina lema,sugu, mbowe, msigwa, lisu. kwangu mimi hawa sio wanasiasa ni wanaharakati..afadhali kidogo mnyika ni mwanasiasa.siasa za udini, ukabila, ukanda zikashika kasi kubwa kama moto nyikani..siasa hizi za wanaharakati ndio zimesababisha chadema kupoteza washabiki wengi sana na kupoteza ule umaarufu wake wa zamani..na kitendo cha kumfanyia fitina zito ndio pigo la mwisho lililoipoteza kabisa chadema,, kitendo hiki kimesababisha mpasuko mkubwa sana .ndio maana nasema huu ndio muda muafaka kwa mbowe na slaa kuondoka kupisha wengine watakaokijenga chama
 
Back
Top Bottom